Hivi huku ni kujivuna au?

Dejane

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
50,269
70,663
Kuna mkaka kanunua gari used ya kawaida tu lakini kabadilika jamani.

Najiuliza angenunua yale magari mazuri haswa kama Range, BMW, sijui ingekuwaje nahisi angepaa.

Zamani alisalimia kila kila mtu sasa hivi hasalimii anajikweza sijui anaona kamaliza kila kitu. Sasa si angeacha kuwa kusalimia tu toka zamani.

Kwanini ubadilike si watu lazima watakusemaa, zamani alijichanganya na watu sasa hivi sijui anajionaje..

Sitaki kumhukumu aisee huwezi jua yaliyompata. Maana kuna rafiki yangu walikuwa wanaongea sana na kuchangamkiana siku hizi siyaoni hayo kama hamjuii ahahahahah..
 
Kuna mkaka kanunua gari used ya kawaida tu lakin kabadilika jamani,,zamani alisalimia kila kila mtu sasa hivi hasalimii anajikweza sijui anaona kamaliza kila kitu ,,,,sasa si angeacha kuwa kusalimia tu toka zamani ,,kwanini ubadilike si watu lazima watakusemaa,zamani alijichanganya na watu sasa hivi sijui anajionaje sitaki kumhukumu aisee huwezi jua yaliyompata .
Maana kuna rafiki yangu walikuwa wanaongea sana na kuchangamkiana siku hizi siyaoni hayo kama hamjuii ahahahahah
Huyo kaka yupo humu?

Au ulimuomba lift akakausha? (Kidding)
 
Kuna mmoja alipata kazi jaman wootee waliomsaidia akawaona hawana maana,kuja kusalimia ndugu mpaka awe na nguo mpya,simu au pochi mpya kuja kuwakonga napo hakai sana anaaga na visababu mara ooh nina kikao mahali,mara nafatilia dili la hela sehemu.
 
ukinunua gari ukapita kitaa ukiwapa hi wadau lazima waseme unaringa ukifunga vioo ukapita kimya kimya ndio kama hivi....ila sijajua sisi waswahili tatizo letu ni nini?
Tatizo wakati huna gari ulisalimia na kuwapa hi washkaji umenunua gari lako tena la kawaida tu ndio husalimii kwanini toka zamani usalimiee?
 
13706814_1016356755168049_1708937023_n.jpg

Weka picha.


swissme
 
Tatizo wakati huna gari ulisalimia na kuwapa hi washkaji umenunua gari lako tena la kawaida tu ndio husalimii kwanini toka zamani usalimiee?
shida iko hivi jamaa angeendelea kusalimia waswahili wangeanza kumsema anaturingishia, na wengine kama mimi tungesema jamaa mshamba wa gari kila akipita anapiga honi na kusimama......dawa ni kupita kimya kimya
 
Tatizo wakati huna gari ulisalimia na kuwapa hi washkaji umenunua gari lako tena la kawaida tu ndio husalimii kwanini toka zamani usalimiee?
Hivi niwaulize; unaweza kuendesha Gari km 6 ukawa unasalimia kila unayeonana naye?
 
Hivi niwaulize; unaweza kuendesha Gari km 6 ukawa unasalimia kila unayeonana naye?
Hiv hujawah ona mtu yupo ndani ya gari akapungia mkono watu,,mbona zamani alisalimiaa angeacha toka zamani ,,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom