HISTORIA FUPI YA IBIN BATUTA

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,446
Ibn Battuta (1304-1377) kwa kiarabu inatamkwa (eebin bahtuta)
2af3685020fea902ca255f6b1528db09.jpg

Katika kitabu chake Ibin Batuta anaandika kwamba kiswahili ni lugha ambayo inazungumzwa na wakazi asilia wa upwa wa pwani ya Afrika mashariki kuanzia mto Juba uliopo Somalia mpaka maeneo ya MsumbujI.kwa miaka mingi sana historia ya Lugha hii imekuwa kwenye njia panda, juu ya asili na wapi Kiswahili kilianzia. Miongoni mwa watu ambao wamechangia sana kutoa ushahidi juu uswahili wa Kiswahili ni Ibin Battuta.Ibin Battuta alikuwa mwanafunzi wa kiislamu ambye alisafiri umbali wa Maili 75000 Sawa Na Kilomita 120000. Ibn Battuta alifanikiwa kutembelea nchi zote za Kiislamu na zile ambazo si za waislamu bali zilipata kukaliwa na waislamu, ambapo kwa kiarabu ziliitwa Dar Al-Islam.
3a4563e895ce0848e4e7542b44635e5b.jpg

Kwa ufupi Ibin Battuta alizaliwa nchini Moroko katika mji uliojulikana kama Tanja (Tangier). Na alipata elimu ya kiislamu katika Madrasa ( kama ilivyo kwa vijana wa kiislamu wanafanya) alipokuwa na miaka 21. Ibin Battuta alipata kuhiji Macca, (kama nguzo moja wapo ya dini la Kiislamu) na baada ya Hijja Battuta hakurudi Moroko na badala yake aliendelea kuingia ndani zaidi kutembelea nchi za kiislamu na baadae kujikuta akitokea nchi ya Hispania na kurudi kwao Moroko. Ibin battuta alifika Afrika msharaiki manamo miaka ya 1330 na kuandika habari mbalimbali alizoziona juu ya Waswahili.
05dfbb883baee88148131f32d1cb4a63.jpg

Ni miongoni mwa watu waliandika habari juu ya mji wa Kilwa wakati ukiwa chini ya Sultani Abu el Mazhafu Hasani. Mchango wa Ibn Batuta ulipatikana pale alipoandika historia yake iliyojikita sehemu kuu mbili yaani, historia ya jamii (social history)


Kupitia maandiko yake ndipo tukakuta historia juu juu ya utamaduni wa watu wa Zanzibar na jamii yao, wakati huo wa karne 13/14 palijulikana kama “Zanj” kwani alipotembelea maeneo hayo alikuta miji akiwa na majina yake, na vitu vilikuwa na majina yao ambavyo vilitamkwa kwa Lugha ya kiswahili, na pia alikuta watu wakiimba mashairi yao ya kusifu miji yao na viongozi wao kwa lugha ya kiswahili. Kwa Namna Hiyo Sisi Waafrika Tulikuwa Na Watu Ambao Waliandika Historia Yetu Hata Kabla Ya Ujio Wa Wazungu Hapa Afrika. Hii ndiyo historia fupi ya Ibn Batuta.
 
Plotemy myunani alifika pwani yetu 63ad na kukuta watu wamestaarabika na kupaita Azania au Rhapta
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom