Hivi hakuna kibao cha kuonesha makazi ya watu kwenye barabara?

Masasaa

JF-Expert Member
Oct 23, 2015
585
623
Hivi katika sheria za barabarani hakuna kibao kinachoonyesha hapa ni makaxi ya watu, maana hii kauli imekuwa kero kwa madereva, mtu barabara hata hujawahi kupita, trafic wanajificha mahali, hakuna kibao cha 50km/h lakini wakikusimamisha utasikia wanakuambia umeoverspped hapa ni makaxi ya watu

Wanajf nisaidieni, najuaje kuwa hapa ni makazi ya watu????
 
Wewe ni dereva uchwara!!kwani vile vibao vinavyoonesha mapito ya wanyama wafugwao,watoto wa shule,kivuko cha waenda kwa miguu,watembea kwa miguu,waendesha baiskeli....JEE HAYO NI MAKAZI YA SOKWE?
Ebu kabla ya kutupia bandiko kwanza muwe mnasuhurishana ugomvi na wanandoa wenzunu kisha ndio mje humu.Ebohhh!!??
 
kama taratibu za uandishi huzifuati hizo za barabarani unazifuata kweli?
hatuna neno makaxi kwenye kiswahili
 
button "Z" kwenye keyboard yako imeharibika?

pole,wewe akikusimamisha komaa nae kutokana na mazingira unayoyaona..kama ni makazi ya watu utayatambua kwa nyumba pembeni mwa barabara na shule mixer maduka na vibiashara vingine vingi.
ni akili yako tu ujiongeze usikubali hela iende kiboya
mwisho jifunze kupunguza speed unapoendesha..sio unaingia barabara ya vumbi mtaani speed utadhani upo barabara kuu unaenda mkoani
HIGH SPEED KILLS!
 
maka
Hivi katika sheria za barabarani hakuna kibao kinachoonyesha hapa ni makaxi ya watu, maana hii kauli imekuwa kero kwa madereva, mtu barabara hata hujawahi kupita, trafic wanajificha mahali, hakuna kibao cha 50km/h lakini wakikusimamisha utasikia wanakuambia umeoverspped hapa ni makaxi ya watu

Wanajf nisaidieni, najuaje kuwa hapa ni makazi ya watu????
makaxi=makazi?
 
Inabidi upitie upya Alana na michoro ya barabarani Angelia 125 na 126 hapo kwenye Picha.

c2d2dab36d70e76c87d2a0cb900a8dae.jpg
cd879e895422b8b532ac70b43ae8f522.jpg
 
Hiyo alama ipo mkuu, tena na speed yake ni 50km/h eneo la makazi ya watu.....

Ila kibongobongo hicho kibao kuonekana ni adimu
 
Back
Top Bottom