Hivi huwa ni nuksi, balaa, laana au?

Hivi huwa ni nuksi, balaa, laana au?

Hornet

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Posts
26,892
Reaction score
52,491
Katika maisha ya kila siku unakuta mtu anahangaika na anafanya Kazi kwa bidii sana ila hana maendeleo.

Akifanya Kazi wiki wiki mbili anatimuliwa bila kosa.

Akishika pesa tatizo linatokea either ugonjwa,kifo ajali n.k.

Akitafuta Kazi anaona mafanikio ikifikia kuitwa anapigwa kiswahili..
inaenda kwa miaka na miaka mpaka kuzeeka.

Hii huwa ni kawaida ama laana ama ni kitu Gani?

Na kuna namna Gani ya kujiepusha na hali kama hii?
cc MziziMkavu, Yericko Nyerere, Kiranga, @ pasco.
na wengineo
 
Last edited by a moderator:
Aisee kwa mitazamo hii itakuwa ngumu sana kukomesha swala la ushirikina na imani potofu za uchawi. Maana hata Yericko Nyerere anaamini ukipata definition ya uchawi basi umepata definition ya uafrica
 
Sometimes the frequency of coincidences may be tempting you into witchcrafty.

Don't let your mind stoop that low.

Always, take a positive perspective: May be its a clear message from your God telling you not to pursue what your on currently. Try something different entirely! Such hurdle may be the clues into discovering your true potential, keep on keeping on trying something new if the previous one didn't work out. Its like a combination lock, keep on turning until the tumblers fall into place.

Kama kila alieshindwa,kuharibikiwa,kupoteza angewaza along the lines of laana,mikosi,kisirani etc, dunia ingekua nyuma bado.

Katika maisha kuna watu wanayapatia maisha kilaini tu kama kumsukuma mlevi, ila wengine lazima jasho la meno liwatoke ili kieleweke. Its just the way it is. Stop assuming you are one of those who will get it easily, so when it doesn't come easily unaanza kuwaza laana,mikosi. Believe in: you are one of those destined to get it the hard way, and muscle up!

Good luck
 
katika maisha ya kila siku unakuta mtu anahangaika na anafanya Kazi kwa bidii sana ila hana maendeleo.
akifanya Kazi wiki wiki mbili anatimuliwa bila kosa.
akishika pesa tatizo linatokea either ugonjwa,kifo ajali n.k.
akitafuta Kazi anaona mafanikio ikifikia kuitwa anapigwa kiswahili..
inaenda kwa miaka na miaka mpaka kuzeeka.
Hii huwa ni kawaida ama laana ama ni kitu Gani?
na kuna namna Gani ya kujiepusha na hali kama hii??
cc MziziMkavu, Yericko Nyerere, Kiranga, @ pasco.
na wengineo

Hapa pananihusu,,,,kukutwa na majanga ya kufukuzw several times, bila concret reason inatokea kwa watu wengi. Ngoja nijifunze zaidi mshana jr pita hapa kidgo.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu hiyo siyo laana wala mikosi! Ni kwamba kila mtu MUNGU alimuumba kwa namna yake ktk kufanikiwa,kutafuta,n.k.Binafsi huwa ninaamini kuwa ninapopatwa na jambo fulani liwe baya au zuri,ni mpango wa MUNGU;TUANZE NA UPANDE WA UBAYA;Ktk maisha sisi binadamu huwa tunakuwa na matarajio yetu,hivyo hata km tunasoma,tunasoma kwa kulenga jambo fulani huko mbeleni,lakini kwa bahati mbaya unakuta juhudi zako zote zimeishia patupu,mf.lengo lako ni kuwa daktari,lkn kumbe MUNGU yeye anataka uwe mwalimu,je unadhani kitakachotokea hapo ili kubadili uelekeo wako kitakuwa kizuri au kibaya? bila shaka ni kibaya,ambapo utaishia kulaumu kuwa una Mikosi au laana kumbe siyo.Mfano mwingine ni wa kufukuzwa kazi,MUNGU hupenda kutumia matukio ya kuumiza ili kukupa kitu fulani chema baadae,fatilia habari za Yusufu aliyeuzwa na ndugu zake,je,una dhani yeye hakujisikia vibaya? lkn baadaye alilia kivulini.Fatilia hbr za Ayubu jinsi alivyopata pigo la kusikitisha,lkn baadaye alilia kivulini.Ukiona umefukuzwa kazi bila sababu maalumu ujue kuwa ulipokuwa sipo MUNGU alipokupangia,MUNGU hawezi kushuka kutoka mbinguni na kukuambia hebu acha kazi hiyo,La hasha! yeye hutumia matukio kukuondoa pale ulipo na kukupeleka sehemu nzuri zaidi.Sema kutokana na ubinadamu wetu unakuta mtu anabaki kulaumu sababu ya kutokujua mipango ya MUNGU KWETU.Ni km vile mtoto mdogo akiondolewa na mzazi wake ktk eneo hatari hubaki analia,bila kujua kuwa mzazi ana nia nzuri ya kumwokoa.
TUJE UPANDE WA UZURI,Wapo watu ambao ktk maisha yao walijaliwa na MUNGU kila anachokifanya anafanikiwa kwa asilimia kubwa,akianguka basi ni kidogo tu! hao nao ni namna yao jinsi MUNGU alivyowajalia na watu kama hao MUNGU anakuwa amewaumba hivyo kwaajili ya kuwafaidia wengine,mf.kwa TZ kuna watu wenye mafanikio km akina MENGI,ambao huwafaidia wengine kwa kutoa ajira na misaada kwa wahitaji mbalimbali.MUNGU HUMJALIA KILA MTU KADRI YA MAPENZI YAKE,UKIANGUKA KAMWE USISEME UNA MKOSI BALI MWOMBE MUNGU AKUONYESHA NAMNA SAHIHI YA KUFANIKIWA KTK SHUGHUKI ZAKO YAWEZEKANA HUKO ULIKO UNASHINDWA KUFANIKIWA KWA SABABU SIYO SEHEMU AMBAYO MUNGU ALIKUPANGIA.
 
Mi naona maisha ni kama bahati nasibu tuu. Kuna watu wanapata na kuna watu wanakosa. Na hakuna maelezo yoyote ya msingi ya kwanini watu fulani maisha yanawanyookea na wengine yanagoma zaidi ya kuwepo sehemu sahihi kwa muda sahihi. Mi nilichokiona:
1. Kuna watu wanapambana saana na maisha - wanafanikiwa
2. Kuna watu wanapambana sana na maisha - hawafanikiwi
3. Kuna watu hawapambani wala nini - wanafanikiwa
4. Kuna watu hawapambani - hawafanikiwi!
5. Kuna watu wanafanikiwa mwanzoni -mwishoni wanalosti
6. Kuna watu wanasota saana mwanzoni - mwishoni wanafanikiwa. N.k.
 
Katika maisha ya kila siku unakuta mtu anahangaika na anafanya Kazi kwa bidii sana ila hana maendeleo.

Akifanya Kazi wiki wiki mbili anatimuliwa bila kosa.

Akishika pesa tatizo linatokea either ugonjwa,kifo ajali n.k.

Akitafuta Kazi anaona mafanikio ikifikia kuitwa anapigwa kiswahili..
inaenda kwa miaka na miaka mpaka kuzeeka.

Hii huwa ni kawaida ama laana ama ni kitu Gani?

Na kuna namna Gani ya kujiepusha na hali kama hii?
cc MziziMkavu, Yericko Nyerere, Kiranga, @ pasco.
na wengineo

sasa ukifukuzwa kazi unalalamika?
si ujiajiri?
the most complex mechanism ever known in the world history is the mind so make use of it fully.

hakuna cha nuksi, mkosi wala gundu your future is in your mind.
 
Last edited by a moderator:
Mi naona maisha ni kama bahati nasibu tuu. Kuna watu wanapata na kuna watu wanakosa. Na hakuna maelezo yoyote ya msingi ya kwanini watu fulani maisha yanawanyookea na wengine yanagoma zaidi ya kuwepo sehemu sahihi kwa muda sahihi. Mi nilichokiona:
1. Kuna watu wanapambana saana na maisha - wanafanikiwa
2. Kuna watu wanapambana sana na maisha - hawafanikiwi
3. Kuna watu hawapambani wala nini - wanafanikiwa
4. Kuna watu hawapambani - hawafanikiwi!
5. Kuna watu wanafanikiwa mwanzoni -mwishoni wanalosti
6. Kuna watu wanasota saana mwanzoni - mwishoni wanafanikiwa. N.k.

Mf. Mimi
 
Hata wasio amni Imani za kishirikina kuna kitu kinaitwa 'karma wanakiamini

Jitahidi kuwa mtu mwema sana,hasa jizuie kudhulumu watu mali zao na haki zao
utafanikiwa tu in the end

mikosi ipo hasa inasababishwa na dhuluma.....

cc Pasco
 
Last edited by a moderator:
anatimuliwa bila kosa?
something wrong here!

inawezekana akatimuliwa bila kosa si unajua tena mambo ya binadamu chuki binafsi, majungu, fitina lakini point ya msingi ni je hana plan B ?
tatizo wabongo wamejaaliwa kulalamika!
 
Hata wasio amni Imani za kishirikina kuna kitu kinaitwa 'karma wanakiamini

Jitahidi kuwa mtu mwema sana,hasa jizuie kudhulumu watu mali zao na haki zao
utafanikiwa tu in the end

mikosi ipo hasa inasababishwa na dhuluma.....

cc Pasco

true story, like attracts like ukipanda ubaya utavuna ubaya and the contrary is true!
 
Last edited by a moderator:
Hata wasio amni Imani za kishirikina kuna kitu kinaitwa 'karma wanakiamini

Jitahidi kuwa mtu mwema sana,hasa jizuie kudhulumu watu mali zao na haki zao
utafanikiwa tu in the end

mikosi ipo hasa inasababishwa na dhuluma.....

cc Pasco

Mkuu mbna kuna mtu alikuwa anadhulumu sana kuibia watu viwanja ilikuwa kawaida yake lkn amefanikiwa balaa apo inakuwaje
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mbna kuna mtu alikuwa anadhulumu sana kuibia watu viwanja ilikuwa kawaida yake lkn amefanikiwa balaa apo inakuwaje

Theory hiyo ni ndefu
unaweza kumuona kafanikiwa kipesa lakini labda hana
'amani ya moyo' na furaha
au labda alio wa dhulumu ni wezi wakubwa kuliko yeye

sometimes kama kila mtu mwizi...the least mwizi anapata nafuu
 
Ndugu yangu hiyo siyo laana wala mikosi! Ni kwamba kila mtu MUNGU alimuumba kwa namna yake ktk kufanikiwa,kutafuta,n.k.Binafsi huwa ninaamini kuwa ninapopatwa na jambo fulani liwe baya au zuri,ni mpango wa MUNGU;TUANZE NA UPANDE WA UBAYA;Ktk maisha sisi binadamu huwa tunakuwa na matarajio yetu,hivyo hata km tunasoma,tunasoma kwa kulenga jambo fulani huko mbeleni,lakini kwa bahati mbaya unakuta juhudi zako zote zimeishia patupu,mf.lengo lako ni kuwa daktari,lkn kumbe MUNGU yeye anataka uwe mwalimu,je unadhani kitakachotokea hapo ili kubadili uelekeo wako kitakuwa kizuri au kibaya? bila shaka ni kibaya,ambapo utaishia kulaumu kuwa una Mikosi au laana kumbe siyo.Mfano mwingine ni wa kufukuzwa kazi,MUNGU hupenda kutumia matukio ya kuumiza ili kukupa kitu fulani chema baadae,fatilia habari za Yusufu aliyeuzwa na ndugu zake,je,una dhani yeye hakujisikia vibaya? lkn baadaye alilia kivulini.Fatilia hbr za Ayubu jinsi alivyopata pigo la kusikitisha,lkn baadaye alilia kivulini.Ukiona umefukuzwa kazi bila sababu maalumu ujue kuwa ulipokuwa sipo MUNGU alipokupangia,MUNGU hawezi kushuka kutoka mbinguni na kukuambia hebu acha kazi hiyo,La hasha! yeye hutumia matukio kukuondoa pale ulipo na kukupeleka sehemu nzuri zaidi.Sema kutokana na ubinadamu wetu unakuta mtu anabaki kulaumu sababu ya kutokujua mipango ya MUNGU KWETU.Ni km vile mtoto mdogo akiondolewa na mzazi wake ktk eneo hatari hubaki analia,bila kujua kuwa mzazi ana nia nzuri ya kumwokoa.
TUJE UPANDE WA UZURI,Wapo watu ambao ktk maisha yao walijaliwa na MUNGU kila anachokifanya anafanikiwa kwa asilimia kubwa,akianguka basi ni kidogo tu! hao nao ni namna yao jinsi MUNGU alivyowajalia na watu kama hao MUNGU anakuwa amewaumba hivyo kwaajili ya kuwafaidia wengine,mf.kwa TZ kuna watu wenye mafanikio km akina MENGI,ambao huwafaidia wengine kwa kutoa ajira na misaada kwa wahitaji mbalimbali.MUNGU HUMJALIA KILA MTU KADRI YA MAPENZI YAKE,UKIANGUKA KAMWE USISEME UNA MKOSI BALI MWOMBE MUNGU AKUONYESHA NAMNA SAHIHI YA KUFANIKIWA KTK SHUGHUKI ZAKO YAWEZEKANA HUKO ULIKO UNASHINDWA KUFANIKIWA KWA SABABU SIYO SEHEMU AMBAYO MUNGU ALIKUPANGIA.

Aiseee umeongea kweli tupu. Nakubaliana na maneno yako. Sababu Mungu akisema ndiyo hakuna wa kupinga hata mchawi hawezi hivyo tuamini tu ni mipango ya Mungu ila tumwombe atuwezesha kuepukana nayo kama ji mabaya.
Sawa na waluozaliwa kwenye familia maskini au nchi maskini. Yaani toka anazaliwa ni shida tu hadi mwisho, siyo laana ila mungu kaweka makundi tofautitofauti kwa namna anayoona inafaa sasa wenye nafasi ni jukumu la kysaidia wasionazo.
 
Sio laana hiyo hizo ni changamoto tu za maisha kwani si wote wanafanikiwa kwa kupita njia iliyonyooka na wakati mwingine yote hayo yanayotokea ni sehemu ya mafanikio kinachotakiwa ni kuchukulia kama dharula tu hizo kwani hata hao wanaopata fedha na kuzitumia unaweza ukakuta background yake haikuwa nzuri na yeye alipitia kwenye magumu kupita hata huyo hivyo kinachotokea hapo ni matumizi sahihi ya kile anachokipata kwa kuwa tayari alishatengeza idea kibao za kupambana na umasikini kipindi kile yupo kwenye magumu hivyo inapokuja suala la kupata fedha tayari anaiwekeza sehemu sahihi. Tulio wengi kipindi tupo kwenye magumu hatutumii muda pia wa kutengeneza idea mbalimbali vichwani hata kama hatuna kitu na ndio maana unakuta mtu amesota miaka 3 anakomaa kutafuta ajira na fedha na bado hazipatikani anakuja kupata kazi analipwa kiwango kizuri ajabu akipigwa chini anakuwa hoi na kurudi kule kule alikotoka hata kama amefanya kazi miaka mitano.
 
ukiona umefukuzwa kazi Mshukuru Mungu inawezekana kakuepushia kubwa zaidi ya hilo, siku ikifika imefika tu hakuna akujuaye zaidi yake yeye aliyekuumba
 
Aisee kwa mitazamo hii itakuwa ngumu sana kukomesha swala la ushirikina na imani potofu za uchawi. Maana hata Yericko Nyerere anaamini ukipata definition ya uchawi basi umepata definition ya uafrica

mtazamo UPI? haukufundisha matumizi ya alama?
 
Back
Top Bottom