Nadhani hapa kitu cha kujiuliza ni:
1. Je kuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa Manji ni fisadi papa?
2. Kwa kumtetea Manji, Marando anavunja katiba ya chadema?
Kuhusu kula hela za Manji sidhani kama hilo ni kosa, kwa sababu Marando anakula kwa jasho lake halali; mbona hata Yanga anatoa mamilioni ya pesa na ninyi wengine ni washabiki wa timu hiyo na mnamshangilia na wala sijawahi kusikia hata siku moja mtu akilalamikia hilo.
Suala hili tunatakiwa kuliangalia kwa marefu na mapana yake. Unakumbuka ishu ya marehemu Dito? Kulikuwa na ushahidi wa kutosha kabisa kuwa aliuwa, Zombe alkadhalika lakini bado walikuwepo mawakili waliowatetea kuwa hawajaua.
So suala la Marando usiliweke kirahisi namna hiyo.