Jumax
Senior Member
- Mar 4, 2017
- 117
- 229
Habari za muda huu ndugu zangu watanzania.
Binafsi kuna jambo lina nitatiza sana kwakweli hapa nchini.
Tumezoea kusikia waziri fulani anatoa tamko au agizo juu ya jambo na baadae mkuu wa nchi anakuja kupinga au kukanusha jambo hilo. Je! Hapa ni kwamba huwa hakuna mawasiliano au kushauriana baina ya hawa watu maana wanatuweka njia panda sisi wananchi ukizingatia wote ni viongozi au ni nini haswa tatizo la hili jambo?
Mifano hai.
1. Mh Nape aliwahi kusema kuhusiana na tatizo la kushutumu watu bila kuwa na uhakika au ushahidi wa kutosha maana inapelekea kuharibu "reputation" ya mtu. Lakini baadae mkuu akasema vingine.
2. Mh mwakyembe ametoa tamko kuhusu kufunga ndo bila ya vyeti vya kuzaliwa. Mkuu pia nahili ametoa tamko la kupinga.
Sasa hapa tuelewe nini jamani, maana maisha yenyewe tu yanatuchanganya na ninyi pia mtuchanganye namna hii.