Historia ya Kampuni ya Apple Inc.

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,439
Mwaka 1975 vijana watatu wataalamu wa kompyuta wenye vipaji vya ubunifu walikua wameajiriwa katika kampuni ya utengenezaji video games iitwayo Atari Interactive. Vijana hao ni Steve Jobs, Steve Wozniak na Ronald Wayne.

Wakawa marafiki wakubwa na wakakubaliana waache kazi ili wafungue kampuni yao. Mwaka 1976 wakaacha kazi. Wayne akapewa jukumu la kusajili kampuni. Ndiye aliyeandika mpango kazi wa biashara yao (business plan), kubuni Corolporate IDs (logo, slogan, phylosophy) na kuandika mkataba. Wayne alikua kama mlezi wa biashara hiyo kwa sababu wakati huo yeye alikua na umri wa miaka 42, Wozniak miaka 25 na Jobs miaka 20.

Kwahiyo Jobs na Wozniak walimtizama Wayne kama kaka aliyebeba maono yao. Mwaka 1976 kampuni ikasajiliwa na ikaitwa Apple Computers ikijikita ktk utengenezaji wa Kompyuta.

Wakagawana hisa. Ronald akachukua 10%, Jobs na Wozniak wakagawana 45% kila mmoja. Jobs akateuliwa kuwa Afisa Mtendaji mkuu (CEO) wa kampuni hiyo akiwa na miaka 21 tu.

Siku chache baadae kampuni yao ikapata 'order' ya kutengeneza Kompyuta 100 kutoka Byte Shop (duka la rejareja la kompyuta mjini Carlifonia). Lakini Kampuni hiyo haikua na mtaji wa kutengeneza Kompyuta hizo. Hivyo Jobs (kama CEO) akaenda bank kuchukua mkopo wa $15,000 kama (TZS 30M) kwa ajili ya biashara hiyo.

Ronald Wayne akawa na wasiwasi kwamba biashara hiyo inaweza isifanikiwe na wakashindwa kurejesha mkopo waliochukua. Kwa kuwa biashara yao ilikua ya ubia (Partnership) ina maana kama wangeshindwa kurejesha mkopo basi mali zao binafsi zingeuzwa kufidia deni.
Waune alipowatizama wenzake hakuna hata mmoja aliyekua hata na baiskeli. Walikua ndio vijana wanaoanza kutafuta maisha wakiwa na umri chini ya miaka 25. Yeye ambaye wakati huo alikua na miaka 41 tayari alikua na nyumba na magari kadhaa. Akaona mali zake ndio zitapigwa mnada kufidia deni.

Baada ya kutafakari akaamua kujitoa kwenye kampuni hiyo. April 12 mwaka 1976 akawaita wenzake na kuwaambia nia yake ya kujitoa. Akataka wamlipe 10% ya hisa zake ili wabakie wawili.

Hisa za Ronald zilikua na thamani ya $2,300 (kama 5M za kitanzania). Lakini akina Jobs na Wozniak hawakuwa na fedha za kutosha kumlipa. Wakamlipa kwanza $800 na baada ya mwaka mmoja wakamalizia $1,500 iliyobaki.

Kampuni ya Apple ikaendelea kukua siku hadi siku. Wakafanikiwa kulipa mkopo na kuendea kukuza mtaji wao kidogo kidogo. Kufikia mwaka 1980 kompyuta zake zilikua zinafanya vizuri sokoni zikishindana na Makampuni makubwa wakati huo kama IBM na HP.
Mwaka 1978 Jobs na Wozniak walimshawishi Wayne arudi kwenye kampuni yao lakini alikataa. Mwaka 1979 walimrudishia 10% ya hisa zake na kumtaka awalipe kiasi cha $5000 tu lakini akakataa 'offer' hiyo pia.

Mwaka 1980 Apple wakaingia hisa zao sokoni kwa mara ya kwanza katika soko la awali (IPO) ili kupata fedha za kukuza mtaji. Zikauzwa $22 kwa hisa moja. Kutokana na watu kununua sana zikapanda na kufikia $29 kwa hisa moja ndani ya muda mfupi.

Biashara ya hisa ikawasaidia kukuza mtaji wao kufikia $1.778Bil sawa na TZS Trilioni 4. Kadri miaka ilivyosonga kampuni hiyo ikaendelea kufanya ubunifu wa bidhaa mbalimbali za elektroniki na kutengeneza simu na vifaa vingine.

Mtaji wa kampuni hiyo uliendelea kukua na hadi mwaka 2011 kabla ya kifo cha Steve Jobs ulikua $450Bil sawa na TZS Trilioni 950. Kwa sasa umefikia $1Trilion sawa na TZS 2.5 Quadrillion. Hii ni sawa na budget yetu ya nchi kwa miaka 90 ijayo (under ceteris paribus).
_
Steve Jobs kupitia familia yake anamiliki 7.4% ya hisa zenye thamani ya $74 Bil sawa na TZS 180 Trilioni. Steve Wozniak nae anamiliki kiasi hichohicho cha hisa.

Nje ya hisa hizo Steve Jobs alifariki na kuacha ukwasi wa $217Mil sawa na TZS 500Bil na Steve Wozniak ana utajiri wa $116Mil sawa na TZS 270Bil.

Kama Ronald Wayne asingejiondoa kwenye kampuni hiyo, angekua anamiliki 10% ya hisa zenye thamani ya $100Bil sawa na TZS 250Trilioni. Lakini Ronald alipoteza fursa hiyo baada ya kujiondoa kwenye kampuni hiyo.

Hata hivyo Ronald anasema hajutii uamuzi wake wa kujitoa, pamoja na kwamba yeye ndiye aliyeandika mpango wa biashara wa kampuni hiyo.

Mwaka 2018 Ronald alihojiwa na kituo cha televisheno cha CNN akasema "Nafurahi kuona Apple imekua kampuni kubwa na inaendelea kufanya vizuri sokoni. Hata hivyo sijutii uamuzi wangu wa kujitoa. Kitu ninachojutia ni kwamba mpango wa biashara wa Apple niliuuza mwaka 1990 kwa $500 lakini mwaka 2016 mpango huo ulizwa kwa $1.6M"
_
Apple kwa sasa ina watumishi 13,000 na maduka 510 katika nchi 25 duniani kote. Mapato yake kwa mwaka ni $260Bil sawa na Trilioni 620 za kitanzania (bajeti yetu ya nchi kwa miaka 20 under ceteris paribus). Kwa sasa bei ya hisa moja ni $331 sawa na TZS 760,000/=.

Credit: G. Malisa

102391310_3058628124228859_4447185303002554501_o.jpg
 
Back
Top Bottom