Samia atosha tukutane2030
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 17,169
- 48,681
Nigusie kwenye issue mbili tu kutazama udhaifu uliopo ndani ya viongozi wa CHADEMA, LISSU excluded. LISSU namheshimu sana na kumpenda. Hana sifa za kuishi kwa fedha chafu. Ni mzalendo kweli kweli ingawa anatumia mbinu za 1960 kupigana 2025. Hatofanikiwa.
Issue ya kwanza: KESI YA LISSU
Wana CHADEMA hasa viongozi huiita kesi ya mchongo, ambayo imetengenezwa na serikali kuidhoofisha CHADEMA.
Kwanini CHADEMA imekubali kuhusika kwenye kesi hii ikiwa kesi hii inaendeshwa na mahakama ya Tanzania ambayo hao hao CHADEMA hawajawahi kuwa na imani nayo?
Moja ya kilio cha CHADEMA ni kwamba Tanzania muhimili mmoja kati ya mitatu unakula mihimili mingine.
Yaani CHADEMA ilishindwa kusema au kuamua kuwa hatutajihusisha kwa jambo lolote kwenye kesi hii kwa kuwa kesi hii ni haramu?
Awali CHADEMA ilitoa mawakili wengi , CHADEMA wanahudhuria kila siku mahakamani. Kwa kufanya hivi mnaipa nguvu mahakama kuendeleza hii kesi mpaka pale itakapothibitika CHADEMA haina nguvu na ushawishi katika jamii.
Na sasa tayari CHADEMA haina nguvu na ushawishi katika jamii kama zamani.
Angalieni kwenye social media reactions za wananchi kwenye post inayohusu CHADEMA halafu linganisheni na zamani
CHADEMA itakosa nguvu zaidi na zaidi, kwa kusema hivi sijamaanisha kuwa wananchi wanaipenda CCM. Wanaweza kuichukia CCM lakini wasiipende CHADEMA.
Issue ya pili: Kesi ya mgawanyo wa mali za chama
Hapa ndio kabisa wamepuyanga.
CHADEMA walitakiwa wakubali mgawanyo wa hizo mali sawa na Zanzibar ila wangehakikisha kule Zanzibar kuna watu sahihi wa kuzisimamia na kuongeza moto wa siasa.
Hii kesi wenzao wanaitumia kuwapiga stop kila wanapotaka kuinuka.
Je, ikiwa kesi hii ikachukua miaka 5 bila kwisha hali itakuwaje?.