Nipo zangu saluni napunguza nywele zangu na low cut ndo staili yangu,mara anaingia mwamba mmoja,ile kuingia lawama zote kwa spain
Alisikika akisema "Spain jana wameniangusha kweli yani sina hata raha" awali sikumuelewa huyu mwamba,nikajiuliza huyu mtu wa namtumbo na kuangushwa na Spain wapi na wapi
Baada mazungumzo kuendelea ndio nikajua kumbe mkeka ulichanika usiku wa jana yake,na mwamba kapoteza rasilimali fedha yake
Wadau kamali haijawahi kumwacha mtu salama,kula utakavyo kula lkn tambua kamali haita kuacha salama,ndio maan si ajabu ikaitwa miongoni mwa kazi za shetani,na uraibu wake ni mbaya mno
Kutoka kwa watu wa karibu wa mwana hip hop mmoja ambaye akifanya featuring na mwana hip hop mmoja mwenye jina linalo fanana na imani fulani ya dini ambaye kiongozi wao yupo vatican,huwa nyimbo zao huwa kali sana,na ambaye alimuoa madam mmoja kutoka east africa,inasemekana chanzo cha ndoa yake kuanguka ni kamari,huyo mwana hip hop unaambiwa kamari kwake kama dini.
Mke kila siku malalamiko kwa mumewe kuwa baby dady hala hala achana na kamari mwamba haelewi,mwisho wa siku madam akajiweka kwa mchezaji mpira mmoja,ishu ilikuwa kamari yaan hizo ni za ndani kabisa.
Kwahiyo tujitahidi sana kuachana na kamari,kwani mwisho wake ni mbaya kwako binafsi kwa familia yako na jamaa zako pia
Hivi nilikuwa naongelea nini vile
Ni hayo tu!