Hivi huko serikalini kuna nini?

Mlachake

JF-Expert Member
Oct 13, 2009
4,412
4,559
Waungwana mnaofanya kazi serikalini hebu Tupeane Hints!! Nina mshkaji mmoja kila zinapotoka kazi za hazina ananishauri ni apply! with much Emphasis!! mbona huo mshara wa TGS D naona kama mdogo sana. hivi haya maisha nitayamudu kweli? just have a look!!

Monthly house rent....... Tshs 250,0000
fuel.................................... Tshs 180,0000
food.................................. Tshs 300,0000
others (viwalo, bia,..... ) Tshs 280,0000

Waungwana mnasemaje?
 

Embu weka sawa maelezo yako:

Huo mnyumbulisho ulioubandika hapo juu ndo huo mshahara wa TGSD, au ndio vile ambavyo wewe unatumia kwa mwezi?

Napata wazo kwamba wewe tayari una kazi mahala pengine, ambapo unapolinganisha unaona hailipi!!

Kama kwa mwezi unatumia kama ulivyoonyesha, huna sababu ya kuacha kazi yako mahala unakofanya sasa hivi, endelea tu mtuwangu.
 
Waungwana mnaofanya kazi serikalini hebu Tupeane Hints!! Nina mshkaji mmoja kila zinapotoka kazi za hazina ananishauri ni apply! with much Emphasis!! mbona huo mshara wa TGS D naona kama mdogo sana. hivi haya maisha nitayamudu kweli?
Ndugu yangu ngoja nikueleze ukweli, huku Serikalini huwa hatuuishi kwa kutegemea mshahara.
Serikalini kuna Posho mbalimbali ambazo zinatufanya tuishi vizuri, inategemea tu upo kitengo gani, sasa hapo hazina ndo fedha zooote za serikali zinapotoka unaogopa nini? shauri yako.
Ukiogopa mshahara wa serikali, Kamwe hutaionja asali ya nchi hii.
 
Kwani mzee wewe ni mfanyakazi wa serikali?
 
kaka nipo nafanya kazi NGO moja Hapa TZ. n hayo actually ndo matumizi yangu kwa mwezi. (roughly)
 

Usiniambie kuwa wewe ni sehemu ya watu wanaokula hela za serikali kwa njia ambazo sio za halali, nadhani watu hao ndio tunataka kuwaweka pembeni ili tuanze na clean slate. Kuna harufu ya wizi, rushwa nk katika hii statement yako.Mwalimu atasema nini yeye atakula wapi, daktari naye atakula wapi, zimamoto atakula wapi, mfagiaji wa serikali atakula wapi. Jamani uzalendo na mapenzi ya nchi yetu yameenda wapi, huna tofauti na meremeta, richmond, dowans, radar, gulfstream, EPA etc
 
 


Wana JF, Huyu mtu wa hatari sana!

Ni wa kumwogopa kama ukoma!

Yaani unasema wazi UFISADI WAKO HAPA JAMVINI?
WE HATE YOU, BAHATI YAKO HATUPAJUI KWAKO!
 
 
Nchi hii ya tanzania.
Ukipata chance kula kitu kizima ndio utaheshimika.
ukiwa muungwana na mwaminifu=UMASKINI
Hakuna atakaye kukumbuka na hutaheshimiwa.
Mfano angalia wazee wetu waliokuwa waaminifu leo hii WAKO WAPI?
 
Nchi hii ya tanzania.
Ukipata chance kula kitu kizima ndio utaheshimika.
ukiwa muungwana na mwaminifu=UMASKINI
Hakuna atakaye kukumbuka na hutaheshimiwa.
Mfano angalia wazee wetu waliokuwa waaminifu leo hii WAKO WAPI?

umenena kaka
 

"Ndugu yangu hujaeleweka,uliitaji msaada au kuongelea mishara ya serikalini,au ulitaka kuonyesha kuwa mshahara wako ni mmkubwa kiasi hicho make, kama matumizi matumizi yako tu ni zaidi ya milioni moja sasa unatafuta nini serikalini.Kaa private sector foever,kama matumizi yako ni hayo.Private sectors is where u can dare to such expenses for a month.I can see that ur monthly house rent only,can pay a proffesiional engineer in the government sector as well as a doctor .So dont dare,stay where u are, and never talk about this.
 
Wana JF, Huyu mtu wa hatari sana!

Ni wa kumwogopa kama ukoma!

Yaani unasema wazi UFISADI WAKO HAPA JAMVINI?
WE HATE YOU, BAHATI YAKO HATUPAJUI KWAKO!


Jamani hata mkiambiwa ukweli hamtaki.
Sasa mnataka mdanganywee tuuu. Bora huyo kakaueleza kwamba usijaji kitabu kutokana na cover, ingia ndani uone uzuri wake.,

Mi nampongeza jamaa kwa kutoboa siri.
Watanzania tunafichana mnoo, ndiyo maana ufisadi ukashamiri kwa sababu kila kitu ni siri. Siri imetutafuna mpaka inatuimaliza.
 
 
sijawahi kuajiriwa serikalini
lakini ajira za kule naambiwa zinashawishi ufisadi ndo maana mpaka karani wa serikali ni fisadi au fisadi mtarajiwa.....
 

Mkuu, nadhani mlachake hajataka kuonyesha kuwa mshahara wake ni mkubwa kwa sababu kusema kweli kwa maisha ya DSM (napata hisia kuwa yupo dar) hayo ni matumizi ya kawaida kwa mtu asiye na njia za kufanyia ufisadi ili kukidhi matumizi na mahitaji mengine.

Mfano hapo hajaweka matumizi ya vitu kama vocha za simu, hajaweka mchango wa harusi (siku hizi elfu hamsini ndogo), hajaweka ada za shule kama ana mdogo wake, wazee kutoka kijijini hawajambomu, kwa sababu kwa hiyo bajeti ya 'mengineyo' bado haitoshi kama akiamua kuweka kila kitu

Kinachoshangaza ni kuwa mfanyakazi wa ngazi ya TGS D, ana matumizi hata makubwa kuliko hayo (kwa kuangalia aina ya maisha pamoja na vitu wanavyomiliki kama magari, viwanja/nyumbank) na ndipo tunapomegewa siri kuwa kuna huu 'ufisadi' wa posho mbali mbali ambazo huwa hazikatwi kodi na wala hazionyeshwi kwenye pay slip ( I guess hata kwenye mkataba wa kazi kama huwa upo)

kweli private sectorutaona mshahara mkubwa lakini inakuwa mainly form hand to mouth kwa vile hakuna mianya ya posho ki vile kama serikalini!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…