Hispania yateua Waziri wa masuala ya Ngono

Bahati furaha

JF-Expert Member
Jul 11, 2012
3,053
1,409
_94923171_uhispania.jpg

Katika juhudi za kuongeza idadi ya watu inayoendelea kupungua, nchini Uhispania sasa serikali imeamua kumteua waziri wa masuala ya ngono.

Waziri mkuu wa nchi hiyo Mariano Rajoy amethibitisha uteuzi wa Edelmira Barreira kuwa afisa mkuu wa masuala ya ngono.

Hatua ya kubuni wizara nzima ya maswala ya ngono na mahaba huko Uhispania imetokana na hofu waliyo nayo wanasiasa.

Wakati kwengineko duniani watu wana hofu kwamba idadi ya watu nchini mwao inaongezeka kushinda rasilmali zilizopo , huko Spain hofu ni kwamba idadi ya watu inapungua, tena kwa kasi ya kutisha.

Mbali na kwamba wengi ya wanandoa huko nchini humo wanashiriki zaidi mbinu na mipango ya uzazi pia kutokuwa na nafasi muafaka wa wanandoa au hata wapenzi kuonana kimwili, kuna laumiwa kwamba ndiko kulikosababisha idadi ya watoto wanaozaliwa kupungua mno.

Takwimu za hivi karibuni za Umoja wa Mataifa zinaorodhesha Uhipania kama moja wapo ya mataifa yanayoongoza kwa kuporomoka kwa idadi ya watoto wanaozaliwa.

Nae waziri wa elimu hivi majuzi amewasilisha ripoti yake kwa serikali na baraza la mawaziri akilalamika kwamba madarasa ya shule hayana idadi ya kutosha ya watoto na akaonya kwamba hili huenda likaathiri Uhispania kiuchumi katika miaka ijayo.

Katika kushghulikia swala hilo kwa haraka waziri mkuu wa taifa hilo Mariano Rajoy amemteua Bi Edelmira Barreira kuwa waziri wa maswala ya ngono na mahaba

Kazi kubwa ya waziri huyo mpya ni kuja na mbinu za mikakati ya kuwahamasisha na kuuchochea umma wa Uhispania kurudi vitandani na kusaidia kutengeneza watoto ili kuijaza tena Uhispania.
 
Ujerumani na Italia pia zina tatizo hili!! Nakumbuka enzi za mwisho za uhai wa papa john Paul 2 aliwahamasisha Italians kuongeza bidii ya kufyatua ili kulinda kizazi cha waitaliano kinachopungua kila uchao
 
View attachment 476543

Katika juhudi za kuongeza idadi ya watu inayoendelea kupungua, nchini Uhispania sasa serikali imeamua kumteua waziri wa masuala ya ngono.

Waziri mkuu wa nchi hiyo Mariano Rajoy amethibitisha uteuzi wa Edelmira Barreira kuwa afisa mkuu wa masuala ya ngono.

Hatua ya kubuni wizara nzima ya maswala ya ngono na mahaba huko Uhispania imetokana na hofu waliyo nayo wanasiasa.

Wakati kwengineko duniani watu wana hofu kwamba idadi ya watu nchini mwao inaongezeka kushinda rasilmali zilizopo , huko Spain hofu ni kwamba idadi ya watu inapungua, tena kwa kasi ya kutisha.

Mbali na kwamba wengi ya wanandoa huko nchini humo wanashiriki zaidi mbinu na mipango ya uzazi pia kutokuwa na nafasi muafaka wa wanandoa au hata wapenzi kuonana kimwili, kuna laumiwa kwamba ndiko kulikosababisha idadi ya watoto wanaozaliwa kupungua mno.

Takwimu za hivi karibuni za Umoja wa Mataifa zinaorodhesha Uhipania kama moja wapo ya mataifa yanayoongoza kwa kuporomoka kwa idadi ya watoto wanaozaliwa.

Nae waziri wa elimu hivi majuzi amewasilisha ripoti yake kwa serikali na baraza la mawaziri akilalamika kwamba madarasa ya shule hayana idadi ya kutosha ya watoto na akaonya kwamba hili huenda likaathiri Uhispania kiuchumi katika miaka ijayo.

Katika kushghulikia swala hilo kwa haraka waziri mkuu wa taifa hilo Mariano Rajoy amemteua Bi Edelmira Barreira kuwa waziri wa maswala ya ngono na mahaba

Kazi kubwa ya waziri huyo mpya ni kuja na mbinu za mikakati ya kuwahamasisha na kuuchochea umma wa Uhispania kurudi vitandani na kusaidia kutengeneza watoto ili kuijaza tena Uhispania.
Nahamia hispania
 
Hacha kupoteza maana au lugha tatizo! Huyo waziri sio kwa maana mnayofikiria bali ni kusimamia sera za kuongeza birth rate na si ngono kama mnavofilia shina watanzania mkiona sex mnaichukulia hovyo
 
Back
Top Bottom