Kizuio
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 845
- 522
Historia ya Tanzania inahusu eneo la Afrika Mashariki ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nchi ina mabaki ya kale sana ya zamadamu (kiumbe aliyekaribiana na binadamu kwa umbile). Sehemu ya Bonde la Ufa, kama Bonde la Oltupai (zamani Olduvai Gorge) lililoko ndani ya hifadhi ya Serengeti, ndiko kulikogunduliwa masalia ya viumbe wa jamii ya watu wa kale yenye umri mkubwa kuliko yote yanayojulikana duniani hadi hivi sasa.
Kutokana na ugunduzi huo, wanasayansi duniani wanaamini kuwa Tanzania bara ni chimbuko la binadamu. Ushahidi wa kisayansi unatokana na nyayo za zamadamu zilizogunduliwa katika eneo la Laetoli lililoko kusini kidogo mwa Oltupai, umeongeza uzito wa hoja ya Tanzania kuwa chimbuko la binadamu.
Binadamu wa kwanza kuishi huko huaminiwa kuwa wawindaji wa jamii ya Wasani, halafu Wabilikimo.
Milenia za mwisho Kabla ya Kristo walihamia huko Wakushi kutoka kaskazini, nao wakameza kwa kiasi kikubwa wakazi asili, wakaingiza kilimo, ufugaji na uzalishaji kwa jumla.
Katika karne za kwanza BK walifika kwa awamu kutoka magharibi wahamiaji Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi. Nao wakameza kwa kiasi kikubwa wakazi waliotangulia.
Hatimaye Waniloti kutoka kaskazini walizidi kuingia hadi karne ya 18.