Hivi Hospitali ya Amana wanafanya biashara gani kwa hivi vichanga vyetu?

kinywanyuku

JF-Expert Member
Jul 13, 2015
3,563
2,628
Wadau Habari za jumapili,

Wiki iliyopita Jumatano mke wa ndugu yangu alipata uchungu wa kujifungua tukamuwahisha Hospital ya Amana; baada ya kufika walichelewa kumuhudumia halafu alipojifungua tu huyo mtoto walichelewa kumsaidia akanywa maji machafu toka kwa mama yake baadae wakamchukua mtoto wakamwekea mashine halafu na kwenda naye kusikojulikana, baada ya saa moja wakajatupa taarifa mtoto kafariki maiti ipo mochwari.

Dah! Inasikitisha sana yaani mwanamke kabeba mimba miezi tisa halafu kuna usanii kama huu, tena siku hiyo zaidi ya watu kumi na tano usiku walipoteza watoto. Kuna jamaa mkewe alijifungua mapacha wakafariki wote kwa uzembe huu.

Hivi wadau, hakuna mamlaka ya kwenda kuwachongea hawa wanakula kodi zetu bure ila wanatufanyia unyama kama huu humu kulikuwa na thread nyingi za kuwalalamikia
 
Hizo tuhuma zako una ushahidi nazo?watoto 15 kufa kwa usiku mmoja?na wote ni uzembe?
Wewe ni mpuuzi ni wa kupuuzwa
 
Hata mwananyamala ni hivyo hivyo!
Inasikitisha sana!

Kuna Mdogo wangu na mimi amefanyiwa hivyo hivyo mtoto akanywa maji kutokea msasani Kanywa maji wakamuweka kapelekwa mwananyamala mtoto akafa

Hili swala inabidi wananchi tupaze sauti serikali ipate kuamka na kuliangalia kuna tatizo kubwa sana.

Mtu atajifunguaje na nesi tu bila daktari hata wa dharura?

Kwanini kusiwepo na standby Dokta masaa 24/7 ?

Kwanini wanaruhusu kujifungulia kwenye zahanati pasipokuwa na daktari?

Kwanini?

Uchungu ulimshika kwa muda mrefu hadi tukashauri aje daktari wa dharura kama vipi amzalishe kwa operation maana chupa imepasuka lakini mtoto hatoki!

Yani hata mama kupona ni Mungu ilikuwa hatari kubwa sana.
 
Back
Top Bottom