Hivi, dunia ilikwisha jana au?

Stevemike

Senior Member
Joined
Mar 12, 2011
Posts
117
Reaction score
15
Nilisikia mapema kuwa dunia ingeisha tr 21/05/2011. Nimejisahau nikajikuta nimefika tr 22. Naomba mniambie kilichotokea jana. Dunia iliisha jana? Nataka ukweli ili nichunguze mahala nilipo na nijue la kufanya.
 
chunguza mi sijui kama nipo ama la
 
Nilisikia mapema kuwa dunia ingeisha tr 21/05/2011. Nimejisahau nikajikuta nimefika tr 22. Naomba mniambie kilichotokea jana. Dunia iliisha jana? Nataka ukweli ili nichunguze mahala nilipo na nijue la kufanya.

hakuna ajuaye cku hiyo itakuwa lini au saa ngapi? ila MOLA tu, hivyo kama unamiungu mingine hapa duniani lazima ubabaishwe na upuuzi huu
 
Hivi siku hizi mpaka mapadre na wachungaji huwa wanatoa fatwa! Nikasema hee ndiyo tutawamiso ndugu zetu wa kikristo au vipi?

Samahani kama nimewakera.
 
huyo mchungaji aliyesema hivyo sijui leo aliwaangaliaje watumishi wake hapo kanisani kwake...mnh
 
Sikuoni huku heaven mie niko St. Luke street tuko na manabii wa kale sio wale wa bongo, wewe uko wapi au unaelekea hell
 
ndio nilipata vipepelushi vya taarifa hiyo March 2011 Arusha,lakini nilivipuuza kwa mwongozo wa vitabu vya Mungu,
kwa upeo wao ingekuwa mwisho ni mwisho kwao....sisi tuendelee na maisha
 
ni kweli dunia ilikuwa iishe jana kabisa, lakini kutokana na bei ya mafuta kupanda imebidi ihairishwe kutokana na abiria wa kuchoma kuwa wengi, kwa hiyo siku bei ya mafuta itashuka zoezi linaanza upya....
 
nahisi km niko hell vile maana ni GIZA TUPU, devil we know anaua watu pale TARIME, tena mwingine anazomewa kwenye mkutano wake, mlinzi wao mkubwa kaja tuko naye huku hell yaani watu wana magamba matupu ukiwauliza eti wanakushangaa mbona tushayavua yakheeee duh HELL ON EARTH!
 
ni kweli dunia ilikuwa iishe jana kabisa, lakini kutokana na bei ya mafuta kupanda imebidi ihairishwe kutokana na abiria wa kuchoma kuwa wengi, kwa hiyo siku bei ya mafuta itashuka zoezi linaanza upya....

hahahaaa! Preta leo umefanya niumize mbavu. Ama kweli wewe ni kiboko kwa kuchekesha! Eti ilihairishw kwa sababu ya bei ya mafuta!
 
mimi nilisema hapa jf kuwa ajuaye siku na saa ni Mungu tu lakini kwa dalili tulizo ambiwa dunia imekaribia mwisho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…