firstcollina
JF-Expert Member
- Aug 8, 2009
- 349
- 24
Wajumbe leo naomba niulize jambo nipate hekima zenu,
Miaka ya nyuma wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere jambo hili lilikuwa linawezekana, wanafunzi walilipiwa ada, walipewa fedha za matumizi hasa wale waliokuwa shule za kulala vyuo na kwingineko. walipewa fedha alimaarufu kama kichele, japo ilikuwa ndogo lakini iliwasitiri sana, walipewa sabuni, mafuta na hata wakati mwingine walipelekwa kwa treni na mabasi yaliyokuwepo. Chakula ilikuwa si shida... maana walipewa na waliula vizuri.
Hayo yote yaliwezekana licha ya ukweli kwamba nchi ilikuwa na watu wachache na hivyo uzalishaji mali ulikuwa mdogo. Vilevile ikumbukwe wakati huo haikuwa rahisi kuzalisha ziada maana hata nyenzo zilikuwa duni, lakini juu ya elimu liliwezekana.
Sasa tatizo ni kwanini mambo hayo siku hizi hayawezekani? Au ndio kusema haya kuwa na tija kwa taifa? Leo vyanzo vingi vya uchumi vinatumiwa. Madini(Tanzanite, Dhahabu,Almas n.k) Maliasili wanyama na misitu pia. Kikubwa zaidi wakati huu hata misaada toka nje imekuwa ni mingi ukilinganisha na enzi zile lakini yet haiwezekani..... Pamoja na kwamba wazazi wanajitolea kwa kuchanga michango mingi tu tena mbalimbali lakini serekali inashindwa nini kufanya yale ya kipindi kilee......
Kwa sasa watu ni wengi....kweli. lakini pia uzalishaji nao pia umeongezeka, makusanyo ya kodi nayo siyo haba. Najiuliza kwanini kule iliwezekana licha ya hali ngumu in both Social, Political, Economic and Technological aspects. Leo hii licha ya kuwepo hayo yote still haiwezekani wajumbe nisaidieni........!
Luteni nimekupata ndugu yangu, lakini hazina si bado ipo palepale na haijakufa...... Tunachozalisha leo si kinaenda hazina...? Priority ni kweli Afya, Elimu ilipewa kipaumbele lakini hata leo serekeli inasema vivyo hivyo Elimu, Afya tena na Kilimo..... lakini wapi bwanaaaa.. It is true, very very SadKwangu jibu ni rahisi, priority ilkuwa elimu na afya na kile kidogo tulichozalisha chote kilikwenda hazina sasa tunachozalisha kingi kinakwenda kwenye mifuko binafsi very sad.
Yes! Lakini ni jinsi gani tuna weza kuibali hali hii maana mawazo ya haiwekani ni mawazo ya Mfu tuI wish ningepitia kipindi hicho maana sasa hali tulionayo sasa ni aibu tupu, kwetu sio kina kabwela tunazidi kupata taabu!
Kwangu jibu ni rahisi, priority ilkuwa elimu na afya na kile kidogo tulichozalisha chote kilikwenda hazina sasa tunachozalisha kingi kinakwenda kwenye mifuko binafsi very sad.
MR, wabenzi wanaendelea kutanua kwa rasilimali zetuI wish ningepitia kipindi hicho maana sasa hali tulionayo sasa ni aibu tupu, kwetu sio kina kabwela tunazidi kupata taabu!
Kuna mambo yaliyovuruga hapa katikati kama Structural Adjustment Programmes (SAPs), neo-liberal policies (globalization), kuvunjika kwa USSR, muungano wa West na East Europe, kuongezeka kwa idadi ya watu bila mipango mirefu na endelevu, ufisadi, vita vya Kagera, kuchanganya biashara na siasa, na mengine mengi uyajuayo wewe.
Tatizo la Umaskini wa Tanzania ni kutokana na baadhi kama si kwa sababu ya yafuatayo:
Kwa sasa watanzania tuamue kuchagua chama chenye sera tofauti na mambo yatabadilika.
- wakati wa nyerere pamoja na kujitahidi kutoa huduma bure uzalishaji ulikuwa chini na watendaji hawakujua kuendesha mashirika kwa faida, pia kupeana madaraka kwa kutumia ukada wa CCM kuliharibu mashirika mengi.
- Baada ya mwl. nyerere kuanchia ngazi nchi haikua na hata senti moja ya akiba, mzee mwinyi aliona njia pekee ya kukwamua nchi ni kufungua milango ili bidhaa ziingie, hapo makosa yaliyofanyika ni kwamba nchi haikujiandaa kufungua milango kwa hiyo wezi na matapeli wengi walitumia nafasi hiyo kuiibia nchi. Pia mzee mwinyi alishindwa kukusanya kodi walau hata kidogo.
- Mkapa ameingia akajitahidi kukusanya kodi kweli mapato yakaongezeka lakini wazungu wakambana ili awauzie madini, wanyama, n.k.
- Lakini kubwa zaidi ktk kukwamisha nchi hii ni CCM kutokuwa na nia ya dhati ya kutenda haki. Mikataba inayoingiwa na watawala wa CCM 90% yote ni ya wizi baada ya wao kuchukua 10%.