Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 58,079
- 134,472
Ukifuatilia muhtasari wa hii hadithi ya Bilioni 90 (87) unachukia sana....
Tulipovunja mkataba wa kandarasi yao ya ujenzi wa barabara ya Wazo Hill hadi Bagamoyo (kibabe), Stirling Civil Engineering Ltd, wakatupeleka mahakamani.>>>> (TUKASEMA HATUTISHWI)
Tarehe 10 Desemba, 2009 - Mahakama ya Usuluhishi ya Paris ikaamuru tuwalipe fidia ya hasara tuliyowasababishia kwa kiburi chetu, ya dola za Marekani milioni 25 (Takribani Shilingi Bilioni 40 wakati huo) >>>> TUKAGOMA!
Serikali yetu ikakata Rufaa, tarehe 10 Juni 2010 hukumu ya rufaa ikasomwa, tukapigwa chini. Tukaamuriwa kuilipa kampuni hiyo fedha hizo vinginevyo kila mwaka mmoja utakaohesabiwa tutalipa na riba ya asilimia 8. >>>>TUKADHARAU!
Kutokana na ucheleweshaji wa malipo, deni hilo limeongezeka hadi dola za Marekani milioni 38.7 kufikia tarehe 30 Juni, 2017. Hii ni sawa na takribani shilingi Bilioni 90 za Tanzania. >>>> TUKAENDELEA KUGOMA!
Mwezi Julai 2017, kampuni inayotudai imekamata ndege yetu, 'Bombadier Dash Q400' - sharti la kurudishiwa ndege yetu (isipigwe mnada) ni sisi kulipa hizo shilingi bilioni 90. >>>> NDIYO TUMEKUMBUKA KUWAPIGIA MAGOTI!
[Tayari Waziri Mahiga amewaomba Stirling Construction tuwalipe Bilioni 30 (kama advance payment) waachie ndege yetu wakati mazungumzo mengine ya namna ya kumalizia deni lililobaki yakiendelea. Halafu kuna watu bila aibu wanasema Lissu ndiye sababu ya ndege yetu kukamatwa. Hivi Lissu anahusikaje hapa?]
Ninajiuliza hivi akili zetu tumemgawia mwekezaji gani?
Yani tunakwenda kuwalipa watu Bilioni 90, za bure [kwa uzembe wa mtu mmoja aliyevunja mkataba kwa kukurupuka.!]
Bilioni 90 ni sawa na Magari 3,000 ya Wagonjwa (Ambulances) na yangeliweza kugawiwa kila kata ya Tanzania.
Bilioni 90 ni sawa na matrekta 1,500 ya kisasa na tungeliweza kuyagawa kwa nusu ya kata za Tanzania na kwa miaka mitano idadi ya Makumi Elfu ya wakulima wangefaidika.
Bilioni 90 ni pesa nyingi sana, mno! Lakini zinakwenda kupotea hivi hivi, na wanaoohusika na kiburi kilichopelekea hasara hii siyo tu kwamba wamekataa kujiuzulu au kuomba radhi! Bali wanatumia nguvu kubwa zaidi kutaka umma uamini kuwa wao ni "watakatifu" na "hawafanyi makosa makubwa kama haya."
Tungekuwa na watu wenye utu wangelitoka hadharani, wangekiri makosa yao, wakajiuzulu na kuomba wasishtakiwe. Kinyume chake, waliotutia hasara hii ndo wako mstari wa mbele kuwatisha waliofichua KASHFA hii.