Hivi hii ni kwa walimu tu?

Trubetzkoy

JF-Expert Member
Oct 31, 2018
298
542
Nchi yetu ina siasa za hovyo sana!

Jana viongozi wakuu watatu wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) Mwenyekiti, makamu Mwenyekiti na katibu wao walifanya ziara katika halmashauri fulani mkoani Njombe. Jambo la kushangaza na kustaajabisha ni kwamba walimu wote wa kike (sina uhakika kama ni wa shule za msingi pekee au hadi sekondari) walilazimika kuhudhuria mkutano huo kwa amri ya Afisa elimu huku wakipewa vitisho vikali kwa yeyote ambaye hatahudhuria.

Ifahamike kuwa kabla ya ujio wa viongozi hao wa chama walimu walishapewa taarifa na kutakiwa kuwa sehemu ya maandalizi ya tukio hilo.

Kama hiyo haitoshi walimu wote wa kike walielekezwa kushona sare zenye rangi ya CCM, nembo ya CCM na picha ya Rais. Inasemekana lengo la mkutano huo lilikuwa ni kusifu na kupongeza juhudi za Rais Samia.

Jana asubuhi walimu hao waliacha majukumu yao ya kufundisha na kusahihisha daftari za watoto na kutumia mchana mzima kusifia na kuimba nyimbo za chama.

Hili jambo limenistaajabisha sana nikabaki kujiuliza hivi walimu wote ni ma-kada wa chama hicho?, Je sheria za utumishi zinasemaje kuhusu siasa na kazi?.

Nilitamani pia kujua ikiwa hii kadhia iliwakumba walimu pekee au na watumishi wa kada zingine walihusika. Nikatamani pia kujua ushiriki wa walimu wa sekondari, hata hivyo maswali yangu sikuyapatia ufumbuzi.

Nimesikitika sana!
 
acha wivu wa kike una ushahidi kuwa walilazimishwa?
 
Back
Top Bottom