Hivi hata wananchi wanauza nchi yao kwa bei poa!!!!!

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,187
670
DC ataka wanakijiji waende mahakamani
Deus Gabone
HabariLeo; Tuesday,October 09, 2007 @00:06

MKUU wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam, Abdallah Kihato amewaamuru wananchi wa Kigamboni wanaoishi Kijiji cha Kigogo-Kisarawe II kupeleka malalamiko yao mahakamani baada ya wananchi hao kukataa kuheshimu kikao alichokiitisha jana kutatua mgogoro wao na mfanyabiashara.


Kihato aliitisha kikao hicho baada ya wananchi hao kumdai mfanyabiashara Mohammed Akbar ardhi waliyomuuzia tangu mwaka 2005 na baadhi yao kukana kuwa hawajawahi kumuuzia ardhi.

Akiwa kijijini hapo, DC Kihato alihitaji kusikiliza malalamiko ya mtu mmoja mmoja kufahamu chanzo cha mgogoro, jambo ambalo halikufuatwa. Kwa baadhi ya waliofanya hivyo, ilibainika baadhi ya madai ya wananchi hao hayana ukweli.

Mkuu huyo wa wilaya alipendekeza wananchi hao wachukue hatua za kwenda katika vyombo vya sheria baada ya kushindwa kupata ufumbuzi wa suala kati ya mfanyabiashara huyo na wananchi wa kijiji hicho ambao wameingia katika mgogoro na mfanyabiashara huyo baada ya kuuza ardhi yao.

Mkutano wa jana wa DC Kihato na wananchi hao ulishindwa kumalizika baada ya wananchi kudai mkuu huyo wa wilaya alikuwa akimpendelea mfanyabiashara huyo wakati anasikiliza shauri hilo.

Hali hiyo ilimlazimu amuagize Mkuu wa Polisi wa Wilaya kukaa na wananchi hao kuangalia jinsi ya kulifikisha suala hilo katika vyombo vya sheria.

Alipopewa nafasi ya kutoa maelezo, mwanakijiji Tausi Sozigwa alisema aliikadiria ardhi yake kuwa inaweza kufikia ekari 16, lakini walipokuja wataalamu wa ardhi kuipima ili alipwe fedha yake halali, wapimaji hao walitambua kuwa ni ekari tisa tu. Mwanakijiji huyo anadai apewe fedha za ekari saba zilizobakia.

Alipoulizwa makubaliano yao na mnunuzi kwa kila ekari, mwanamke huyo alidai walikubaliana Sh 180,000 kwa kila ekari, na alipoulizwa kama alilipwa kiasi chote cha ekari zilizopimwa alisema hana uhakika na fedha alizolipwa kama zilikuwa zimetimia kwa kuwa hajui kusoma.

Mwanakijiji mwingine, Margaret Shija alidai mumewe aliuza shamba lote wakati yeye akiwa safarini Tabora, hivyo fedha alizopewa mume wake hana uhakika kama zilitimia.

Alisema alipoamua kufuatilia kwa mnunuzi huyo, mumewe Pius Mduhu alikana kumuuzia ardhi na kudai mnunuzi huyo aliingilia shamba hilo bila idhini yake, ndipo alipopelekwa mahakamani na kufungwa miezi mitatu kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Alipopewa nafasi ya kuelezea utaratibu anaoutumia katika kununua ardhi na nia ya kufanya hivyo, mfanyabiashara huyo alisema anapitia katika serikali za vijiji ambako anawapa fomu ili wanakijiji wanaotaka kuuza ardhi yao wajaze na baadaye anaipima ardhi kabla ya malipo kufanyika.

“Kawaida wananchi wanapeleka maelezo yao katika serikali na kujaza fomu za kuthibitisha kuwa ardhi wanayo. Huweka picha na saini kwenye fomu hizo kabla ya kuletewa taarifa na kuonana nao, kisha tunaipima na mhusika analipwa kwa maelewano,” alisema Akbar.

Alisema madhumuni ya kununua ardhi hiyo ni kwa kujenga nyumba za bei nafuu na kuziuza kwa wananchi kwa bei nafuu, ikiwa ni pamoja na kuliendeleza eneo hilo. Hadi sasa, wananchi waliouza ardhi yao ni zaidi ya 100 ambao wameuza zaidi ya ekari 800. (


source habari leo
 
Alipoulizwa makubaliano yao na mnunuzi kwa kila ekari, mwanamke huyo alidai walikubaliana Sh 180,000 kwa kila ekari, na alipoulizwa kama alilipwa kiasi chote cha ekari zilizopimwa alisema hana uhakika na fedha alizolipwa kama zilikuwa zimetimia kwa kuwa hajui kusoma.
Laki na themaninini??
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom