Hivi haiwezekani kutengeneza chanjo moja tu kwa ajili ya aina zote za virusi? Wataalam mnisaidie

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Kila siku vinaibuka virus tena vina majina ya ajabu ajabu sasa mimi nina swali, hivi haiwezekani kuwa na chanjo moja tu kwa ajili ya virusi vyote? Kwamba iwe ni chanjo moja tu lakini ya kuzuia virus vyote?

Maana sasa tutakua tunadungwa machanjo tu? Maana kila siku unaibuka ugonjwa mpya mimi hofu ni kuwa miaka 20 ijayo miili yetu itageuka kuwa na makovu ya masindano ya chanjo hili jambo linanipa stress sana nafikiria watoto wangu watakuja kuishi vipi ktk zama zao?

Hivi haiwezekani kuwa na chanjo moja tu ya kukinga virus vyote?
 
Haiwezekani Mkuu na sababu ni Wadudu hawa au vimelea hivi havifanani generically au kwenye Vinasaba vyake hazifanani.
 
Inawezekana kabisa. Ili kufanikisha hilo, lazima dhana ya ^specificity^ (umahususani) wa chemikali ama dawa-chanjo ihusike. Ni kama ufunguo kwenye kufuli; kila kufuli na ufunguo wake. Hakuna kufuli mbili tofauti zinazoshare (or, more accurately, zinazopaswa kushare) ufunguo mmoja. But kinga natural ya mwili ni some sort of ^a master key^ inayotibua kotekote.

Constraints ama vikwazo vizuiavyo kufikia hatua hiyo mujarabu & sadifu:

1. Halafu mabourgeoisie walafi & wanyonyaji watakula wapi!?

2. Halafu 2030 Depopulation Vision & NWO itafikiwaje!?

3. Halafu Afrika itaendeleaje kutawaliwa!?

4. Halafu wanasayansi watapataje ^human lab^ za kufanyia inhumane experiments zao!?

5. Halafu dawa expired na za tentative trials na defective ziuzweje & wapi!?

NB: Shetani anakuletea ugonjwa na maradhi, kisha anavumbua solution halafu anakuambia umwabudu yeye. Nonsense!
 
Kila siku vinaibuka virus tena vina majina ya ajabu ajabu sasa mimi nina swali, hivi haiwezekani kuwa na chanjo moja tu kwa ajili ya virusi vyote? Kwamba iwe ni chanjo moja tu lakini ya kuzuia virus vyote?..
Ni sawa na ku suggest kutengeneza brashi moja kwa ajili ya kusugulia MENO, MASINKI, VIATU, KARO, SAKAFU nk. Unaionaje hiyo?
 
Haiwezekani, kwasababu virusi wapo wa aina mbalimbali kimaumbile,kisize na vingine vingi, mfano Kuna virusi wenye gamba gumu au layers za magamba zaidi ya moja.

Pia chanjo za virusi hutengenezwa kwa kutumia virusi mwenyew(yaan wanamdhoofisha virusi wanamuweka kwenye mwili wako kwa vile amedhoofu mwili wako utamshambulia na kumuua na kujitengenezea kinga/ nguvu itakayoweza muua virus wa namna hiyo.

Virus wa ukimwi wataalam wameshashindwa kumdhoofisha ndo maana hakuna chajo ya ukimwi
 
Kila siku vinaibuka virus tena vina majina ya ajabu ajabu sasa mimi nina swali, hivi haiwezekani kuwa na chanjo moja tu kwa ajili ya virusi vyote? Kwamba iwe ni chanjo moja tu lakini ya kuzuia virus vyote?..
Inawezekana ila bado sana mkuu,tusubiri mpaka wamalize madini yote Africa, sasa hivi wako kwenye mpango wa kutupunguza kwanza...
 
Back
Top Bottom