Historia ya Mzee Kipusa

Hakuna watu wanaoabudu MIZIMU kama MACHIFU...

Kila kitu kwao kuanzia uongozi wao..

Kuzaliwa watoto...

Kuoa...

Mvua nk...vyote waliomba mizimu

Naomba usimame na Mungu sana...

Maana una vita kubwa...
Amina.

Note: Yeyote ambae alikua akifika pale kijijini ilikua lazima achanjwe chale na yule Babu.

Huyu chifu alizikwa huku amekaa! Alikua ni Kiongozi mwenye HEKIMA na Busara sana....
 
Amina.

Note: Yeyote ambae alikua akifika pale kijijini ilikua lazima achanjwe chale na yule Babu.

Huyu chifu alizikwa huku amekaa! Alikua ni Kiongozi mwenye HEKIMA na Busara sana....
Mnamaagano makubwa...

Unakazi kubwa ya kuyavunja...

Ila usimame upande mmoja, isiwe Leo kwa Mungu kesho kwa mganga...

Utawehuka...
 
Seek Medical Help.
Nimewahi kufanya.....tena kwà kujipeleka mwenyewe. Nilienda katika hospital maarufu Dodoma...yule doctor akanikatalia ....akanipa councelling tu. Baada ya kumwambia situation ninayopitia....na kwakua nilikua na bima ya Afya akanipa hifadhi pale hospitalini kwenye wodi VIP. Cause wakati huo nilikua homeless....nilikua nalala pale Railway Station , Dodoma kwenye Jumba la Wasafiri. Afu ikifika Asubuhi naenda kupiga mishe za kuosha magari.

KILA ilivyokua ikifika mid night kuna askari wakawa wanapita mule ndani kukagua kama waliomo mule wote ni Wasafiri.....

Jamaa walinikuta zaidi ya mara 4...KILA siku nawapanga tu. Nikaona naweza kukamatwa na kupelekwa kwà Afande Muroto ( huyu alikua anapenda kuwaonyesha wazururaji kwenye vyombo vya habari ) .

Ndio nikaamua kukimbilia hospitali ya general Dodoma, wakaniambia siumwi chochote...nakawaomba nilazwe wakasema hawawezi kufanya hivyo.

Nikaenda hospitali nyingine....huko mako docta akataka kukataa , alikua ni kijana ( nikamsihi sana..maana ilikua kipindi cha mvua / mwili wangu ulikua umedhoofika sana ) baadae akanionea huruma na kunipa hifadhi.
 
Hali yako ya Afya ya akili iko sawa mkuu?
My friend...ni kwamba sijapata nafasi ya kuonyesha uwezo wangu. Ni kama kuna stambling block....

Nina amini nikipewa nafasi hata kwà majaribio tu. Nitafanya vizuri sana. Na hayupo ambae ataona kama nina SHIDA ama Changamoto kichwani. Haya ni mapito tu Ndugu. Nimepitia mitihani mingi sana sana. Mizito
 
 
Pole sana MzeeKipusa njoo PM mzee wangu , nisamehe nilikuwa nikiona mambo yako nikahisi changamsha genge ila sasa nimekujua na nimeshakutambua .

Njoo Dm walau tuendelee kugawana kidogo baba .

Pole sana kwa yote japp dunia duara sikujua kama wewe ndiye wa leo hakika Maisha ni duara
 
Shida inaweza kuwa hapa,Unaweza kuwa kwenye Midlif Crisis ya mapema,au Fortunes zako zimekaa vibaya,Jaribu kufanya meditation kwa wingi,kama unatumia kilevi chochote acha kabisa,Na uache tabia ya kuwaza shida na magumu unayopitia na badala yake tazama ule wema ambao Mungu anakutendea.Mengine Tayari unayajua ya kufanya
 
Keep talking brother it heals....
Nimewahi kuishi katika stand kubwa kubwa za mikoa tofauti...kwenye majumba ya Wasafiri. Nimelala sana kwenye mabenchi.

Nimewahi kutembea kwà miguu kuanzia Asubuhi mpaka usiku , maeneo tofauti tofauti hapa TANZANIA. ( Kwasababu ya Kukosa nauli ya bus )

Nimejishughulisha kufanya Kazi ndogo ndogo nyingi uzijuazo wewe..but to no avail.

Nimesotea Kazi sana migodini. Kiufupi nimepambana sana...kutafuta ridhiki...mpaka kariakoo nilitaka kujaribu kulalia box ...

Sijui NIMEMKOSEA NINI MUNGU wangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…