Hivi huwa wana apa au kuapishwa ili iwe nini?

JERUSALEMU

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
3,112
3,536
salamu wanajamvi!
Ni kuigiza au kufuata walivyo kuwa wanafanya watangulizi wao au kwasababu wazungu wanafanya? Nimefuatilia kwa muda mrefu sana lakini nimeona huku kuapa au kuapishwa hakuna maana mbele ya wananchi na mbele ya MUNGU.Ile KATIBA na kitabu cha MUNGU huwa wanaviacha palepale wanapo apia kamwe hawabebi chochote kichwani.

Jiulizeni, Makonda aliapa? aliahidi mbele ya Rais na mbele ya MUNGU ya kuwa atakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa watu wake! lakini leo hii ni mtumishi wa umma anaye tuhumiwa kwa mambo mengi machafu pengine kuliko wote. Anatumia vyeti fake, amevamia ofisi za watu kwa mitutu ya bunduki usiku wa manane kwa nia ovu, amepokea magari ya kuhongwa! rushwa, lakini bado katika ofisi ya umma! kuapa kwake kulikuwa na faida gani?

Jiulizeni, Rais Magufuli aliapa na kutuahidi watanzania na MUNGU wetu na wake utumishi ulio tukuka, lakini kutumia fedha za umma bila Bunge kupitisha ni sawa? anashindwa nini kuitisha Bunge la dharura ili lipitishe matumizi hayo? Hotuba zake nyingi siku hizi ni kutisha watanzania, je, huko siyo kwenda kinyume na kiapo chake? kuongeza makato kutoka asilimia 8 hadi 15 kwa wanufaika wa mikopo wakati wanasoma elimu ya juu bila kuwaandaa wahusika ndio utumishi ulio tukuka?

Rais Magufuli amezuia kwa makusudi kabisa watumishi wa umma wa TAMISEMI wasihame kwa muda wa miaka miwili sasa hata kama wanajilipia gharama za uhamisho, je huko siyo kuwakomoa kwasababu zisizo julikana? watumishi wa serikali kuu wana hama bila shida yeyote, kwanini anabagua watumishi wa umma? kuapa kwake kulikuwa na maana yeyote?

Nchi inahitaji maendeleo ya watu kwanza ndio tuje kwenye maendeleo ya vitu kama viwanda. leo hii kila mtanzania analalamika maisha magumu.hivi tulikuchagua ili utuletee maisha magumu? kwa mara ya kwanza wanafunzi wanao somea masomo yanayo hitaji mafunzo kwa vitendo kama walimu, madaktari, wahandisi, masoroveya(surveyors) hawataenda! Utumishi ulio tukuka ni kuona kuwa taasisi mbalimbali zinafanyakazi kwa mujibu wa kuanzishwa kwake tena kwa kiwango.

Dr Mwakyembe juzi aliapa kuifuta TLSkama Tundu Lissu akichaguliwa kuwa Rais wao.Jiulize aliapa kuja kukiuka sheria au kutekeleza sheria? kuapa kwake si ilikuwa mbwembwe na kupoteza fedha za umma?

Siku hizi manung'uniko kuwa wateule wengi wa Rais wanatoka kanda moja,Jambo hili siyo zuri kwani lina haribu umoja na amani kazini.

Tukiapa basi kiapo chetu kiwe cha kweli na tuiheshimu KATIBA na MUNGU tuliye muahidi kuwa tutakuwa watumishi wema.
 
Kuapa ni Formality. Hazina athari yoyote kwa asiyeapa. Kwa waumini wanaoapa wakaenda kinyume Na viapo mambo bado yanawanyokea.
 
Kuapa ni Formality. Hazina athari yoyote kwa asiyeapa. Kwa waumini wanaoapa wakaenda kinyume Na viapo mambo bado yanawanyokea.
Sasa kwanini tupoteze muda na fedha kwa jambo ambalo absolutely wahusika hawata tekeleza?
 
Kuapa ni Formality. Hazina athari yoyote kwa asiyeapa. Kwa waumini wanaoapa wakaenda kinyume Na viapo mambo bado yanawanyokea.
Mfano makonda Daudi mpaka sasa kaenda kinyume na kiapo kwa asilimia 80% anawatukana watu, anawabambikia kesi, anawapora magari, anashinda ikulu kupiga majungu kinyume na kiapo chake cha kufanya kazi kwa mjibu wa Katiba
 
Sasa kwanini tupoteze muda na fedha kwa jambo ambalo absolutely wahusika hawata tekeleza?
Pesa ya umma kwa awamu hii ya tano inapotelea kwa mambo ya hovyo hovyo yasiyo na tija, Pesa za Safari za nje na pesa yote ya kubana matumizi inatumika kudhoofisha upinzani huku Lipumba akila pesa ndefu, zingine hutumika kuwapa wabunge wa CCM wakwamishe miswada ya Wapinzani bungeni na zingine sasa zinatumika kumlinda makonda Daudi, Tanzania ni Nchi ya vioja kwa sasa.
 
Hivi mtu hawezi kuapa maramoja na ikatosha katika awamu flani? Mf katika awamu hii Mwakyembe ameapa mara ngapi?
Na pia kiapo kingefanyiwa marekebisho kidogo, waweke na tahadhali kuwa "Mungu na wananchi wanisamehe pale nitakapokengeuka na kushindwa kutekeleza kiapo changu maana wengi wanaishia kukengeuka na kufanya kinyume
 
salamu wanajamvi!
Ni kuigiza au kufuata walivyo kuwa wanafanya watangulizi wao au kwasababu wazungu wanafanya? Nimefuatilia kwa muda mrefu sana lakini nimeona huku kuapa au kuapishwa hakuna maana mbele ya wananchi na mbele ya MUNGU.Ile KATIBA na kitabu cha MUNGU huwa wanaviacha palepale wanapo apia kamwe hawabebi chochote kichwani.

Umesahau wameongeza kiapo kingine kinaitwa cha maadili 'integrity pledges'.

Naona wangeongeza mstari kwenye maneno ya kiapo kuhusu 'shetani'.

"... because even the life is so temporary, lakini Tanzania yetu sio temporary, itaendelea kuwepo ... is supposed to be there permanently".

Sayansi na maandiko ya dini tofauti zinasemaje kuhusu haya madai ya Tanzania kuwepo permanently? Hivyo vitabu vya dini wanavyoshika hapo vinasemaje kuhusu Tanzania kuwepo permanently?
 
Hivi mtu hawezi kuapa maramoja na ikatosha katika awamu flani? Mf katika awamu hii Mwakyembe ameapa mara ngapi?
Na pia kiapo kingefanyiwa marekebisho kidogo, waweke na tahadhali kuwa "Mungu na wananchi wanisamehe pale nitakapokengeuka na kushindwa kutekeleza kiapo changu maana wengi wanaishia kukengeuka na kufanya kinyume
You are a great thinker.Actuary wote baada ya muda huwa wamekengeuka.madaraka yana levya!
 
Mfano makonda Daudi mpaka sasa kaenda kinyume na kiapo kwa asilimia 80% anawatukana watu, anawabambikia kesi, anawapora magari, anashinda ikulu kupiga majungu kinyume na kiapo chake cha kufanya kazi kwa mjibu wa Katiba
Halafu anakwambia ni mwakilishi wa mungu hapa Dar es salaam!!
 
Back
Top Bottom