Hivi huu mzuka hua tunautoa wapi ?

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,779
Punde hivi nilikua kwenye duka la Muhindi, nikinunua chupa ya chai.
Nikamwambia dosi "nipatie thermos" akaniuliza
"nataka ile kuba au dogo , au ile kati ? Ile kuba iko beba kombe 12"
Nikamjibu
"mimi taka ile kuba"
Mara ghafla akatokea mzee mmoja akawa anamwambia yule Muhindi
"Dewji iko jambo wewe, toto, mama ote jambo?"
Hapo ndipo niulizalo lilipoanzia si mimi tu , kunitokea nishawasikia watu wengi waongeapo na watu wenye lafdhi flani kama hiyo ya kihindi , kimasai, kiarabu hutokea wakaiga kiswahili chenye lafdhi ya anaeongea nae!
Huu mzuka wa kuongea kiivo huwa watoka wapi?
 
Judgment,Bora namie ntapata majibu,maana kuna watu nawajua,wakiongozana na wazungu,basi ndo hata salam za kikwetu hawajui,wao ni, 'jambow..au habaree'au hapana juwa mimi' teh teh
 
Automatic click,ndio maana kuna wanaomshambulia Hashim akiongea kiswahili kwa shida......

St. Paka Mweusi, bora yeye anaishi udhunguni. Kuna wale hata Kenya hawajafika ila akiambiwa tu yule Mkenya, hata asimjue, basi ndo kiswahili kisha-change ghafla! Lol
 
Tujifunze kuwa sisi.Wewe ni wewe you can't be otherwise.Ila nami nimeathirika si umeona nimechanganya kiwahili na kizungu.
 
Back
Top Bottom