Hivi huyu mwanamke nimkubali au nimkatae?

Changes boy

JF-Expert Member
May 17, 2017
552
362
Kuna mwanamke nilisoma nae Chuo alinipenda sana kwa kuwa life Chuo lilikua sio zuri nikampotezea sikutaka demu kipindi hicho, sasa Niko mkoa mwingine mbali nae ila kila upuuzi wangu anausapoti mpaka sasa naona kama simfai atafute mwanamme anayemfaa, ajawai kuwa na mwanamme anajieshimu kwao kuna hela za kutosha kitu ambacho kinaniogopesha zaidi, juzi kunamzigo wangu ulikua umekwama sehemu akanisaidia ukafika halafu akatupia picha ya sehemu mzigo wangu ulipokwama wala hajaongea chochote kuhusiana na mzigo wala sikumwomba msaada. Kila nikiwasiliana nae nahisi furaha ananichangamkia kwelikweli, hapa najishauli nimukubalie halafu anashida na mtoto kwelikweli ambacho kinaniogopesha life halipopoa maana kwao wanadini sana, lazima ndoa ifungwe mapema naona nitaaribu plan zangu.
 
Kwahiyo wewe ulitaka wa aje mkuu? Umepata anaekupenda, anaekujali na anaekupa furaha na kutabasamu unaomba ushauri kama umkatae. Vijana mnafeli sana aisee.

Ona kaka, hebu achana nae hakufai huyo. Mwanamke gani anakupa furaha kila wakati? Yaani mtu mzigo wako umekwama anajitolea kukusaidia hata hujaomba msaada, piga chini fastaaaaa. Baharia lazima usumbuliwe na demu, lazima demu akuzingue ndio mzuri huyo. Huyu hakufai mwana piga chini huyo.
 
mwanamme ukizidiwa hela na mwanamke Mara nyingi uhusiano haudumu hicho kinaniogopesha sana, ila ni mwanamke classic flani hivi
 
Hayo ni mawazo yako ndugu wapo wenye pesa lakini wanawaheshimu waume zao. Huku kwetu kuna mwalimu aliolewa na fundi ujenzi lakini anamheshimu sana mume wake. Mwanamke akikupenda hata angekuwa na hela kiasi gani lazima atakuheshimu tu.
 
pamoja mkuu
 
Back
Top Bottom