mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,722
Tunavyojua Watumishi wa Umma hawapaswi kujihusisha na siasa. Kuna kipindi huyu ndugu alitipitia Misukosuko hadi kutikisa ajira yake kisa kujihusisha na mambo ya CHADEMA. Nadhani alibadilika ndio maana akawa hadi prof. Hadi kesho nilijua Mkumbo ni Mshauri(Consultant) wa ACT wazalendo na kazi hiyo sidhani kama ni siasa bali ni ya kitaalam.
Kuteuliwa kwake na Rais kelele zimezuka kana kwamba amechukuliwa Kiongozi nguli wa Upinzani, Wengine wanalalamika Rais anaua Upinzani, Wengine Mchumia tumbo au Kibaraka wa CCM, Ninaowaelewa moja kwa moja ni wale wanaomlalamikia kwa kusaliti maoni yake juu ya Waadhiri kuteuliwa, Ingawa ninaamini ameisaliti kwa faida ya taifa.
Tunaanzia wapi Kusema Mpinzani huyu ndugu?
Au ameteuliwa akiwa kama nani?
Mpinzani, Mwalimu wa chuo na mtumishi wa Umma, Mwanasiasa machachari, Mshauri wa mambo ya kisiasa?
Ninaomba wajuvi wa haya mambo mnitoe tongotongo tusijekuwa tunapiga kelele kwa vitu ambavyo havipo...