Hivi CCM hakuna uchaguzi wa mwenyekiti?

Ntile II

Member
Nov 19, 2015
22
12
Nimeisoma taarifa ya msemaji wa chama Ndugu Ole Sendeka inaonesha kwamba tarehe 23/July kuna makabidhiano ya Kijiti cha Mwenyekiti.

Sasa najiuliza, hakuna tangazo la kuchukua wala kurudisha fomu! Pia hakuna kujinadi wala kunadiwa!

Nadhani mfumo wa kukabidhiana ulifaa sana kwa miaka 1960s, 1970s, 1980s lakini sio katika zama hizi?

# Demokrasia
 
# Domokrasia

Kwani UKAWA wakati mnachagua mgombea urais 2015 nani alichukua fomu?
 
Nimeisoma taarifa ya msemaji wa chama Ndugu Ole Sendeka inaonesha kwamba tarehe 23/July kuna makabidhiano ya Kijiti cha Mwenyekiti.
Sasa najiuliza, hakuna tangazo la kuchukua wala kurudisha fomu! Pia hakuna kujinadi wala kunadiwa!
Nadhani mfumo wa kukabidhiana ulifaa sana kwa miaka 1960s, 1970s, 1980s lakini sio katika zama hizi?
# Domokrasia
Kwani kuna chama wanatangaza nafasi za kuwania uenyekiti ?huenda Chadema,hata hao CUF ,chaguzi zao ni kiinimacho tu Maalim mara ajiteua kuwa katibu mkuu mara ajiteue kuwa Mwenyekiti ,hukoCUF ni Maalim ndie huteua wengine wote ni yakheehatuwezi kumpinga maalim atii
 
Kuhusu suala la demokrasia ya ndani ya vyama hasa kwenye kukabidhiana Uenyekiti, vyama vya upinzani havina sifa ya kukosoa kabisa. Kuna watu ni wenyeviti 20 years plus. Ndio maana hiyo ya nyani haoni mkundue iko sahihi kabisa.
 
Yaani uenyekiti CCM taifa ni kama kuvalishana joho la ukamanda baada ya kuwa uchaguzi inageuka sherehe ya kumtangaza mwenyekiti
 
hakuna chama kinachokiuka katiba yake chenyewe kama ccm kamwe. eti mtu ambaye hayupo kwenye mlolongo wa chama anapewa uongozi kama njugu. mweh...
 
Nimeisoma taarifa ya msemaji wa chama Ndugu Ole Sendeka inaonesha kwamba tarehe 23/July kuna makabidhiano ya Kijiti cha Mwenyekiti.
Sasa najiuliza, hakuna tangazo la kuchukua wala kurudisha fomu! Pia hakuna kujinadi wala kunadiwa!
Nadhani mfumo wa kukabidhiana ulifaa sana kwa miaka 1960s, 1970s, 1980s lakini sio katika zama hizi?
# Domokrasia
Unasubiri fomu CCM? pole sana ni sawa na kusubiri meli airport.
 
Nimeisoma taarifa ya msemaji wa chama Ndugu Ole Sendeka inaonesha kwamba tarehe 23/July kuna makabidhiano ya Kijiti cha Mwenyekiti.
Sasa najiuliza, hakuna tangazo la kuchukua wala kurudisha fomu! Pia hakuna kujinadi wala kunadiwa!
Nadhani mfumo wa kukabidhiana ulifaa sana kwa miaka 1960s, 1970s, 1980s lakini sio katika zama hizi?
# Domokrasia
Wewe unaona uenyekiti wa CCM tu. Urais wa nchi ya wadanganyika unafanywa kwa style hiyo hiyo tu kupitia usanii wa "uchaguzi mkuu" na Tume "huru" ya kivuitu. Polisi na Jeshi linatumika kuzuia "fyokofyoko" ili usimikaji wa mtawala asiyependa kutawaliwa alete ndoto ya Taifa la viwanda vya majipu, viwanda vya matamko, viwanda vya maisha ya kishetani, viwanda vya kufanya maombi ,kumwombea mwenye mamlaka kuwapiga wadanganyika kwa maisha magumu kwa mwendokasi na kuwageuza makasuku wa kuimba "mfalme amevaa joho la kioo linalomeremeta"

Hii ni nchi ya Domo-krasi

Mwandishi mmoja aliandika kuhusu "nchi ya kusadikika". Hii ya kwetu ni nchi ya kusadikikana. Nchi ya "makwanjanja, wapumbavu na malofa na walamba viatu vya watawala, nchi ya watu ovyo ovyo"
 
Back
Top Bottom