HISTORIA FUPI YA KOREA KASKAZINI

HISTORIA FUPI YA KOREA KASKAZINI

NI MTAZAMO TU

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2014
Posts
1,203
Reaction score
1,001
Korea Kaskazini kama nchi ya pekee ni tokeo la ugawaji wa Korea baada ya vita kuu ya pili ya dunia.

Korea ilikuwa koloni la Japan kuanzia 1910 hadi mwaka 1945. Kwenye mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia jeshi la Urusi liliwafuata Wajapani kaskazini mwa rasi na Wamarekani waliingia kusini.

Mwanzoni kulikuwa na majadiliano ya kuunganisha Korea tena lakini Vita Baridi ilileta uadui kati ya pande hizo mbili. Kila moja ilianzisha serikali ya pekee katika kanda la utawala wake kufuatana na itikadi yake. Warusi walitaifisha tasnia na ardhi wakaacha serikali ya kikomunisti katika kaskazini na Wamarekani waliacha uchumi wa kibepari na serikali iliyochaguliwa katika kusini.

Katika vita ya Korea iliyofuata Korea ya Kaskazini iliweza kudumu kwa sababu ya msaada msaada wa kijeshi wa China iliyomwaga askari milioni moja nchini.

Kiongozi Mkomunisti Kim Il-Sung alishika mamlaka akatawala kama dikteta kwa msaada wa chama cha kikomunisti na jeshi.

Alipokufa mwaka 1994 mwana wake Kim Jong-Il alichukua nafasi yake hadi alipofariki tarehe 17 Desemba 2011. Nafasi yake ilichukuliwa na mtoto wake Kim Jong-un.

Kim Il-Sung aliunda itikadi ya "Juche"; inaitwa falsafa ya kuendeleza Umaksi, lakini hali halisi ni itikadi inayotakiwa kutoa msingi kwa utawala wa kidikteta. Ingawa ilidai kutafuta maendeleo ya kujitegemea, Korea Kaskazini ilikuwa nchi iliyotegemea msaada kutoka Urusi kwa historia yake yote.

Baada ya mwisho wa Umoja wa Kisovyeti msaada huo ulikwisha na Korea Kaskazini iliingia katika kipindi kigumu sana kiuchumi.

Leo hii nchi haiwezi kulisha watu wakeː hutegemea usaidizi wa vyakula kutoka jumuiya ya kimataifa.

Udikteta katika Korea Kaskazini ni wa Kikomunisti kwa jina, lakini una tabia za kidini ndani yake. Kim Il-Sung alitangazwa kuwa "rais wa milele"; Kim Jong-Il hakutumia cheo rasmi isipokuwa "mwenyekiti wa kamati ya utetezi wa taifa" kinachomaanisha kitu kama "mkuu wa jeshi".

Katika mwaka 2006 Korea Kaskazini ililitekeleza mlipuko wa nyuklia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom