GE2020 Hivi huyu Kiliba ni msemaji wa CCM au ni Rais wa TAHLISO, majukumu yake anayetekeleza kweli ipasavyo?

GE2020 Hivi huyu Kiliba ni msemaji wa CCM au ni Rais wa TAHLISO, majukumu yake anayetekeleza kweli ipasavyo?

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
844
Reaction score
1,604


Akiwa Mkoani Kagera leo Jumanne Oktoba 14, 2025, Mwenyekiti wa Kampeni ya Kitaifa ya Mama Asemewe Bw. Geofrey Kiliba amesema Ushiriki wa Vyama 18 kati ya 19 katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 pamoja na mamilioni ya Watanzania wanaohudhuria mikutano ya kampeni za Vyama mbalimbali vya siasa nchini ni dhihirisho la kufeli kwa nia ovu ya baadhi ya watu waliokuwa wakieneza chuki na hamasa ya kususia uchaguzi.

Kiliba ameyaeleza hayo wakati akitoa tathmini ya Taasisi ya Mama Asemewe kuhusu Kampeni za uchaguzi huo, akisema watu hao waliokuwa wakihamasisha wananchi kususia uchaguzi walifika pia kwenye Taasisi za elimu na Jumuiya zake pamoja na kwa Viongozi wa dini nchini bila ya mafanikio, suala ambalo sasa limedhihirisha ukuu wa Mungu na mapenzi ya Watanzania kwa nchi yao.

"Hawa wahuni wamekataliwa na zaidi ya Taasisi 56, wamekataliwa na Watanzania, wamekataliwa kwetu Wanavyuo, wamekataliwa na wafanyabiashara wadogo, maafisa usafirishaji (Bodaboda na Bajaji) na wamekataliwa na Taasisi makini za kidini zinazotulea.

“Ninaamini kuwa hii vita tutaishinda kwa data na takwimu kwasababu Tanzania yetu ipo chini ya Mikono salama ya Mwenyenzi Mungu,” amesema Bw. Kiliba.

Aidha, Kiliba pia amezungumzia madai ya hivi karibuni ya kulihusisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ na siasa za Tanzania pamoja na tukio lijalo la uchaguzi Mkuu wa Tanzania, akisema kuwa Vijana wa Tanzania hawana hofu wala wasiwasi kwani Vyombo hivyo vya ulinzi na usalama vinao uwezo wa kuwadhibiti na kushughulika na watu hao aliwaoita kuwa wahuni wasioitakia mema Tanzania na watu wake.
 
Kuruka kwa Maharage ndo kuiva kwake

CCM wamechanganyikiwa.

Jeshi haliwataki, wenye akili TISS hawawataki.


Kila mwenye akili nchi hii ameshajua chanzo cha kukwama kwetu ni hawa wajinga na wapuuzi CCM

Ndo mana saivi wanaishia kuwalipa wachawa iki kuendesha propaganda za kipuuzi.


Haya yote mwisho wake ni Oktoba 29
 
Back
Top Bottom