tajirijasiri
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 2,863
- 3,854
- Thread starter
- #21
Mkuu, hii nayo huwa siielewi, Eti Meli chakavu bilioni 8, wakati Meli mpya Bilioni 6. Bilioni 2 ziko wapi?
Mkuu, hii nayo huwa siielewi, Eti Meli chakavu bilioni 8, wakati Meli mpya Bilioni 6. Bilioni 2 ziko wapi?
Nimeisoma thread yako yote nikawa natafuta sehem waliyoshtakiwa polisi au mahakamani nikitegemea kuona namba ya kesi ya mashtaka yao(RB KWA POLICE CASE AU CRIMINAL CASE NO..KWA MAHAKAMANI)
Lkn sikuona hata sehemu moja!!!!
BTW.HIYO POINT NDIYO ILIYOMPA KIFUA MBOWE..TUNDU LISU. ..MNYIKA N.K(UKIWEMMO NA WEWE) KUMCHUKUA LOWASSA WALOMUITA FISADI FOR 8 CLEAR YEARS KUWA HIVYO. ..NA WAKATAKA KUMUWEKA MAGOGONI JAPO MUNGU HAKUPENDA!!!
SO..Brother it's better you shut up your rotten mouth kwa kuwa hizo ni ZILIPENDWA!!!!![/QUOTE
Ndiyo ninyi mnaouaminisha Umma kuwa ufisadi ni Lowassa na Lowassa ni ufisadi,laiti ungelitumia japo akili yako uliyobakiziwa kwa ajili ya kuvukia barabara,ungemuelewa mleta mada anamaanisha nini.
Ili kuithibitishia nchi kuwa mna dhamira ya dhati ya kupambana na ufisadi,mlipaswa mzitazame upya Kashfa zote za ufisadi zilizowahi kulikumba Taifa letu.Huwezi kujisifu unatumbua vichunusi na vijipu uchunguzi,wakati Taifa lina majipu kama ya Buzwagi,meremeta,Tangold,kiwira,DeepGreen,uuzwaji wa nyumba za Serikali na mashirika ya Umma,Rada na sekta zote za manunuzi ya Umma.
Fedha zilizopotea kupitia ufisadi huo,zinatosha kututoa hapa tulipo lakini hakuna hata mmoja anayeweza kuzigusa kashfa hizo,ndiyo Maana tunadhani kashfa hizo zilikuwa ni motisha chanya kwa watendaji wa Serikali ili wapewe nafasi kubwa za kufisadi Taifa.
Joka la makengeza lilithibitishwa na Taasisi ya kimataifa ya SFO kuwa limeliibia Taifa kupitia udalali wa manunuzi ya Rada na likakiri kwa kinywa chake kuwa linamiliki akaunti ya vijisenti huko ng'ambo,lakini hadi leo bado linabadilishwa nyadhifa tu na kudhihirisha kuwa ni jitu safi.
Hatutaki usanii,tunataka hatua stahiki zichukuliwe ili kulinusulu Taifa letu.
JK alishasema, pesa za ESCROW si za UMMA. Kwa maana Rugemalila aliamua kugawa pesa zake baada ya kuwa na ziada kubwa katika utajiri wake.
Mrudisheni na werema basi , mbona mmemtenga ?Nimeisoma thread yako yote nikawa natafuta sehem waliyoshtakiwa polisi au mahakamani nikitegemea kuona namba ya kesi ya mashtaka yao(RB KWA POLICE CASE AU CRIMINAL CASE NO..KWA MAHAKAMANI)
Lkn sikuona hata sehemu moja!!!!
BTW.HIYO POINT NDIYO ILIYOMPA KIFUA MBOWE..TUNDU LISU. ..MNYIKA N.K(UKIWEMMO NA WEWE) KUMCHUKUA LOWASSA WALOMUITA FISADI FOR 8 CLEAR YEARS KUWA HIVYO. ..NA WAKATAKA KUMUWEKA MAGOGONI JAPO MUNGU HAKUPENDA!!!
SO..Brother it's better you shut up your rotten mouth kwa kuwa hizo ni ZILIPENDWA!!!!!
Sijui kwa nini walalamikaji kuhusu Escrow acc wanasahau hitimisho hili muhimu. Serikali ilishasema hizo hazikuwa pesa zake bali za wanahisa wa IPTL (wafanyabiashara binafsi). Tibaijuka na wengine hawakuwajibishwa kwa makosa ya jinai kuhusiana na Escrow bali kwa kutotoa taarifa mapema kuhusu kupokea kiasi kikubwa cha pesa kulingana na kanuni za maadili ya viongozi serikalini.
Kwa msimamo huo wa serikali ambao haujabatilishwa na mahakama, ni kupoteza muda kuwazungumzia wahusika wa Escrow acc kama mafisadi au wajinai (criminals). Ni vyema mjadala ujikite kuhusu busara nzima ya kuwa na uwekezaji wa aina ya IPTL na namna ya kuachana na aibu/hasara hiyo kwa taifa. Someni makala za Mihangwa kwenye Raia Mwema.
Kwa hiyo tumtegemee Werema kuwa promoted???Kama ulihusishwa Na wizi Wa Escrow hakika were in lazima update Promation
Kama Escrow ilikuwa Mali ya wanahisa a.k.a wawekezaji binafsi, ilikuwaje ikatunzwa BOT?, siku hizi BOT wanatunza pesa binafsi? Kama pesa si ya Umma nini hasa dhima ya maelekezo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenye pesa ambayo inawahusu watu binafsi? Nini hasa ilikuwa nia na lengo la Gavana wa Benki Kuu kutaka Mwongozo toka Serikalini juu la kulipa Fedha za Escrow ambazo wana sema ni Mali binafsi? Tangu lini Fedha za mtu binafsi zikaombewa mwongozo Serikalini?
Tukubali tukatae Escrow Acc ilikuwa na Fedha za walipa Kodi wa Tanzania.
Nimekuelewa mkuu, hao wahusika sasa ndio tunawataka haswaa, hayo ndio majipu ya kutumbua tunayoyataka. Hatutaki dilly dally za kuhangaika na vipele.Mkuu sikubishii unachosema. Lengo langu ni kusisitiza msimamo iliotoa serikali kuhusu suala hili na kutaka tuufanyie kazi badala ya kuhangaika na watu binafsi kama Muhongo na Maswi ambao walikuwa "wakitumwa" tu kufanikisha ulaji wa "wenyewe". Hao "wenyewe" ndio waliotufunga na mkataba wa ovyo sana wa IPTL ambao unaendelea kufilisi taifa kupitia TANESCO (soma makala za Mihangwa katika Raia Mwema). Usifikiri ulaji kupitia IPTL ulianza na kuishia na acc ya Escrow. Zaidi ya pesa za Escrow acc, kila mwezi TANESCO inailipa IPTL kama USD 4m za "capacity charges". Jiulize wanufaika wa malipo hayo ni kina nani hasa na kwa nini tunaendelea kuendekeza mkataba wa aina hiyo. Badala yake naona watu wameng'ang'ania kupambana na akina Muhongo badala ya wahusika "wenyewe".