Papaa Azonto
JF-Expert Member
- Jun 30, 2013
- 319
- 277
kumbe real madrid ni kibonde wa liverpool.
Miongoni mwa mchezo unaotazamwa kwa jicho la tatu na mashabiki, wachambuzi wa masuala ya mpira wa miguu, wakiwemo wachezaji wenyewe ni mchezo kati ya liverpool mabingwa mara 5 wa kombe la ligi ya mbaingwa barani Ulay wanaotaka kulinda heshima ya wakubwa zao dhidi ya mabingwa mara 10 wa kombe hilo klabu ya Real Madrid.
Mechi hii inapewa uzito mkubwa ni kutokana na hisitoria iliyopo baina ya klabu hizi mbili. Liverpool ambao ni wenyeji wa mchezo wa leo wamekutana takribani mara 3 dhidi ya Real Madrid. Katika vipindi vyote hivyo vitatu Liverpool wamekuwa wababe wa real Madrid huku ushindi mkubwa wakiupata mwaka 2009 kwa jumla ya goli 4-0 katika uwanja wa Anfield.
Ikiwa kama hisitoria bado inaongea katika medani ya mpira wa miguu basi Liverpool watakuwa wanaingia uwanjani hali ya kuwa wanajua tayari wameshinda. Nachelea kusema hivi ni kutokana na historia nzuri waliyonayo majogoo hawa
Kwa ufupi ni kwamba kwa mara ya kwanza klabu hizi zilikutana mwaka 1981 katika fainali ya kombe la ulaya (European Cup) kwenye uwanja wa PARC DES PRINCES unaotumiwa na klabu ya Paris Saint-Germain ya nchini Ufaransa na Liverpool ikaibuka na ushindi wa goli moja lilifungwa na mlinzi wa pembeni(Left Fullback) Alan Kennedy.
Mara ya mwisho kukutana ilikuwa ni mwaka 2009 katika hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barani ulaya. Mechi ya kwanza ilikuwa 25/02/2009 ambapo Real Madridi walikuwa wenyeji. Adi firimbi ya mwisho inapulizwa Liverpool walitoka na ushindi wa goli moja lilifungwa na Yossi Benayoun katika dk 82.
Katika mchezo wa marudiano ulifanyika tarehe 10/03/2009 kwenye uwanja wa Anfield, Liverpool ilidhihirisha ubora wake mbele ya mashabiki wapatao 42,550. Magoli ya Liverpool yakiwekwa kimyani na mshambuliaji aliyekuwa hatari miaka 3 iliyopita Fernando Torres dk 16, Naodha Steven Gerrad 28 kwa penati, akardi tena katika dk 47 kablya ya beki Andrea Dossena kupigilia msumari wa dk 88 na hvyo Liverpool kusonga Mbele kwa ushindi wa Magoli 5-0.
Lakini Liverpool ya mwaka 2009 si hii ya leo, na pia Real Madrid ya mwaka 2009 si hii ya leo. Kikosi cha Liverpool kilichoitandika Real Madrid ya mwaka 2009 kimebadilika kwa takribani asilimia 90, mchezaji aliyebaki na aliyefunga katika mchezo ule ni mkongwe Steven Gerrad, wengine wamestaafu,wengine wameenda kutafta maisha pengine kama vile Fernando Torres na Alvaro Arbeloa ambaye anatazamiwa kuwepo katika mchezo wa leo akiwa kama mchezaji wa Real Madrid.
Kwa upande wa Real Madrid ni kama asilimia 80 ya kikosi cha wachezaji walioondoka au kustaafu, na hivyo asilimia iliyobaki ya wachezaji walikuwepo kwenye kikosi kilichopigwa 5-0 na Liverpool ni kama 20 %, Wachezaji hao ni golikipa Ikar Casillas, Pepe, Sergio Ramosi pamoja na Marcelo. KUELEKEA MCHEZO WA LEO. Vikosi vyote hivi vinamabadiliko makubwa sana. Huku Real Madrid ikiwa na kikosi bora zaidi kuliko Liverpool kwani Klabu ya Real Madrid inawachezaji wenye kuamua ushindi dakika yeyote.
Kinachoweka uzito katika mchezo wa leo ni historia iliyopo baina ya vilabu hivi viwili, Liverpool wanaotaka kuendelea umwamba hali ya kuwa Real Madrid wao wanataka kulipiza kisasi
Ukimuuliza mshabiki wa Liverpool kuhusu mchezo wa leo kwa haraka haraka atakuambia "aah maswali gani hayo, hujui kuwa Real Madrid ni kibonde wetu" mwingine atakujibu "kaka historia inaongea," kwa wachache wanaojua watakuambia "mchezo wa leo ni mgumu basi" kwani wanakijua kikosi chao kilivyo ikwemo mapungufu yake.
Kwa upande wa Real Madrid wao watakuwa wanawaza kwenda kulipiza kisasi huku wakitambua kuwa kucheza katika uwanja wa Anfield ni pagumu kuibuka na ushindi kutokana na kelele za mashabiki wa klabu ya Liverpool.
Mchezaji anayetazamiwa kuwa mwiba mkali kwa mabeki wa Liverpool Christiano Ronaldo amekiri na kuwataadhalisha wachezaji wake kuwa makini kwani anfield ni uwanja mgumu na kuongeza kuwa hata kama Liverpool wangefungwa goli 10 na QPR katika mchezo wa ligi mwisho mwa wiki iliyopita bado angekuwa na wasasi mkubwa kutoka kwa mashabiki ambao kwa takribani miaka 5 hawajaiona klabu yao ikishiriki ligi ya mabingwa ulaya, chanzo Alvaro Arbeloa www.telegraph.co.uk
Ukiachalia hilo, klabu ya Real Madrid mwishoni mwa wikii hii itakuwa na mchezo mgumu wa ligi dhidi ya Barcelona. Hivyo klabu hii inatazamiwa kucheza hali ya kuwa ikielekeza mawazo yake pia katika mchezo huo wa mahasimu wao wakubwa
Michezo 5 waliyocheza Liverpool kabla ya leo, imeshinda michezo 2 ya ligi na mmoja wa kombe la ligi. Ikitoka sare ya kufungana goli 1-1 dhidi ya Evarton, na Kupoteza mchezo mmoja wa ligi ya mabingwa dhidi ya FC Basel ya nchini Switzerland
Wapinzani wao Real Madrid wameshinda mechi zao zote 5 kablya ya leo, wameshinda mechi 4 za ligi, na moja ya ligi ya mabingwa dhidi ya Lodogorets ya nchini Bulgaria. chanzo ni Geitanyumbani.blogspot.com