TANZANNIA
JF-Expert Member
- Sep 29, 2015
- 1,047
- 384
hivi karibuni kumekuwa na mtindo wa kila tv stesheni kuwa na dekoda au kisimbusi chake,hali hii hufanya sisi wateja kuchanganyikiwa na kutojua twende wapi,na kama unapenda kuona mambo tofauti maana yake ni kuwa na visimbuzi zaidi ya kimoja,ushauri wangu kwa wamiliki wa tv kama inawezekana ili kutupunguzia mzigo wa kuwa na dekoda za aina tofauti,wangejipanga waunde dekoda moja ambayo ina uwezo wa kubeba tv stesheni tofauti ili mtu achague mwenyewe alipie stesheni gani.