Hivi hawa wana lengo zuri na mimi?

Hivi hawa wana lengo zuri na mimi?

jakackseru

Senior Member
Joined
Mar 15, 2014
Posts
132
Reaction score
27
Kuna binti tulipendana kwa kipindi kirefu mpaka hapo kulipotoke sababu ya kutufanya tuishi pamoja japo sio mimba. Tumeishi wote huu mwaka wanne, siku hizi kimezuka tabia kila tunapopishana kauli hata kama ni kwenye simu basi anaondoka na kwenda kwa shangazi yake.

Akiwa huko nakuwa sijui mpaka ninaporudi nyumbani ndipo nakuta hayupo na simu yangu haipokelewi tena, ingawa ni sehemu ya karibu ambayo ni gari moja na nauli ni mia nne tu. Lakini huyo shangazi yake humpokea na kukaa naye hata wiki pasipo kunitaarifu na wala kuuliza kulikoni huko alipotoka.

Nimeivumilia hii tabia lakini inazidi kadri siku zinavyokwenda. Siku moja nikaamua kumtolea uvivu japo ni mtu mzima. Nikamuuliza kwamba, Je, huwa anajitafakari kwa hayo anayoyafanya? Alichonijibu siwezi kukiaandika humu.

Wadau naombeni ushauri wenu je hivi ndivyo tunavyotakiwa kuishi na mabinti wa siku hizi?
 
Mmmmmhhhhh im loosing there she gat she gat you gone...! Wanaanzaga hivo hivo mdogo mdogo usipopingana na hako katabia utasikia bora niende kwa my aunt kule nakuwa na amani yaaani ikifkia hapo jua kwamba wewe ni bosheni tuu..! Knga ni bora ikifikia kwenye tiba it will cost you alot..!
 
Kweli hatamimi nimehisi hivyo hivyo,sasa nifanyeje? maana hatanikijaribu kumzuia pia inakuwa ugomvi then mwishowe anaenda hukohuko tena.
 
Mpige mkwara huyo shangazi mtu mwambie hanaruhusa ya kumpokea mke wako . Na ikiwezekana gombana naye iliawe anakuogopa hutakiwi kuonekana mtaarabu ktk hili hiyo ndiyo dawa pekee
 
Asante kwaushauri,nitalifanyia kazi maana hatajana nabaridi hili nimelala mwenyewe kitandani,chumba kilikuwa kikubwa kama disco alafu upo pekeyako naviti wametoa.
 
Pole sana mkuu huyo shangazi yake anaonekana hamnazo! Mpe ukweli kuwa tabia hiyo haifai.. lakini pia je huyo binti wazazi wake bado wapo hai? Kama wapo ikibidi waeleze tatizo la huyo shangazi anayemuhifadhi mke wa mtu bila kuhoji kwa kina.
 
Hebu weka hadharani kile akichokujibu ndipo wengine tutakapoweza kukusaidia. Wakati mwingine kauli inatoa mwanga juu ya yote anayofikiria na kile unachoweza kufanya.
 
Huyo shangazi ndo anakuharibia ndoa, ndo anampa miongozo dhaifu huyo mkeo. Kuwa na msimamo mpige marufuku mkeo kwenda huko kama hataki akaolewe hukohuko kwa shangazi yake
 
Tatizo lipo hapa...

Hata mwembe haukai muda mrefu hivi kabla ya kuanza uzao wa kwanza wa maembe...

Miaka minne mtu mzima unakaa na binti ukimpa tu ahadi za kumuoa???

Ndio maana nikasema "tumeishi wote kutokana nasababu flani" ila mchakato wandoa ulikuwa uanze mwezi wanne ila alipata msiba wababa yake hivyo tumeirusha mpaka mwezi wasita
 
Hebu weka hadharani kile akichokujibu ndipo wengine tutakapoweza kukusaidia. Wakati mwingine kauli inatoa mwanga juu ya yote anayofikiria na kile unachoweza kufanya.

Alinitolea maneno machafu sana,tena mbele yabint
 
Ndio maana nikasema "tumeishi wote kutokana nasababu flani" ila mchakato wandoa ulikuwa uanze mwezi wanne ila alipata msiba wababa yake hivyo tumeirusha mpaka mwezi wasita
Nijuwacho mtu huwa anapewa ushauri kutokana na taarifa alizozitoa. Wewe unataka ushauri lakini kuna taarifa hutoi unategemea ushauri utakuwa kamili..?? Hayo mambo flani au alichosema shangazi ambacho huwezi kukiandika pengine ndo yanabeba sehemu kubwa ya ushaufi..... Haya se ficha taarifa sisi tufiche kauli
 
Alinitolea maneno machafu sana,tena mbele yabint

Alikutukanaje? Zungumza tu, hatufahamiani humu. Mf; mtu akikueleza, wewe ni mwanaume gani usie na pesa, hiyo ni dalili ametafutiwa mwanaume wanaeamini ana uwezo kuliko wewe au amekuwa akiuvumilia uhusiano na hivyo anataka mtu mwenye uwezo. Sasa eleza tu hayo matusi usaidiwe, kuwa black and white tu.
 
Ninachokiwaza siwez kukiandika hapa.

Labda tuanze na kauli ya shangazi alokujibu, na mi nitaweza kuandika.
 
Ndio maana nikasema "tumeishi wote kutokana nasababu flani" ila mchakato wandoa ulikuwa uanze mwezi wanne ila alipata msiba wababa yake hivyo tumeirusha mpaka mwezi wasita

ndo umuoe anaona unamcheleweshea ndoa au huonyeshi dalili
 
Kama bado hujamuoa huna mamalaka nae sana. Ni yeye mwenye maamuzi ya kukusikiliza au laah. Fanya kama unatangaza nia, uone heshima itakavyorudi.
 
Back
Top Bottom