ACADEMIA TODAY
Senior Member
- Jun 7, 2013
- 179
- 86
ma president is lowasa 2015 sion na sijaona anayeweza kuvaa viatu vya urais zaidi ya lowasa 2015..ukiijua siku atakayogawa vibahasha tustue na sisi tukajizolee. Kura na siri yetu.
ni hatari kwa afya ya nchi hii ila sijui kwa nini hata chama chake hakichukui hatua ya kuepusha madhara tunayo yaona sisi great thinkers wa jf.
Sina uhakika kama huwa unaelewa mada kabla ya kuchangia.Suala la msingi ni kufuata kanuni na maadili ya msingi ambayo yatasaidia wagombea kutoingia kwenye hali ya kuligawa taifa; na kisha baada ya hapo si uchaguzi upo bwana? sasa ya nini tupige makelele ?Hakuna mtu wa kumzuia Lowassa. Wananchi wanampenda na hela anayo. Hata kama hupendi huna budi kukubaliana na ukweli japo ninaelewa unaumia lakini ndiyo hakuna namna ya kuubadilisha. Huwezi kuukimbia ukweli.
Sina uhakika kama huwa unaelewa mada kabla ya kuchangia.Suala la msingi ni kufuata kanuni na maadili ya msingi ambayo yatasaidia wagombea kutoingia kwenye hali ya kuligawa taifa; na kisha baada ya hapo si uchaguzi upo bwana? sasa ya nini tupige makelele ?
- Huyu mtu ana mpango wa kugombea urais 2015,
- Huyu mtu huyu hutangazia nia yake maeneo ya ibada,
- Huyu mtu huyu hutanguliza vibahasha katika maeneo hayo ya ibada kabla ya kutangaza nia (na vibahasha vyake vya ukweliii).
- Huyu mtu huyu wengine humlaumu eti ni fisadi.
Sasa mimi wasi wasi wangu ni pale ninapoona hakuna mtu anayemkemea.Najiuliza je! ina maana huyu mtu yuko sahihi? Kama tunadhani yuko sahihi; ni kwa nini? Hatuoni kuwa kama akiendelea hivi, wenzake ambao nao wana nia ya kugombea urais 2015, wataanza kuingia na vibahasha kwenye maeneo ya ibada na hiyo sio tu kwamba itakuwa ni aina fulani ya rushwa bali pia itachochea migawanyiko ya kidini?
Kama hayuko sahihi; kwa nini vyombo mbali mbali vya kitaifa kama vile Chama chake, Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, Rais, TISS, n.k wasimshauri? Je! inamaana watakuwa hawaoni, au wanamuogopa, au wana maslahi na kinachofanyika?
Kwa maoni yangu jambo hili linachukuliwa kama mzaha ila mwisho wa siku linaweza kuleta migawanyiko mibaya.Wenzake watakuwa wanasoma upepo, wakiona hili la kutoa na kusaidia kuchangisha fedha kwenye maeneo ya ibada linasaidia nao watawekeza huko huko.Mwisho wake watu wataanza kuhoji fulani kachangia msikiti au kanisa? kama kachangia kanisa kachangia bei gani na msikiti kachangia kiasi gani? kisha kwa nini kule kachangia zaidi ya kule ? kwa nini kwetu hajachangia? kwa nini kapendelea dini ile au hii? fulani na yeye na aje kwenye dini hii au ile n.k. Hii ni hatari aisee.
Nashauri katika kuchangia msitaje majina ya watu.Changieni tu hoja kwa ujumla wake kwa sababu mkitaja taja majina ya watu, upo uwezekano wa uzi huu kupoteza muelekeo na kisha kufungiwa
Hudhani kama mtu kaiba na anataka kutubu; basi dawa ni kukiri mbele ya aliemuibia kwamba alimuibia na sasa anaomba radhi na kisha kurudisha alichoiba?tujiulize mtu ameiba na tayari anazo pesa na hajachukuliwa hatua.Kaamua kutumia hizo hizo pesa kuimarisha nyumba za ibada badala ya kujijengea majumba ya kifahari nje ya nchi pengine ni moja ya namna yake ya kutubuSiungi mkono utaratibu wa viongozi wa dini kuwaalika wanasiassa waongoze harambee za kidini.Kwa nini viongozi wa kidini wasiongoze masuala ya kidini na viongozi wa kisiasa wakaongoza masuala ya kisiasa?je unataka kuwashauri viongozi wa nyumba za ibada wazikatae?
Hata mimi sijui kama ana shida ya uraisi .Ila tu tujue baada ya kutoa mchango wake hutangaza dhamira moja kwa moja , au kiufichouficho.Hata hivyo mimi sijui kwa nini haya yanafanyika sasa kuelekea uchaguzi mkuu.Labda unaweza kutusaidia.Huyo mtu sidhani kama ana shida ya UraisTunajadili yale tunayoyaona.Wewe unajua mambo yanayofanyika ndani ya NEC ya CCM?maana kama nia ni hiyo angewahonga Nec ya chama chake kwani unauhakika gani kama atapitishwa na chama chake?
Nadhani mda mwingine hata unachosema hukijui. Hebu tetea hoja yako ieleweke we kibaka sio una jamba jamba tu humu. Kakufanyia nini la maana huyo fisadi?Hakuna mtu wa kumzuia Lowassa. Wananchi wanampenda na hela anayo. Hata kama hupendi huna budi kukubaliana na ukweli japo ninaelewa unaumia lakini ndiyo hakuna namna ya kuubadilisha. Huwezi kuukimbia ukweli.
Watu wa chama chake na wao wanalalamika pembeni bila ya kumfesi mhusika tena hawathubutu hata kumtaja jina kama mwanzisha mada alivyoogopa kumtaja jina.
Kuna kitu si cha kawaida kwa Lowasa, kwa nini anaogopwa na kila mtu hapa nchini?
Hadi mwenyekiti wa chama chake anamwogopa.
Sina uhakika kama huwa unaelewa mada kabla ya kuchangia.Suala la msingi ni kufuata kanuni na maadili ya msingi ambayo yatasaidia wagombea kutoingia kwenye hali ya kuligawa taifa; na kisha baada ya hapo si uchaguzi upo bwana? sasa ya nini tupige makelele ?
navyoamini mimi fisadi huyu hawezi kuwa rais wa nchi yetu labda kama sikuzaliwa mara!ikitokea akawa basi bwana!Ndiyo maana ni mara chache sana huwa ninawaReply watu wanaoniQuote hapa Jukwaani kwasababu ya "pumba" zenu.
Kuchangia kwake ujenzi wa nyumba za ibada analigawa vipi taifa? It seems like you are INSECURE.
Kwanza hii thread yenyewe imejaa nadharia tupu ni kwavile umetukuta sisi waSwahili tunapenda mambo marahisi marahisi lakini kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kuchangia thread ambayo imejaa nadharia tupu (umeshindwa hata kulitaja jina la huyo muhusika umeishia kutuaambia "huyu mtu").
Ni aibu kwa threads za namna hii kuruhusiwa kuwepo hapa kwenye Jukwaa la Siasa. Huyu mtu?! WTF?
kuna siku utakuja kukimbia kivuli chako mwenyewe .nakuambia hizi dini bora zisingekuwepo zimerudisha maendeleo nyuma sananavyoamini mimi fisadi huyu hawezi kuwa rais wa nchi yetu labda kama sikuzaliwa mara!ikitokea akawa basi bwana!