Hivi huu mchezo wapinzani hawauoni au ndio uhovyo wenyewe wa Upinzani TZ.

kajekudya

JF-Expert Member
Sep 24, 2015
2,469
4,904
Tangu Mfumo wa vyama vingi uanze hasa kwa upande wa Rais wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania, kuna mchezo ambao vyama vya Upinzani vimekuwa vikichezewa na Chama Tawala a.k.a CCM, Chama dora na dubwasha lililoshindikana Africa nzima na duniani kwa ujumla.

Mchezo wenyewe ni huu, kuanzia kwa Augustino Mrema 1995, Prof.Lipumba 2000, Freeman Mbowe 2005 na Dr. Slaa 2010, CCM wanahakikisha kila uchaguzi mpya wanaibuka na Mgombea mpya kwa upande wa upinzani. Mgombea huyo hutengenezwa na kupewa nguvu na mvuto bandia kiasi kwamba anamu outshine Mgombea aliyetoka kuwatoa jasho na matumaini yote ya wapinzani yanahamia kwake.

Kama nilivosema watu hawa hupewa nguvu na mvuto bandia ambao CCM wenyewe wanajua hauwezi kuwasumbua watakapoingia naye kunako dimba la uchaguzi.Mwaka pekee ambao Mgombea wa Upinzani ali maintain na pengine kuipandisha ni 2010-2015 ambapo kiukweli Dr. Slaa alizidi kuwa juu na tunaweza kusema aliendelea kubaki na mtaji wake wa kura wa 2010 na ulikuwa umeongezeka mno hadi kufikia 2015, lakini kilichotokea wote tulibaki na mshangao usio kifani.

Sasa Mzee wa safari ya matumaini akatisha Sana, kura Millioni sita kibindoni, wailokunywa bendera ya chama hadi leo wanaamini alishinda Babu Lubuva akamchakachua kama walivokuwa wakisema kwa Dr.Slaa 2010-2015.

Cha ajabu huyu mtu mwenye mtaji wa 6 milioni votes( zinaweza zikawa haziko hivo as to the moment due to different reasons) sasa hawamtaki, wanamtaka Tindu Lissu.

Kwa wale wenye kumbukumbu Mara tu baada ya Uchaguzi wa 2015 kulikuwa na nguvu kubwa sana
ya kuhakikisha Lowassa anakosa fursa ya kuilinda nguvu yake na mvuto aliotoka nao kwenye Uchaguzi mkuu, ni katika kipindi hicho ndipo alipoanza kuibuka shujaa mpya Tundu Lissu, huyu ndiye akawa anapimana ubavu na Raisi, mpambano ukahama ghafla kutoka Kati ya Magufuli na Lowassa hadi kuwa Kati ya Magufuli na Lissu.

Guyss this wasn't co-encindence, ni mpango uliosukwa ukasukika, yaliyotokea baada ya hapo wote mnajua, Lissu yupo Europe na ukweli ni kuwa Lowassa na Lissu kwa sasa ukiwalinganisha, Lissu anaonekana kuwa na mvuto kuliko Lowassa, Lissu ameshamaliza kazi aliyotengenezwa kuifanya pengine bila hata yeye kujijua, kazi ya chama dora, dubwasha hili.

Sasa ni wazi 2020 Mungu akitujalia na akamjalia Rais Magufuli na akamjalia Tundu Lissu, basi mchuano ni Kati ya hawa wawili, lakini ukweli Lissu Ni kinyago ambacho kimechongwa na wazee wenyewe, amepewa nguvu na mvuto bandia, 2020 atagombea na matokeo tunayajua, atashindwa, baada ya hapo naye atachongewa kinyago kingine kitakachomfanya asahaulike kufikia 2025.

Upinzani unazidi kufanya kosa lile lile, ningekuwa Lissu ningepambana kuufanya huu mvuto na nguvu bandia nilizopewa kuwa za kweli ili 2025 niingie nikiwa Mbichi.
 
Back
Top Bottom