Hivi inakuwaje Jeshi linapotrain askari wa nchi nyingine?

Shekizongoro

JF-Expert Member
Dec 9, 2013
388
195
Wanajamii naomba kueleweshwa; leo kati ya maofisa 208 waliohitim TMA 15 sio raia wa Tanzania, mfano watano ni waganda, wanyarwanda watatu n.k; Swali ni kwamba hawa si wataenda kuwatonya mafunzo ya maofisa yetu yalivyo? (strength & weakness), mbona wamekula kiapo kumtii raisi wetu? Itakuwaje tukiwa maadui nao ndo tushawafundisha? Naomba msaada nijue huwa inakuwaje hasa tnavyotrain majirani zetu.
 

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,372
2,000
Umenikumbusha juzi kati kuna jamaa mmoja mjeda hapa kitaa ni afisa wa jeshi, alikua anasema Mawali inalalamika chini kwa chini kuwa inawezekana 50% ya maafisa wake wa Jeshi ni wa-TZ, ila kuwatambua ndio mziki mzito..

Kwenye mambo ya kijeshi hii kitu ni kawaida sana
 

MATASO

Member
Jan 4, 2012
10
0
Kaka mafunzo ya kijeshi huwa almost yanafanana hiyo ni just kubadilishana uzoefu, tukija kwenye issue ya vita hiyo ni just timing kwa nchi zinazolingana nani atamuwahi mwenzake so issue ya time vitani ni muhim sana
 

The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
15,222
2,000
Kaka mafunzo ya kijeshi huwa almost yanafanana hiyo ni just kubadilishana uzoefu, tukija kwenye issue ya vita hiyo ni just timing kwa nchi zinazolingana nani atamuwahi mwenzake so issue ya time vitani ni muhim sana

Na ndio mambo ya STRATEGY yalipoanzia huko.
 

Madela Wa- Madilu

JF-Expert Member
Mar 24, 2007
3,070
1,195
Tanzania tuna wanajeshi kibao wamesoma Urusi Canada UK na Israel.
Ninyi mnadhani wakienda huko hawaonekani wageni kama muwaonavyo watu kutoka nchi nyingine wageni kwenye chuo chenu?

Jeshi letu na Uganda yamejengwa kwa mfumo wa Kiisrael hata majina yake yanaenda UDF ,TDF
JKT nayo waliofanya utafiti wa awali ni jeshi la Israel.
 

Shekizongoro

JF-Expert Member
Dec 9, 2013
388
195
Tanzania tuna wanajeshi kibao wamesoma Urusi Canada UK na Israel.Ninyi mnadhani wakienda huko hawaonekani wageni kama muwaonavyo watu kutoka nchi nyingine wageni kwenye chuo chenu?Jeshi letu na Uganda yamejengwa kwa mfumo wa Kiisrael hata majina yake yanaenda UDF ,TDFJKT nayo waliofanya utafiti wa awali ni jeshi la Israel.
Ahsante mkuu; lakini mi nakuwa na wasiwasi kwa nchi ambazo ni jinani na wanaweza kuwa enemy mda wowote mfn Uganda na Rwanda, wala nisingekuwa na shaka sana kama hizi trainings tungewapa waphilipino, thailand n.k. Ndo maana nkauliza haiwezi kuathiri tukiingia kwenye uadui hasa vita.
 

Daddo

JF-Expert Member
Jan 17, 2013
1,409
2,000
Kati ya hao 208 unaosema kuna maafsa 4 waliofanya kozi ya uafsa Kenya wengine Uganda na mwaka jana 2 walifanyia Rwanda 4 Uganda na 4 Kenya hapo wanapata Commission ya Rais tu. Hivyo hiyo ni njia tu ya kudumisha uhusiano wa kimataifa. Jeshi ni taasisi yenye mpangilio wake mzuri ila mara nyingi inaharibiwa na wanasiasa kama tunavyosia nchi nyingine duniani. Na hii ni kutokana na kile kinachofahamika kwamba rais ndiyo amiri jeshi mkuu hivyo akitoa amri ni utekelezaji tu.
 

Madela Wa- Madilu

JF-Expert Member
Mar 24, 2007
3,070
1,195
Sisi tuna maafisa wa jeshi kuanzia Sudan, Uganda,Congo, Rwanda, Burundi, Msumbiji Angola na may be Namibia. Huko south Africa tuna wajeshi kibao wa vyeo vya juu wamefundishwa ujeshi hapa Tz.
Usiwe na hofu wala shaka. Umdhanie adui yako mkuu huenda ni rafiki yako na rafiki yako ndiye adui yako mkuu.
Isitoshe hakuna urafiki kati ya nchi na nchi. Watu binafsi kati yanchi huweza kuwa marafiki.

Ahsante mkuu; lakini mi nakuwa na wasiwasi kwa nchi ambazo ni jinani na wanaweza kuwa enemy mda wowote mfn Uganda na Rwanda, wala nisingekuwa na shaka sana kama hizi trainings tungewapa waphilipino, thailand n.k. Ndo maana nkauliza haiwezi kuathiri tukiingia kwenye uadui hasa vita.
 

nyakashenyi

Senior Member
Jan 15, 2013
139
195
Ni kawaida sana na kwa utaratibu wetu ni kuwa kabla ya Mkuu wa sasa vikosi vya hawa watu vilikuwa vinakuja kuwa trained hapa na maofisa wetu but jamaa alianzisha utaratibu wa wakufunzi wetu kwenda kuwafundishia huko kwao.Wanabaki watu kidogo kama hao wanne wanadumisha "mahusiano mema na majirani"
 

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
11,519
2,000
wanajeshi wanafanana, kuwasha mtuu wote wanajua, kinacho fanya jeshi kushinda si mafunzo pekee yake lakini ni timing na intelligence nyuma yake. mfano israel ilipo wapiga waarabu kwenye vita ya siku sita, ilikuwa ni timing based on facts from intelligence sources na sio uwezo wa wanajeshi wao pekee yake.
 

SENGE

Member
Jan 20, 2012
20
45
si wanajeshi tu. mbona hata vyuo mbalimbali hadi marais tumetoa eg uganda na DRC. so ni yale yale
 

kukomya

JF-Expert Member
Sep 20, 2011
344
195
Ahsante mkuu; lakini mi nakuwa na wasiwasi kwa nchi ambazo ni jinani na wanaweza kuwa enemy mda wowote mfn Uganda na Rwanda, wala nisingekuwa na shaka sana kama hizi trainings tungewapa waphilipino, thailand n.k. Ndo maana nkauliza haiwezi kuathiri tukiingia kwenye uadui hasa vita.
Mafunzo ya awali ya uofisa ni standard na mfumo wa mafunzo karibu sawa karibia duniani pote. Ni mafunzo ya kumpa Afisa ukakamavu, uwezo wa kufikiri na kuamua kwa haraka, uwezo wa kuwaongoza walio chini yake kwa hekima na werevu, uvumilivu na mbinu za msingi za kivita.
Hii ndiyo maana unaweza kukuta mchanganyiko katika kikosi kimoja maafisa waliochukulia mafunzo ya awali Uingereza, Canada, Monduli na hata Malawi au Kenya lakini wakifanya kazi kwa maelewano makubwa.
Hakuna hatari yoyote hapo zaidi ya kupata elimu ya misingi ya kijeshi.
Ushindi katika vita hutegemea mengi ikiwa ni pamoja na sababu, malengo, zana na werevu wa vikosi shindani.
 

conservative3

JF-Expert Member
Nov 12, 2013
998
1,000
Pia ujue kufundisha ni biashara ila kuna mbinu ambazo zinamfanya askarh wetu awe na mafunzo ya ziada hatuwez andika hapa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom