Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi CCM kuna wasomi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by msnajo, Feb 8, 2011.

 1. m

  msnajo JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,075
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Wadau naomba kuuliza swali, ccm hakuna hata mmoja aliebahatika kusoma na akaelimika? Inakuaje chama kizima tena kikongwe barani Afrika kinakosa washauri na wataalam waliobobea mambo ymbalimbali!! Wameshindwa hata kumshauri Mwenyekiti wao mambo ya kuzungumza na wanamwacha anaingia kichakani! Kweli ukila na kipofu usimguse mkono. jK, mheshimiwa raisi unatueleza kuwa huwatambui wamiliki wa Dowans! What do you mean exactly?

  Haingii akilini uliposema kwamba ulikaa kimya kuwaachia wengine wazungumze kwa niaba yako like Ngeleja, halafu alichozungumza Ngeleja ni tofauti na wewe. Ina maana kama Ngeleja alizungumza kwa niaba yako iweje awafahamu wamiliki wa Dowans wewe ushindwe kuwatambua? Na wewe JK una uwezo wa kumaliza hili swala kwa kuamuru kutokulipwa Dowans na kumfungulia mashtaka Ngeleja kwa kuudanganya umma kwa kututajia majina ya uoogo. Au ni nani mkweli kati yako JK na Ngeleja? Jamani Watz huu uranii wa raisi wetu ni hadi lini.

  Kuna maswala nyeti na muhqgmu kwa Taifa ambayo angeweza kuzungumza cku ya ccm, wewe anajichekesha na kutuambia akutukanae hakuchagulii tusi, ulielezwa ukweli siku hizi umetukanwa? Namwomba raisi aache mzaha na maisha ya Watz, huu mfumuko wa bei wa kutisha namna hii hauoni,, mi sijui ni Taifa gani anaongoza. Wenzake wote wamemuacha mbali kabisa, angalia Rwanda Na Burudi, majuzi tu walikua vitani leo hii wameshajitutumua na safari ya mafanikio inaonekana wazi bila kusahau Angola.. Raisi wetu amepotea na hajuph hata afanye lipi na aache lipi?

  Anatafuta cheap popularity kwa kujichekesha kwa watu waliochoshwa na maisha? Amefikia mahalph anadhubutu kusema eti hata Nyerere alikuwa na makosa, kama ndivyo hiyo ndo sababu ya kufanya madudu kwa kuwa mtangulizi wako alikosea mahali kwa hiyo anashindana nae kiuzembe badala ya ufanisi. Kwangu mimi huku ni kutokujitambua na nafika mahali na kujiuliza huko CCM hakuna wasomi wenye uwezo wa kumshauri JK ajaribu kuzidigest hotub zake kabla yakusoma kama gazeti? Hawa madoka Chami, Davidi, Mwakyusa, Lukuvi, n.k wamesomea wapi elimu zao kiasi kwamba huyo udaktari falsafa haipo kabisa. Raisi ambaye amekua ombaomba ili hali Nchi yake ina utajiri wa kupindukipa hana maana kabisa, na hafai. Nawaomba wasomi wetu wachukue hatamu ya kumshauri JK hata kama hawapo CCM, watumie taaluma zao kutuletea mabadiliko chanya.
   
 2. F

  FUSO JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 9,838
  Likes Received: 366
  Trophy Points: 180
  sikio la kufa ndugu yangu...

  bado anafikiri watanzania ni mazezeta, yes badala ya kuongelea mfumuko wa bei na maisha kupanda wao wanasema ni mambo ya kawaida - chama limezeeka na nawazo yamezeeka pia. kuongozwa na chama chenye mawazo ya mwaka 47, kisicho kuwa na dira wala mwerekeo hizi ndiyo gharama zake.

  Watanzania inabidi tufunge mikanda, hii nchi haina mwenyewe kwa sasa, ndiyo tumeshaingia kwenye hili gari moshi lisilo na mwelekeo ndugu zangu - eee mwenyezi mungu tuokoe tunaangamia wana wako.
   
Loading...