Hivi Elimu yetu itakuwa ya Majaribio mpaka lini?

Shebbydo

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
1,174
1,937
Habari wana JF,

Nitoe masikitiko yangu makubwa juu ya mfumo wetu wa elimu jinsi unavyochezewa kwa majaribio ya viongozi wanaokabidhiwa wizara hii. Hii sasa imekuwa ni "fasion" kwa mawaziri wanaokabidhiwa wizara hii kuondoa yale waliyoyakuta na kuweka ya kwao wanayoamini kuwa ndiyo yanayofaa.

Kibaya zaidi hawaji na mawazo ya kuondoa mfumo tulioachiwa na Wakoloni waliokuwa na lengo moja tu la kuchuja hadi wabakize wale waliowahitaji kwa ajili ya kuendesha shughuli za serikali zao. Sehemu ambayo imekuwa ikichezewa ni upangaji wa madaraja na viwango vya alama tu kiasi kwamba imefikia katika nchi hii hii moja kuwa na vyeti vya kuhitimu elimu ya sekondari tofauti takribani vinne kuanzia 2013 hadi 2016.

Kwa mfano kidato cha sita; 2013 kurudi nyuma alama zilikuwa kama ifuatavyo:
F 0-24, S 25-34, E 35-44, D 45-54, C 55-64, B 65-74, A 75-100.
Madaraja yalikuwa hivi;
I 3-9, II 10-12, III 13-17, IV 18-19, O 20-21

Mwaka 2014 mfumo ukabadilishwa ghafla wakati vijana wapo katikati ya mitihani.
Alama;
F 0-19, E 20-29, D 30-39, C 40-49, B 50-59, B+ 60-69, A 70-100.
Madaraja;
I 3-6, II 7-9, III 10-13, ikafuata division 4 ambayo haikuwa na point yoyote na zero ambayo ni NECTA tu ndiyo waliokuwa wanajua ilianzia ngapi.

Mwaka 2015 tukaletewa GPA lakini alama zikabaki vilevile, tukiaminishwa huo ndiyo mfumo bora kuliko wa kupanga Madaraja. Imeingia serikali yenye "uamuzi mgumu" tumerudishwa kwenye madaraja kama yale ya 2013 kurudi nyuma lakini alama tofauti ambapo F ni 0-34, S 35-44.

Mwaka 2014 na 2015, kutokana na kuiondoa "S" na kuweka "B+" ilibidi E=S ya zamani yenye weight ya 0.5, D=E ya zamani yenye weight ya 1, C=D ya zamani yenye weight ya 2, B=C ya zamani yenye weight ya 3, B+ = B ya zamani yenye weight ya 4 na A kama kawaida. Hapa ni kwenye udahili wa chuo kikuu. 2014 ilibidi watu waliokuwa wamepewa daraja la nne(division four) nao wadahiliwe chuo kikuu kwa sababu walikuwa na sifa za udahili. Kwa mfano; mtu aliyepata DDE alikuwa na daraja la nne lakini anapoint 2.5 kwa mujibu wa TCU guide book. Mwaka 2015 ilibidi makosa haya yafichwe kwenye GPA.

Hivi elimu yetu ichezewe hivi mpaka lini? Je, ni kweli aliyefaulu alama za darasani vizuri ndiye mtu pekee aliye na akili chanya inayoweza kuleta mchango wenye manufaa kwenye taifa hili kiasi kwamba kila mwaka upangaji wa alama ubadilishwebadilishwe? Je, hawa watu hawajawahi kusoma historia ya Sir Isaac Newton mwenye mchango mkubwa kwenye Physics na Hesabu kuhusu ufaulu wake darasani? Kila mtu ana "Ujiniazi" wake. Hata yule wa mwisho darasani ana "Ujiniazi" wake endapo ukifuatiliwa utaugundua. Yawezekana akawa ni mchoraji mzuri sana, mchezaji mzuri sana au ni muimbaji mzuri sana.

Rai yangu kwa Ndalichako na wizara yake, sasa ni muda wa kuifikiria elimu "nje ya boksi" na si kuhangaika na alama na madaraja. Muda wa kumwambia mtoto "nenda shule, upate alama nzuri, utapata kazi nzuri na salama" umepita. Huo mfumo wa elimu hautatufikisha kokote. Kwa nini tusijiulize swali hili; mbona kuna maprofesa wapo ambao wanafanya mambo ya hovyo kuliko hata darasa la saba? Kuna mtu aliitwa Professor Machunda mnaelewa mwisho wake? Kwa nini Nyerere alimtoa kwenye system ya Uongozi? Acheni kuhangaika na madaraja njooni na jibu sahihi kwenye mfumo huu wa elimu.
 
Good idea asee, kila ili jambo linasemwa but hakuna anaye lifanyia kazi, viva former RC moro Dr??????
 
Kwa nchi yetu hakuna namna nyingine ya kupanga ufaulu zaidi ya haya madaraja.
 
Mara moja niliwahi msikia prof machunda,naskia aliishia kuwa (mkokozi) hata kifo chake,wale wakazi wa kanda ya ziwa watanielew maana ya neno hili ktk mabano.
 
Tz ya Ccm ya fikra mgando kila kitu niajaribio . Kama kimesemwa rasmi au lah lazima kitelekezwe au kuweka ktk mashelfu baada ya majaribio. Wenzetu wana tenda kwa kusikia tuu kelele zetu.
 
,Muundo wa Kwanza ni upangaji wa viwango katika ngazi ya Shule ambapo Alama Mgando (Fixed Grade
Ranges) zifuatazo hutumika kupanga madaraja: A = 81 – 100; B = 61 – 80; C = 41 – 60; D = 21 – 40 na F = 0
– 20. Muundo huu umetumika kwa muda mrefu na umezoeleka kwa walimu na wanafunzi wa elimu ya
sekondari kwa ujumla.
Muundo wa Pili ni wa viwango vinavyotumiwa na Baraza la Mitihani la Taifa ambapo ambapo kabla ya
mwaka 2012 muundo wa viwango nyumbufu (flexible grade ranges) ulitumika. Katika muundo huu uwigo
wa alama ulibadilika badilika kulingana na hali ya matokeo ilivyokuwa kwa mwaka husika. Lakini kuanzia
mwaka 2012, Serikali iliamua kutumia mfumo wa Upangaji wa Alama Mgando (Fixed Grade Range) kwa
Kidato cha Nne na Kidato cha Sita. Katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012 Baraza lilitumia mfumo
huu wa alama mgando ambapo: A = 80 – 100, B = 65 – 79, C = 50 – 64, D = 35 – 49, F = 0 – 34. Kwa
upande wa Kidato cha Sita Baraza lilitumia mfumo wa A = 80 – 100; B = 75 - 79; C = 65 – 74; D = 55 – 64; E
= 45 – 54; S = 40 – 44 na F = 0 – 39. Mifumo hii ya Baraza haikuwa inafahamika kwa wadau na hivyo kuwa
sehemu ya malalamiko katika sekta ya elimu na mafunzo.
,
 
Mwaka 2014 kwa kidato cha nne mtu aliyepata 30~39 kwa masomo yote alihesabika ana DDD na wengi wameenda chuo lakini mwaka 2012&2013 huyo mtu angelipata zero,.
 
,Muundo wa Kwanza ni upangaji wa viwango katika ngazi ya Shule ambapo Alama Mgando (Fixed Grade
Ranges) zifuatazo hutumika kupanga madaraja: A = 81 – 100; B = 61 – 80; C = 41 – 60; D = 21 – 40 na F = 0
– 20. Muundo huu umetumika kwa muda mrefu na umezoeleka kwa walimu na wanafunzi wa elimu ya
sekondari kwa ujumla.
Muundo wa Pili ni wa viwango vinavyotumiwa na Baraza la Mitihani la Taifa ambapo ambapo kabla ya
mwaka 2012 muundo wa viwango nyumbufu (flexible grade ranges) ulitumika. Katika muundo huu uwigo
wa alama ulibadilika badilika kulingana na hali ya matokeo ilivyokuwa kwa mwaka husika. Lakini kuanzia
mwaka 2012, Serikali iliamua kutumia mfumo wa Upangaji wa Alama Mgando (Fixed Grade Range) kwa
Kidato cha Nne na Kidato cha Sita. Katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012 Baraza lilitumia mfumo
huu wa alama mgando ambapo: A = 80 – 100, B = 65 – 79, C = 50 – 64, D = 35 – 49, F = 0 – 34. Kwa
upande wa Kidato cha Sita Baraza lilitumia mfumo wa A = 80 – 100; B = 75 - 79; C = 65 – 74; D = 55 – 64; E
= 45 – 54; S = 40 – 44 na F = 0 – 39. Mifumo hii ya Baraza haikuwa inafahamika kwa wadau na hivyo kuwa
sehemu ya malalamiko katika sekta ya elimu na mafunzo.
,
Hivi ni kweli ubora wa elimu utapatikana kwa kuhangaika na ubadilishaji wa kupanga madaraja ya ufaulu?
 
Kwa nchi yetu hakuna namna nyingine ya kupanga ufaulu zaidi ya haya madaraja.
Mimi sina tatizo sana kupanga ufaulu kwa madaraja isipokuwa jinsi kila Waziri anavyokuwa na mtazamo na upangaji madaraja kama ndiyo njia pekee ya kuonesha elimu ni bora.
 
Back
Top Bottom