Hivi hawa ndege wanafaa pia kwa kitoweo?

General Galadudu

JF-Expert Member
Nov 7, 2015
1,868
2,200
Tumeona Kuku, bata, kware, kanga, mbuni, bata mzinga nk. wanatumika pia kwa vitoweo majumbani....... lakini nimekuwa najiuliza kuhusu KASUKU na TAUSI hivi nao huwa wanaliwa au wao wapo kama mapambo tu?
 
Nenda Magogoni uombe mmoja ujaribu maana Tausi waliletwa toka India hivyo sijawaona msituni. Kasuku nawaona kwenye Cage za watu siyo kwenye msitu au anga. Kama unaweza iba mmoja toka Magogoni kisiri halafu utupe majibu kama alikuwa mtamu au kama we mpishi wa mapadlock muombe mchinje mmoja.
 
Hivi kwa nini tausi hawafugwi majumbani mwa watu kama ilivyo kwa kasuku? Kwa vile tausi ni ndege wa kufugwa na siyo kama wale waishio porini tunaowaita "nyara za serikali" raia wa kawaida wangeruhusiwa kuwafuga ingesaidia sana kuongeza kizazi chao hawa ndege. Au ni Magogoni pekee ndiyo wenye haki ya kuwafuga na kuendeleza kizazi cha hao tausi?
 
Hawa ni ndege wa kuletwa siyo kama Mbuni unayeweza kumchukua mbugani au kuiba mayai yake. Inabidi ufanye mpango na hao wa magogoni ili utupe majumuisho.
 
kula mnyama inategemea umebase ktk dini ipi, mfano kuna dini (way of life)nyingine hawali kuku na wengine hawana dini wanakula vidudu vya ajabu ajabu mara kala nyani mara kala simba mara mwengine kala kenge n.k sasa apo utajua unakula kwa mtindo gani wa maisha.
 
sema tupo Na choice nyingi za vyakula ila Kama ungekuwa mahali ambapo kasuku ndo wanapatikana kwa wingi kwa maana nyingine ndo only source of protein ungewala Tu hao kasuku.na tausi Ni ndege wa kuletwa sio indigenous hapa kwetu Tanzania Na Afrika mashariki .
 
Umeshawahi kumtembelea mwenyeji wako halafu akakuandalia kitoweo kisha ukamuuliza hii ni nyama gani? Eti galadudu?
 
Back
Top Bottom