The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 3,611
- 9,269
View: https://youtu.be/8RLQbwTTqTU?si=rcVAi6NXBIxw43aW
➡️Kumbe binadamu anaweza kubadilika kutoka kuwa mtu mwema na kuwa mtu mbaya na katili sana aieseee...
➡️Kwenye video hii hapo anaonekana Hayati Rais John P. Magufuli na aliyekuwa Vice President (VP) wake by then, Bi Samia Suluhu Hassan katika kikao chao Ikulu pamoja na viongozi waziri Jaffo na katibu mkuu TAMISEMI wakipewa maelekezo na boss wao namna ya kuwa - handle wamachinga ktk miji mbalimbali...
➡️Nimempenda sana Hayati Rais Magufuli hapa kwa moyo wake wa kuonesha kujali maslahi, utu na ubinadamu wa watu wengi wa maisha ya kiwango cha chini na kati wanaohangaika kujitafutia riziki katika ardhi zao badala ya tajiri na mwekezaji mmoja anayependelewa na baadhi ya viongozi wachache kiasi cha kuamua kufukuza maelfu ya wakazi wa eneo au kijiji fulani eti ili apewe mwekezaji mmoja tajiri...
➡️Hii video inathibitisha uzalendo na sehemu ya ubinadamu wa Hayati Rais Magufuli aliyekuwa akipenda rasrimali za nchi tulizopewa na <Mungu ziwanufaishe Watanzania kwanza.
➡️Kinachoshangaza ni Bi Samia Suluhu Hassan aliyekuwa VP wakati huo, Sasa ni Rais kamili wa Tanganyika. Lakini ghafla kageuka na kawa sio Samia Suluhu wa wakati huo anayeonekana kukuitikia kila point ya boss wake.
➡️Leo Bi Samia Suluhu Hassan huyu katugeuka kabisa Watanganyika. Hili somo na Magufuli analopewa hapa kumbe halikumwingiaka kabisa akilini mwake. Samia huyu Leo ndiye dalali mkuu wa rasrimali asili zetu zote kwa wajomba zake waarabu wa Dubai na Oman.
➡️ Samia huyu kauza bandari zetu zote za Tanganyika kwa waarabu wa Dubai. Kauza misitu, mbuga zetu mamilioni ya hekari kwa wajomba zake waarabu wa Oman. Ni kwanini huyu mama wa Kizanzibar kageuka na kuwa katili hivi kwa Watanganyika..?
➡️Najiuliza hivi ni kwanini Samia yuleyule aaliyekuwa VP wa Magufuli ni tofauti na Samia Rais wa Tanganyika ya Leo? Amekula maharage ya wapi huyu mama yaliyombadilisha na kuwa katili hivi...?