Historia ya dhifa (banquet)

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,720
215,774
Dhifa ni chakula kinachoandaliwa kutoka tangulizi, mlo mkuu na kufuatia mlo baada ya chakula. Mara nyingi mlo huu huandalaiwa kwa heshima ya mgeni au ugeni na unafuatiwa na hotuba fupi. Katika ujenzi wa ofisi za serikali au nyumba za matajiri zamani walizingatia ujenzi wa banquet rooms. Vyumba hivi vinakuwa vikubwa vyenye paa lililoinuka kupisha mzunguko mzuri wa hewa.

Katika historia, baada ya mlo wa kwanza wa dhifa, wageni walikaribishwa katika chumba cha pili ambacho kilikuwa na mvinyo mtamu (sweet wine). Huko wageni walisimama wakisikiliza mziki wa ala uliosikika kwa mbali, hii ni kupisha watu wa huduma ya chakula (catering staff) kuondoa sahani, kubadilisha vitambaa na kuandaa mlo wa pili, hali kadhalika mlo wa pili ukimalizika mwenyeji aliongoza wageni kwenye chumba cha pili kupisha waandaji kufuata utaratibu uliofuata.

A_banquet_for_Babur.jpg


Picha hii ni mfano wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Babur mwaka 1507. Unaweza kuwaona watu wa catering wamesimama na mabakuli wakisubiri amri ya kubadilisha mabakuli.

Babur alitokea Persia na alifanikiwa kuanzisha dola ya Munghai nchini India mwaka 1504.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom