mastersajenti
Senior Member
- Dec 4, 2015
- 165
- 23
Nimeshangazwa sana na taarifa ya kuvurugika kwa uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Kinondoni. Kwa mujibu wa maelezo ya Mkurugenzi wa manispaa hiyo ni kwamba fujo zilizuka baada ya wajumbe wa CCM kutoka Zanzibar kuja kupiga kura Manispaa ya Kinondoni kumchagua Meya. Hakika jambo hili haliingii akilini kabisa Mzanzibari kuwa Mjumbe wa halmashauri ya Kinondoni kama sio vurugu za CCM katika nchi hii.
Ni vema viongozi wa CCM wakawa wanaheshimu maamuzi ya wananchi na kutii Sheria na kanuni za nchi hii. Sisi sote tuna haki ya kuongoza na kutawala sio CCM pekee. Uchaguzi wa bara uligubingwa na malalamiko, uchaguzi wa Zanzibar mpaka sasa una matatizo makubwa na chaguzi zote in CCM.
Nchi yetu ni ya amani na utulivu. Madiwani wa Kinondoni ndio kisheria wana haki ya kumchagua Meya wao, mbona uchaguzi wa mwaka 2010 wajumbe wa CCM kutoka Zanzibar hawakuja kumchagua Mh. Mwenda?
Kama kura hazitoshi kubalini matokeo.