HISIA ZANGU: Nani anajali alipo Hassan Dilunga?

Nani pia nani anajali alipo Ditram Nchimbi mchezaji aliekuwa muhimu kwenye timu ya Taifa? Wachezaji wetu wanapotea kizembe zembe sana.Dilunga what a player!
Huyu walimuonesha amekuwa dereva boda
 
Huu ushauri wako utumike hata kwenye ndoa pia, huu sio ulimwengu wa kuoneana huruma....mtu unahitaji kuwa katili kusimamia maslahi yako.
Aiseee ndoa si biashara, ni muunganiko wa watu waliokubaliana
 
Kabisa una mke ndani analala muda wote achana nae tafuta mpya, una mke hajiwezi tupa mbali huo ndio ushauri mzuri

Au unajishaua kumsomesha mke au mume, Kama hajasomeshwa kwao atajijua, hapa kafata ndoa sio scholarship, majukumu ya ndoa yakimshinda unapiga chini.

Ndoa pia ni mkataba Kama mikataba mingine.....tukifuata ushauri huu wa kila mmoja kusimamia maslahi yake hata mauji yatapungua.
 
Fei toto anakenua meno tu wakati yupo kwenye peak lakini husikii hata tetesi za kuhama anafikiri utopolo ni baba yake, hawajifunzi kwa Ngasa.
Sijui maisha yake uko zenji ila hapa bara namuonaga na ki IST cheupe kimepigwa chata kila kona FEI TOTO mwanzo nilifikiri ni cha biashara ila kumbe ni chake cha mizunguko sasa Kwa hadhi ya Mchezaji kama yeye hapa bongo inabidi awe anamaisha ya Uhakika Ndinga ya maana kwakwel Naunga mkono hoja wachezaji wetu wajitathmini sana

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
NDIVYO ukweli wa maisha ulivyo, hasa katika dunia ya kibepari. Nani anajali alipo Hassan Dilunga maarufu kwa watangazaji wa Azam kama ‘HD’ ? Miezi 24 iliyopita alikuwa wa moto hasa. Halafu baadaye akaumia. Akaanza kujiuguza.

Akiwa ndani ya majeraha mkataba wake ukakata roho. Simba ikachukua maamuzi mazuri kwa maslahi ya klabu yao wakaachana naye. Huwezi kuwalaumu Simba. Mkataba wa Dilunga ulikuwa umeisha na hauwezi kumuongezea mkataba mchezaji ambaye ana majeraha ya muda mrefu.

Kuna watu wanaishi katika dunia ya kijamaa walitaka Dilunga aongezewe mkataba halafu aendelee kutibiwa. Dunia ya kibepari haipo hivi. Simba walichukua maamuzi sahihi kwa maslahi ya klabu yao. Nafasi ya Dilunga ingejazwa na mchezaji mwingine na maisha yangeendelea.

Lakini kinachochekesha zaidi ni kwamba hata leo wakati baadhi ya mashabiki wanapobishana kuhusu uwezo wa Kibu Dennis au Ousmane Sakho huwa hawamkumbuki Dilunga. Hawaulizii kama anakaribia kupona. Hawaulizi chochote. Wanataka wachezaji wapya wachukue nafasi Januari au mwisho wa msimu.

Najua Dilunga au watu wake wa karibu watakuwa wanalalamika kwamba Simba imemtelekeza. Narudia, Simba wapo sahihi na soka ni mchezo wa kikatili ndani na nje ya uwanja. Wachezaji wetu ndio wanakosa ukatili nje ya uwanja.

Nje ya uwanja wachezaji wetu wanageuzwa kuwa mashabiki wa hizi timu. Wanapokuwa wa moto huwa wanafanya makosa matatu. Kosa la kwanza ni pale wanaposaini mkataba huku wakiwa wanagombewa. Mchezaji anaweka wazi kwamba anatamani kwenda Yanga. Huwa hajiweki katika mnada. Matokeo yake Yanga wakijua basi anasajiliwa kwa dau la chini.

Mfano ni Salum Aboubakary ‘Sure Boy’. Watu wote walijua hatima yake ingekuwa kuishia Yanga. Hata alipoingia katika matatizo na Azam, Yanga walijiona salama na Simba hawakutaka hata kuingiza kucha zao. Wachezaji hao wanapatikana zaidi Tanzania tu.

Kule kwa wenzetu mchezaji anaweza kutamani timu fulani lakini kwa sababu tayari anajua dau analoenda kupata. Huku tulifahamu Sure Boy ni Yanga kwa muda mrefu ingawa alikuwa anavaa jezi ya Azam. Haya ni miongoni mwa makosa ambayo wachezaji wetu wanayafanya.

Kosa la pili ambalo wachezaji wetu wanafanya ni pale wanaposaini mkataba mwingine wa kuendelea kuitumikia klabu. Wanageuzwa kuwa mashabiki wa timu hizi. Klabu inakuwa haina wasiwasi na mchezaji husika kwa sababu mchezaji anajifunga kimaneno na kimatendo kwa viongozi.

Mchezaji haonyeshi kama anaelekea kuwa huru au ana mawazo ya kuhamia kwingine. Kitendo hiki kinamshushia dau lake yeye mwenyewe. Wakati haya yanatokea anakuwa yuko fiti na anajiona ni mfalme katika klabu husika.

Wenzetu huwa wanavunja uhusiano wao na klabu na kuangalia kwanza maslahi yao. Hata wale waliokuzwa klabuni katika nyakati kama hizi wanazisikiliza zaidi menejimenti zao kuliko wanavyozisikiliza nyimbo tamu za viongozi.

Unajikuta unajiuliza maswali kadhaa. Arsenal wamemlea Bukayo Saka tangu akiwa na miaka saba lakini leo kwa muda mrefu yupo katika mazungumzo ya mkataba mpya na Arsenal. Ingekuwa Tanzania kingekuwa kitu rahisi tu kumwambia ‘Saka tumekulea wenyewe unashindwa kutuelewa kitu gani?’

Ni vivyo hivyo nyakati zile nilipokuwa nasikia kwa zaidi ya miezi sita Liverpool ilipokuwa katika mazungumzo na kiungo wao, Steven Gerrard. Ni kiungo waliyemlea na ingekuwa rahisi tu kusema ‘Gerrard tumekulea wenyewe hapa lakini kwanini unatuhangaisha?’

Kumbe maisha hayaendi hivi. Unalazimika kuwa katili katika maamuzi yako kwa sababu hata kuna nyakati ambazo klabu itakuwa katili dhidi yako ingawa itakuwa imesimama katika upande wa haki yao. Ni kama Simba ilivyosimama katika upande wa haki yao katika sakata la Dilunga.

Wachezaji wetu wajikite katika kujali maslahi yao zaidi wakati wanacheza kwa sababu wao sio mashabiki, ni watumishi wa klabu. Nashukuru kuna wachezaji wa kigeni ambao miaka ya karibuni wamekuwa wakiwafundisha wachezaji wetu wazawa kuishi hivi.

Alikuwepo Emmanuel Okwi kisha Clatous Chotta Chama. Simba ilipotaka kutanua mikataba ya mastaa hawa maisha hayakuwa rahisi kwao. Walitenganisha utumishi na ushabiki na wakafanikiwa kupata mikataba minono zaidi.

Sijui kama hali ya kiuchumi ya Dilunga ipo vipi lakini ninachojua ni kwamba muda si mrefu haitakuwa nzuri tofauti na vile alivyokuwa anacheza. Ninachojua ni kwamba yaliyomtokea Dilunga kama yakimtokea Chama leo bado ana nguvu kubwa ya kiuchumi kutokana na kujitambua kwake.

Jambo jingine la tatu ambalo wachezaji wanapaswa kuliangalia ni suala la bima. Kumbe maisha yanaweza kwenda kasi hivi kwa mchezaji. Ikumbukwe Dilunga hachezi tena kwa sasa kwa sababu ya majeraha na sio uzee au kushuka kwa kiwango.

Kwa wachezaji wa wenzetu huwa wanakatiwa bima au wanakata wenyewe. Bima yao inaweza kueleza utaendelea kulipwa kwa miaka miwili au mitatu endapo utapata majeraha ambayo yatakwamisha ghafla uwezo wako wa kiutendaji uwanjani.

Sijui kama Dilunga alikuwa na bima ya namna hii lakini kama hana basi ni kitu ambacho wengine wanapaswa kujifunza kutoka kwake. Tatizo kubwa kwa wachezaji au raia wa kawaida wa nchi inayoitwa Tanzania ni kwamba wakati mwingine huwa wanadhani kuweka bima ni kutabiri matatizo. Sio kweli, matatizo yapo tu na ni kama tunavyoona kwa Dilunga au kwa mchezaji kama Gerard Mdamu wa Polisi Tanzania.

Wachezaji wetu waweke bima za afya zao kila wakati. Najua klabu zetu huwa zinafanya geresha katika jambo hili lakini hili ni suala la mtu binafsi na familia yake.

Nafahamu kina Sergio Aguero wanalipwa kiasi kikubwa cha pesa kama bima baada ya kushindwa kuendelea kucheza soka kutokana na matatizo ya kiafya.

Nafahamu kwamba familia ya Marc-vivien Foe ililipwa pesa nzuri baada ya staa huyu wa kimataifa wa Cameroon kufia uwanjani Ufaransa mwaka 2003. Wachezaji wetu waanzishe utaratibu huu na hapana shaka utawasaidia katika siku za usoni.

Source : Mwanasport​
Yanga ilifanya hivi kwa yacouba sogne na balama mapinduzi nafikiri simba ili kulinda image ya klabu wangefanya uungwana tu kumpa mkataba alafu kutemana nae pale atakapopona kabisa
 
Fei toto anakenua meno tu wakati yupo kwenye peak lakini husikii hata tetesi za kuhama anafikiri utopolo ni baba yake, hawajifunzi kwa Ngasa.
Kipindi anasaini mkataba wa sasa alikua bado hana jina kubwa kama alilonalo sasa hivi nafikiri huo mkataba utakua umebaki mwaka mmoja tu kwaiyo huo mkataba ujao inabidi awakamue pesa ndefu pale yanga aziz ki na morrison wanamzidi mshahara karibu mara 3 wakati yeye mchango wake ni mkubwa zaidi
 
Hili andiko apelekewe kila mchezaji alisome. Mpira ni ajira/biashara tofauti yake tu ina kikomo cha lazima. Wachezaji waache huruma kwa vilaby wanapokuwa kwenye peak. Mrisho Ngassa watu walifunga safari kutoka Sudani akaishia kujificha na kubaki Yanga. Jerry Tegete hivyo hivyo. Mpira wa miguu ni ukiwa kwenye kiwango cha juu tu tofauti na hapo si kitu.
 
Fei toto anakenua meno tu wakati yupo kwenye peak lakini husikii hata tetesi za kuhama anafikiri utopolo ni baba yake, hawajifunzi kwa Ngasa.
Nadhani Feitoto alifanyia kazi ushauri wako. Hassan Dilunga ameanza kupasha na Simba

0c9e5b01-32ba-43b9-a998-e87d664cebd4-jpeg.2551385
...
231e2114-7735-4659-8038-b39328e5f536-jpeg.2551382
 
Back
Top Bottom