Hivi Bendi za Dansi za Tanzania huwa zinajifunza kweli kutoka kwa wenye Mziki wao Wakongo au Bandeko Nangai?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,542
108,877
Nimewahi Kuhudhuria ' Shows ' za Mashujaa Band na Twanga Pepeta huko nyuma ambako ' interest ' yangu Kubwa ilikuwa ni kuona tu Kwanza jinsi wanavyofanya ' Maandalizi ' yao pale Jukwaani hasa kwa Kupangilia Vyombo vyote kabla ya Kuanza ' Kuporomosha ' Masebene na kudhani kuwa Wao ndiyo walikuwa ' Mafundi ' sana kumbe wapi.

Wakati Bendi za nyingi za Tanzania zikichukua / zikitumia takribani Masaa kati ya Mawili au Moja katika ' Maandalizi ' yao na wenyewe wakidhani wamepatia na Kukamilisha kila Kitu nilichokishuhudia kwa wenye ' Mziki ' wao Wakongo ( zamani Wazaire ) au Bandeko Nangai ni tofauti kabisa na hapa sasa ndiyo nadiriki kusema kwamba Wakongo wanapiga Muziki na Watanzania tunajaribu kupiga Muziki.

Ni kwamba Bendi yoyote kutoka nchini Kongo ikiwa inapiga ' Show ' yake Saa Moja usiku basi Wataalam wa Muziki wa Bendi hasa wa ' Sound ' pamoja na Wanamuziki ' Waandamizi ' kadhaa watafika pale Saa Nne asubuhi ambapo wataanza Kujipanga kwa ' Kuseti ' kila Chombo ambacho Kitatumika huku wakihakikisha kwamba kila Chombo kinasikika vyema.

Na hata pale ambapo wakimaliza Kupanga kila Kitu na Kuandaa wapo ambao huondoka eneo la tukio lakini kuna wengine hasa wale Wataalam wa Sound hubaki pale pale kuhakikisha hakuna tatizo lolote litakalojitokeza. Na labda kwa msiojua tu taarifa iwafikieni kwamba zile nyimbo zote ambazo huwa mnaona zinapigwa Kwanza wakati ' Show ' ikianza huwa ni za ' Majaribio ' tu ambapo pale kinachoangaliwa sana ni Sauti imekaa vipi, Vyombo vyote vinapiga sawasawa na ' Mzuka ' wa Watu pale upoje.

Kama kuna Kitu ambacho Wanamuziki wa Kikongo hawakipendi na huwa wanakuwa Wakali nacho ni pale wanapoona Uwanja / Ukumbi umejaa Watu wametoa Viingilio vyao halafu wanapiga vibaya nyimbo au hawawaridhishi na ndiyo maana basi hata ' Maandalizi ' yao kabla ya ' Show ' kuanza huwa ni ' Kabambe ' ambapo hata Wewe ukihudhuria huwezi Kujutia kutoa ' Kiingilio ' chako Kikubwa na unaridhika kabisa.

99% ya Bendi za Muziki wa Dansi za nchini Tanzania huwa hawafanyi ' Maandalizi ' ya Kiutaalam na Kiufundi kama hawa Wakongo na pengine ndiyo maana hata Mimi GENTAMYCINE bado hujanishawishi niwe nahudhuria kutokana na kwamba Wanamuziki wengi wa Bendi za Dansi za Tanzania hawako ' that serious ' na wanachojua wao ni ' Kulipualipua ' tu Kimaandalizi kisha Watu wakijaa Ukumbini / Uwanjani pale wanaanza kupita taratibu ' Kugongea ' Bia na Mvinyo.

Kweli nimeamini kwamba Mwenyezi Mungu aliamua ya kwamba........

Brazil itawale kwa Mpira wa Miguu duniani
Congo itawale kwa Muziki wa Dansi duniani
Tanzania itawale kwa ' Ujanja Ujanja ' duniani
Israeli itawale kwa Uwerevu duniani
Rwanda itawale kwa Ushujaa, Upambanaji na Uzalendo duniani
Urusi na Venezuela zitawale kwa Wanawake Warembo duniani
Waingereza watawale kwa Ubahili uliotukuka duniani

Shikamooni Wakongo!

Nawasilisha.
 
Tz tuna mziki wetu,wengine pia waje kujifunza kwetu,sio wakongo tu hata wanaotoka Ulaya,Asia na marekani waje tu kujifunza...!unyonge mwengine ni wa kujitakia.
 
Umeandika kishabiki zaidi ya uhalisia ulivyo. Rwanda ina ushujaa gani!!? Ushujaa wa kuchinjana 1994!? Kwanini mashujaa tusiwe sisi tuliomuondoa Nduli Amini aliyewashinda Waganda? Turudi kwenye mada: Mziki wa dansi tumeiga kutoka huko Congo kama ambavyo ukitembelea majimbo ya Congo utakuta vijana wanasikiliza kwa umakini na kuiga uimbaji wa vijana wetu (Diamond, Kiba, Mavoko nk) maana kiuhalisia zama za mziki wa dansi hata huko Congo ndo zinatokomea zake, vijana hawavutiwi sana na mahadhi na miondoko ile zaidi wanavutiwa na mziki wa kisasa. Dansi umebaki kuwa mziki wa viongozi na watu wazima, kifupi: Congo wana mziki wao (Dance) ambao wanauweza sana nasi tuna mziki wetu (BongoFlavour) ambao wanautamani sana.
Nimewahi Kuhudhuria ' Shows ' za Mashujaa Band na Twanga Pepeta huko nyuma ambako ' interest ' yangu Kubwa ilikuwa ni kuona tu Kwanza jinsi wanavyofanya ' Maandalizi ' yao pale Jukwaani hasa kwa Kupangilia Vyombo vyote kabla ya Kuanza ' Kuporomosha ' Masebene na kudhani kuwa Wao ndiyo walikuwa ' Mafundi ' sana kumbe wapi.

Wakati Bendi za nyingi za Tanzania zikichukua / zikitumia takribani Masaa kati ya Mawili au Moja katika ' Maandalizi ' yao na wenyewe wakidhani wamepatia na Kukamilisha kila Kitu nilichokishuhudia kwa wenye ' Mziki ' wao Wakongo ( zamani Wazaire ) au Bandeko Nangai ni tofauti kabisa na hapa sasa ndiyo nadiriki kusema kwamba Wakongo wanapiga Muziki na Watanzania tunajaribu kupiga Muziki.

Ni kwamba Bendi yoyote kutoka nchini Kongo ikiwa inapiga ' Show ' yake Saa Moja usiku basi Wataalam wa Muziki wa Bendi hasa wa ' Sound ' pamoja na Wanamuziki ' Waandamizi ' kadhaa watafika pale Saa Nne asubuhi ambapo wataanza Kujipanga kwa ' Kuseti ' kila Chombo ambacho Kitatumika huku wakihakikisha kwamba kila Chombo kinasikika vyema.

Na hata pale ambapo wakimaliza Kupanga kila Kitu na Kuandaa wapo ambao huondoka eneo la tukio lakini kuna wengine hasa wale Wataalam wa Sound hubaki pale pale kuhakikisha hakuna tatizo lolote litakalojitokeza. Na labda kwa msiojua tu taarifa iwafikieni kwamba zile nyimbo zote ambazo huwa mnaona zinapigwa Kwanza wakati ' Show ' ikianza huwa ni za ' Majaribio ' tu ambapo pale kinachoangaliwa sana ni Sauti imekaa vipi, Vyombo vyote vinapiga sawasawa na ' Mzuka ' wa Watu pale upoje.

Kama kuna Kitu ambacho Wanamuziki wa Kikongo hawakipendi na huwa wanakuwa Wakali nacho ni pale wanapoona Uwanja / Ukumbi umejaa Watu wametoa Viingilio vyao halafu wanapiga vibaya nyimbo au hawawaridhishi na ndiyo maana basi hata ' Maandalizi ' yao kabla ya ' Show ' kuanza huwa ni ' Kabambe ' ambapo hata Wewe ukihudhuria huwezi Kujutia kutoa ' Kiingilio ' chako Kikubwa na unaridhika kabisa.

99% ya Bendi za Muziki wa Dansi za nchini Tanzania huwa hawafanyi ' Maandalizi ' ya Kiutaalam na Kiufundi kama hawa Wakongo na pengine ndiyo maana hata Mimi GENTAMYCINE bado hujanishawishi niwe nahudhuria kutokana na kwamba Wanamuziki wengi wa Bendi za Dansi za Tanzania hawako ' that serious ' na wanachojua wao ni ' Kulipualipua ' tu Kimaandalizi kisha Watu wakijaa Ukumbini / Uwanjani pale wanaanza kupita taratibu ' Kugongea ' Bia na Mvinyo.

Kweli nimeamini kwamba Mwenyezi Mungu aliamua ya kwamba........

Brazil itawale kwa Mpira wa Miguu duniani
Congo itawale kwa Muziki wa Dansi duniani
Tanzania itawale kwa ' Ujanja Ujanja ' duniani
Israeli itawale kwa Uwerevu duniani
Rwanda itawale kwa Ushujaa, Upambanaji na Uzalendo duniani
Urusi na Venezuela zitawale kwa Wanawake Warembo duniani
Waingereza watawale kwa Ubahili uliotukuka duniani

Shikamooni Wakongo!

Nawasilisha.
 
Mkuu,umeandka ukweli mtupu kwenye upande wa music wa Lingala/Kongo
Kuna baadhi ya wanamuziki nchini Kongo huwa wanawaajiri sound engineer kwaajili ya kuhakikisha panakuwepo na mpangilio mzur wa sauti kwenye kazi zao na hata live shows!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom