Historia ya Joseph Kusaga

Clouds = Mawingu. Ilikuwepo mwanzoni mwa miaka ya 1990 wkati niko Arusha. Walikuwa wanapiga hapo disco lao hapo mjini kati karibu na mnara wa saa.

Ni kweli mitaa ya Goliondoi hapo. Wakiwa na Mr C.

Jo kakuta clouds imeshaanzishwa. Yeye kaiendeleza tu akishirikiana na Ruge.
 
Mambo mengine ni siri za kambi
 
Dah nimewakumbuka watayarishaji wa matamasha Enzi hizo kim&the Boyz Hawa walikuwa wanaanda matamasha kabla hata ya mawingu/clouds
Watoto wadogo hamuwezi kuelewa

Ova
Kim&Boyz ndiyo ilikuwa ya Magomelo?...
Enz za kina Digadiga,Black Moses ,Saba Jackson....
 
Clouds = Mawingu. Ilikuwepo mwanzoni mwa miaka ya 1990 wakati niko Arusha. Walikuwa wanapiga disco lao hapo mjini kati karibu na mnara wa saa.
Umenikumbusha mtu mmoja alikuwa anaitwa Athuman njahidi sijui yuko wapi
 
Am stand to be corrected

Kilichoitwa Mawingu Radio hakihusiani na clouds?

Aidha historia yako iko very shallow aisee kwa ukubwa wa clouds na Joseph na Ruge hazikupaswa kuwapo paragraphs chache kiasi hiki.



Sent from my itel W5001P using JamiiForums mobile app
 
Njaidi baadae walikwenda naye Dar wakati Clouds FM inaanzishwa. Akawa mtangazaji. Baadaye alikwenda USA. Sijui kwa sasa yuko wapi.
Umenikumbusha mtu mmoja alikuwa anaitwa Athuman njahidi sijui yuko wapi
 
Mbona hiyo historia ni kuduchu sana.

Joseph Kusaga..............
Alizaliwa lini
Baba yake ni nanMama yake nani
Alisoma shule zipi
Matokeo ya shule
Alianzia wapi disco(Clouds Disco Mwananyama,a?)
Clouds alia zia jengo gani
Kuungua kwa Studio ya kwanza.
Walipohamia
Sasa kampuni Zilipo
Picha za Joseph kusaga
Picha za Ruge
Kifo cha mbia Ruge
Wanavyoendelea sasa...............
...................
Hadithi iwe inajibeba!

Fanya research makini uto the whole story si robo robo.
 
Alipewa na Baba yake baada ya kupata mafao ya kustaafu kazi. Ndio maana Clouds ni mali ya familia ya Kusaga
 
Kim&Boyz ndiyo ilikuwa ya Magomelo?...
Enz za kina Digadiga,Black Moses ,Saba Jackson....
Marehemu Abdulhakim Magomelo alikuwa mtu poa sana.

Aliturusha sana kwenye "Yo Rap Bonanza" na concerts nyingine watoto wa mjini wa siku hizo.

DJ Kim mtu mmoja mtaratibu sana, halafu ana akili ya kuweza kukaa na watu wa kila aina, kuanzia wa Uswazi kina GWM mpaka wa Ushuani Masaki IST, wakorofi wa ghetto mpaka Waswalihina.

Alikuwa na apartment yake katikati ya mji hapa Mchafukoge ukipita kidogo tu ilipokuwa Billicanas.

Tulikuwa tunaenda tunapiga stories sana za mambo ya muziki na burudani.

DJ Kim anaandaa concert kubwa sana wanakuja mabishoo wote wa mjini. Wanakuja wagumu wote. Anatuunganisha tunafurahia muziki kistaarabu bila kujali tofauti zetu.

Lakini ukimuona alivyo mpole na mtaratibu hana majivuno hata huwezi kujua huyu ndiye DJ Kim Magomelo.

Umenitajia rafiki yangu umenikumbusha zamani sana Dar. Aliturusha sana.

RIP Kim Magomelo.

Alivyofariki gazeti la This Day lilimuandika hapa.
Home » Columnist
 
Nandy % yake iko wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…