Hivi hawa wasanii wetu ni vipi?

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
13,096
22,625
Awali ya yote naomba kuweka wazi kuwa mimi si mshabiki wa chama chochote cha siasa ila ni mtanzania na raia wa kuzaliwa wa nchi yangu tukufu ya TANZANIA.........

Leo nimeona haja ya ushiriki wa wasanii wetu kutoka tasnia za muziki na maigizo katika kampeni za mwaka huu. Kwa jicho la kinafiki unaweza kusema wanafanya hivi kwa mapenzi ya chama ambacho kila m'moja anachagua kukishabikia.......lakini kwa jicho la uwazi bila chembeya uongo ni kuwa hawa wasanii kwa asilimia zote wapo hapo kwa maslahi ya kipesa kitu ambacho sita walaumu sana kutokana na ugumu wa kupatikana pesa katika uchumi wa leo hapa nchini uliokithiri. Wengi wao kwa asilimia kubwa ni vijana wadogo na pengine wanaupeo mdogo sana kuhusu muelekeo wa siasa zetu na ombwe la uongozi bora linalokuwa kila kukicha......

Miaka ya tisini kwa wale mliokuwepo mtakumbuka pale south afrika katika harakati za uhuru wasanii kama Lucky dube.......pati shange.......Ivyon chaka chaka.......na wengineo wengi walitenga sehemu kubwa ya ushairi wao kuimba maneno ya ukombozi kwa jamii yao.....iwe ni kwa kificho au wazi wazi...........ila waliimba kwa sauti ya umoja kupinga uonevu na ukosefu wa haki katika jamii yao. Hapa Tanzania hali ni tofauti kidogo..........hakuna mkoloni mweupe tena ila wanaoleta shida ni rangi moja na sisi na wa asili moja na sisi.....yaani waafrika watanzania wenzetu (our kind)......ni ile story ya m'mbwa kala m'mbwa...

Najiuliza hivi hawa wasanii katika mtazamo wa kuipenda Tanzania na jamii kwa ujumla........wanahisi ni sahihi kwa wao kukaa mbele ya umati wa watanzania ambao wanawaamini.....wanawafuatilia.......wanaiga maisha yao muda mwingine.......wanawasikiliza ........na kuwashawishi kuwa ni sahihi kumchagua kiongozi mtendaji mzuri lakini ambaye ametokea kwenye genge la wasaliti wasio hata na chembe ya uzalendo......wafilisi rasilimali......wasiojali hatima ya raia......wanaohisi wao ni kwanza TANZANIA baadae....... Hivi kweli?!

Fiddy Q kwenye mashairi yako katika siri ya mchezo si ulizungumzia kuhusu serikali ya DUBU na M'MBWA MWITU wanaoshambulia kondoo.......au sio wewe....?! Leo hao followers wako wote wakueleweje......?!

Nimesikitika sana........nilitegemea wasanii mngekaa mliko kuwa siku zote za kupuuzwa na kuanza kuipa jamii ya TANZANIA mawazo hasi sasa......ili tubadili mfumo huu wa kinyonyaji wa makaburu weusi tunao waachia wakituburuta kila uchao........MUNGU anawaona......na ninawaombea yawakute mnayostahili........underground wapo wengi sana na watakuja......khaaaaaaa!

Yaaani m'mekazana mnapotosha uma kuwa hilo genge ambalo limekuwa linatubadilishia maneno tuh na kauli mbiu ni la hadhi ya juu na mwajua fika kuwa hali si hivyo........kwani nani asiyejua vitu vinavyofanywa na hao jamaa hadi leo mjifanye vipofu na viziwi kutojua nini kinazungumzwa hapa.......huo ni unafiki wa hali ya juu......uarabuni mngenyongwa ulaya mngefungwa ....mbinguni mngechomwa kwa huo unafiki.........daaaaaah.

Naishia hapa ila nimegundua kuwa jamii yetu bado iko nyuma sana hadi kukifikia kile kizazi cha mabadiliko chanya ya kimaendeleo.......kwa kuwaona tu hawa wasanii ndio bureeee kabisa..........hamna kitu........!
 
mi na amini Tanzania bado kabisa. kubadilika au tuseme kurudia katika maisha yale yazamani kwamba kwa mfano shule ni bure kama zamani madaftari peni penseli kila kitu kiwe bure kwa upande wa elimu. kwa hapo kwanza. ingeweza kufanya tu badilike. we leo hii nchi yetu kuna kijimfumo flani ivi ambacho na amini kabisa mfumo huu umechangiwa haswa na ccm kufanya mazoea kwa kua washa tuzoea kama ukitaka matibabu mazuri una enda hosiptali binafsi.shule nzuri kwa mwanao nako mpeleke binafsi.ajira watu wamesoma vizuri nako waende kwenye makampuni binafsi Ni kitu ccm wametuwekea kua yani kuna maisha ya feki na maisha orijino kweli ccm wame tu fikisha pabaya leo hii umeme tuna fua gesi bado wanatafuta sababu ili unafu usionekane kisa wana jua kua kitu kikishapanda bei hakishuki bei. nchi yetu Tanzania nzuri sana sema raia na uongozi wetu wote kwa ujumlaa hatujielewi kabisa nasema hatujielewi tukubali tu katae
 
Back
Top Bottom