GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Kwanini Watu wote ( kasoro Mimi ) tukipanda Daladala tukikaribia kushuka Vituo tunavyoshuka hata kama tupo jirani ( pua na mdomo ) na Dereva lakini wote tutahangaika kupaza sauti zetu kwa Kondakta aliyepo nyuma au mbali yetu kidogo.
Je hii hali inaashiria nini? Ni sahihi abiria wanavyofanya au ndiyo pengine uthibitisho wa matatizo yetu ya kufikiri?
Hebu tulijadili hili kwa kina kwani binafsi ninapoona abiria wakifanya hivi huwa nahisi kuwa wana uwendawazimu fulani hivi kichwani kwani haiwezekani Dereva ambaye ndiyo anajua mbele kulivyo na anaendesha gari unaacha kumwambia akushushe na unahangaika kumwambia Kondakta tena kwa kupiga kelele kuwa akushushe.
Uwanja ni wenu katika " kutiririka " zaidi nikijua kuwa kati ya Members 330,000 tuliopo humu JF wanaotembelea magari yao binafsi wakizidi sana ni 23 tu lakini wote 329,977 ni full kupanda Daladala 24 / 7 ( ukibisha basi tu unataka bundesliga " ubishi " na mimi usiyo na maana ) ila ukweli ndiyo huo.