Hivi huu utapeli bado unawaumiza watu kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi huu utapeli bado unawaumiza watu kweli?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Hofstede, Sep 30, 2009.

 1. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Nimepata email, kwenye official email yangu ambayo ni highly secured na sijui jamaa wameipata vipi, ila imeingia kama "SCAM". Ninachotaka kufanya ni kushare na watu na kuwatahadharisha kuwa japo utapeli huu unaonekana kama umepitwa na wakati ila bado kuna watu wanalizwa sana tu chukua tahadhari.

   
 2. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Utapeli wa namna hii bado upo; mimi pia juzi juzi nimeletewa barua na jamaa toka South Africa anasema kuna Rand millioni nyingi anataka azitume kwenye akaunti yangu halafu atanipa mkato kidogo!! Nimemtolea nje; hawa jamaa nadhani wanafikiri watu bado wamelala wanaweza kuwaibia kiulaini!!.
   
 3. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  ah..hawa jamaa wanawala wazungu kwa kwenda mbele. Juzi niliona mmoja analia alifunga safari hadi nigeria. Alafu kuna mpya nyingine imekuja kwenye hizi social sites, sana sana hi5 kama bado unatumia. Utaona mtu anakuomba urafiki, alafu ananza stori za yeye kuwa mkimbizi, sijui umtumie dola kiasi gani aweze kuondoka kambini. Ujinga mtupu!
   
 4. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Unajua hii kitu bado ipo, kuna mtu ninamfahamu mpaka leo tunamuita "Ambassador" jina la utani. Aliwahi kutumiwa mpaka diplomatic entry clearance ya SA aliuza kila kitu akawa na kama USD$ 20,000 azipeleke SA ili awe Tanzania branch directior wa biashara, kilichomuokoa ni Idara ya uhamiaji ya SA, walimshitukia kuwa iweje diplomat wa aina yake asafiri na basi badala ya ndege. Wakamuweka chini na kumtaka awaambie ukweli kwani wanaweza kumsaidia. Akawaambia jamaa wakamwambia huko anakoenda ni kitongoji cha uhalifu na huenda akifika basi hata maisha anaweza kupoteza badala ya kuibiwa tu. Jamaa akageuzia mpakani.
   
Loading...