Hivi ACT-Wazalendo kujaza watu mkutanoni ndio kukubalika?

ngogo

JF-Expert Member
Oct 19, 2012
359
54
Kwa wale wapambe na wafuasi waaminifu wa Zitto Kabwe wanajitahidi sana kujinasibu kuwa Zitto Kabwe ni mwanasiasa tishio kwa Tanzania ya sasa.

Hawaishii hapo tu, wanajaribu kuitumia mitandao ya kijamii kuwaaminsha Watanzania kuwa Zitto na genge lake watawasambalatisha UKAWA kwa kuwa mikutano yao inajaza sana watu.

Mimi nasema kujaza watu sio tatizo lakini hao watu waliojaa mudi zao zinakuwaje wanaposikiliza mikutano yenu? au anawapokeaji pale mnapomaliza maneno yenu mnayolombo?

Watanzania hawako hivyo kama wawazavyo wajinga, wao wakishamtilia mtu mashaka kumuamini ni kazi ngumu.

Watanzania sio watu wa kuwageuza geuza kama unavyotaka wewe, na suala la kupata watu wengi katika mikutano yenu sio issue.

Kama hili hamuamini basi asiwepo Zitto bali Mwigamba na Mchange waenda katika uwanja wowote na ikapo kilichofunikwa kitambaa chekundu na kujifanya waganga wakienyeji patajaa watu wenyewe watashangaa
.
 
Nlisikia eti alizoa wanachama zaidi ya elfu moja.....wakati mwingine ndio maana huwa najipa likizo ya kushabikia siasa
 
Hiyo ni dalili ya kukubalika na kupendwa, si mchezo watu waache shughuli zao waje kukusikiliza, andaa mkutano wewe uone kama kuna mtu atakuja, Zitto anapendwa sana

Oktoba mzizi wa fitna ndo utakatwa na tutajua anapendwa mtu au kitu
 
Hivi unaweza kuuliza swali la namna hii, unajua unaweza anzisha thread halafu kiongozi wako mkuu akaipitia unasababisha apatwe na mshtuko kuona anawafuas wasi jielewa hawajui msing wa chama ni nn! tumesha wazowea na mwakahuu mpaka mtakosa lakuandika hum
 
Hii ni dalili ya kukubalika sana. Angalia CUF kama wanaweza kuandaa mkutano mikoani tofauti na Pwani Pwani huko. Au andaa wa kwako uone kama watakuja watu kwa sababu ya upya.
 
huu mwezi mvua nyingi na watu washapalilia hakuna kzi ukipata mda unaenda kushangaa nyago.
 
Back
Top Bottom