Hitaji la ukumbi wa kufanyia Sherehe ya Sendoff

Hitaji la ukumbi wa kufanyia Sherehe ya Sendoff

MjombaRiziki

Senior Member
Joined
Feb 14, 2013
Posts
145
Reaction score
129
Habari za leo wakuu!

Nijikite moja kwa moja kwenye Mada. Natarajia kuozesha binti yangu katikati ya mwezi wa Sita mwaka huu, nategemea kumfanyia Sherehe ya kumuaga-SendOff.

Nahitaji Ukumbi wa kuweza kutosha watu wasiopungua 200, naishi Kongowe na Ukumbi uwe Maeneo ya Kilwa Road kuanzia Bendera Tatu-Kurasini hadi Mtoni kwa Aziz Ally ili iwe rahisi kwa Watu wengine kuja kujumuika.

Nilitegemea kupata Kumbi za Pale Sabasaba Maonesho lakini kwa kipindi ninachotarajia kufanya hio shughuli kumbi hizo hazitopatikana kwa sababu ya Maandalizi ya Maonesho ya Sabasaba.
Nawasilisha!

================
UPDATE;
Wakuu Ahsanteni kwa Michango ya Mawazo.
Kiufupi tayari nimepata Ukumbi wa Baraza la Maaskofu - KURASIINI

AHSANTENI
 
Pale Mgulani JKT kuna ukumbi wa kukidhi hitaji lako mkuu.
Asiporidhika na Mgulani aingie Ndani ya Viwanja vya Sabasaba achague Hitaji la Moyo wake naaamini atapata Ukumbi murua kwa bei ya Kizalendo.
 
Asiporidhika na Mgulani aingie Ndani ya Viwanja vya Sabasaba achague Hitaji la Moyo wake naaamini atapata Ukumbi murua kwa bei ya Kizalendo.
Mkuu ZAMDELA kama nilivyoeleza kwenye Uzi wangu kumbi kwenye Viwanja vya Sabasaba Hazikodishwi wanaziandaa kwa ajili ya Maonesho ya Sabasaba
 
Nilitegemea kupata Kumbi za Pale Sabasaba Maonesho lakini kwa kipindi ninachotarajia kufanya hio shughuli kumbi hizo hazitopatikana kwa sababu ya Maandalizi ya Maonesho ya Sabasaba.
Nawasilisha!
Ulishafika pale Equator Grill?!! Kama bado basi fanya haraka kwa sababu mwezi wa 6 sio mbali, na hizi kumbi zinakuwa na demand sana; kwahiyo unatakiwa kuwahi kufanya booking.
 
Mkuu ZAMDELA kama nilivyoeleza kwenye Uzi wangu kumbi kwenye Viwanja vya Sabasaba Hazikodishwi wanaziandaa kwa ajili ya Maonesho ya Sabasaba
Kwenye mitihani wanakwambia soma maelezo kikamilifu kabla ya kujibu swali nahisi jamaa atakuwa akifeli mara kwa mara kwa kutosoma maelezo kikamilifu
 
Back
Top Bottom