Hivi huwezi piga rangi gari bila kupiga puti?

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,109
18,326
Nilipeleka gari kwa fundi anipigie rangi, sasa baada ya kupiga rangi kweli gari lilipendeza na rangi ikawa na mng'ao mzuri sana kiasi kwambanunaweza jiona sura yako.

Baada ya kama mwaka hivi rangi imefubaa na sehemu nyingine inatoka na inabakia rangi nyeupe.

Mara ya kwanza nilidhani ile nyeupe ni rangi ya mwanzo lakini gari toka litoke japani halijawahi pigwa rangi nyeupe.

Mtu mmoja akanimbia hiyo nyeupe ni puti ambayo huwa wanaweka kuzima sehemu zilizo bonyea zikae sawa.

Lakini nikajiuliza mbona rangi original hata uikwaruze huwezi ona kitu cheupe?

Kwanini hawa mafundi wanaweka maputi mengi badala ya kutumia muda mwingi kunyoosha.

Je, tatizo ni nini? Hakuna vifaa?

FB_IMG_1593358373802.jpeg
 
Inategemea unapiga palipochubuka, muda gani baada ya kuagiza gari. Kama gari umeshakaa nalo mwaka mmoja, lazima rangi ya awali ianze kutokuwa na mng'ao kama wa mwanzo.

Kwahyo ukipiga sehemu iliyochubuka tu, GARI ITAKUWA NA MABAKA MABAKA, kwa sababu sehemu uliyopiga rangi itakuwa inang'aa kuliko sehemu zingine.

Hapo ndo utalichukia gari zima...!!
 
Magari mengi yanayouzwa yard hapa bongo kutokea Japan yamepigwa rangi,ukitaka kujua zinapigwa rangi pitia garage za Morocco ndo utaelewa!

Wananunua magari ya Bei rahisi na yenye ubora mdogo hasa yaliyopata accident na kuja kuyakarabati na kutuuziwa! Hata Japan kwenyewe unatakiwa kuomba status ya gari kabla ya kuagiza ili kujiridhisha kama limepigwa rangi au laa kabla ya kununua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom