Msamiati wa hesabu/hisabati unaangazia: majina mbalimbali ya tarakimu/nambari; kuandika tarakimu kwa herufi.maneno; tarakimu za kiarabu; akisami (fractions) na asilimia (percentages).
Tumekuandalia:
- Nambari za Kimsingi (0-9) Kiswahili na Kiarabu
- Kumi na (11-19) Kiswahili na Kiarabu
- Makumi/Ukumi (10-90)
- Akisami (fractions)
- Mifano Kadhaa
NAMBARI ZA KIMSINGI
Haya ni majina ya tarakimu mbalimbali zinapoandikwa kwa herufi (badala ya nambari) yenye asili ya Kiswahili/Kibantu na pia yale yenye asili ya Kiarabu. Pia, tumeongezea majina ya makumi mbalimbali (10-90)
| TARAKIMU | KISWAHILI | KIARABU | | 0 | sufuri | sufuri | | 1 | moja | wahed | | 2 | mbili | thenini | | 3 | tatu | thelatha | | 4 | nne | aroba | | 5 | tano | hamsa | | 6 | sita | sita | | 7 | saba | saba | | 8 | nane | themania | | 9 | tisa | tisa |
KUMI NA
Majina ya ya tarakimu kutoka (11-19) kwa Kiswahili na kwa Kiarabu.
| 10+ | KISWAHILI | KIARABU | | 11 | kumi na moja | edatashara | | 12 | kumi na mbili | thenashara | | 13 | kumi na tatu | thelathashara | | 14 | kumi na nne | arobatashara | | 15 | kumi na tano | hamsatashara | | 16 | kumi na sita | sitatashara | | 17 | kumi na saba | sabatashara | | 18 | kumi na nane | themantashara | | 19 | kumi na tisa | tisatashara |
MAKUMI
Kuandika tarakimu mbalimbali katika hali ya ukumi. (11-99).
| *10 | JINA | MFANO | | | | # | KISWAHILI | KIARABU | | | | 10 | kumi | 12 | kumi na mbili | thenashara | | 20 | ishirini | 27 | ishirini na saba | saba wa ishirini | | 30 | thelathini | 32 | thelathini na mbili | thenini wa thelathini | | 40 | arobaini | 42 | arobaini na mbili | thenini wa arobaini | | 50 | hamsini | 52 | hamsini na mbili | thenini wa hamsini | | 60 | sitini | 61 | sitini na moja | wahed wa sitini | | 70 | sabini | 76 | sabini na sita | sita wa sabini | | 80 | themanini | 89 | themanini na tisa | tisa wa themanini | | 90 | tisini | 93 | tisini na tatu | thelatha wa tisini |
AKISAMI
Akisami hutumiwa kuonyesha sehemu ya kitu kizima. Kwa mfano, ukigawa kilo moja kwa visehemu vinne vinavyotoshana, kila kisehemu kitakuwa na uzani wa robo kilo ( sehemu ya nne au moja kwa nne ) ya kilo.
| 1/# | JINA | MFANO | | | | 1/2 | nusu | 1/2 | nusu | moja kwa mbili | | 1/3 | thuluthi | 2/3 | thuluthi mbili | mbili kwa tatu | | 1/4 | robo | 2/4 | robo mbili | mbili kwa nne | | 1/5 | humusi | 3/5 | humusi tatu | tatu kwa tano | | 1/6 | sudusi | 4/6 | sudusi nne | nne kwa sita | | 1/7 | subui | 6/7 | subui sita | sita kwa saba | | 1/8 | thumuni | 7/8 | thumuni saba | saba kwa nane | | 1/9 | tusui | 3/9 | tusui tatu | tatu kwa tisa | | 1/10 | ushuri | 6/10 | ushuri sita | sita kwa kumi | | 1/100 | asilimia | 72/100 | asilimia sabini na mbili | sabini na mbili kwa mia moja |
MIFANO ZAIDI
- Andika nambari zifuatazo kwa maneno/herufi:
- 3 ⇒ tatu
- 952 ⇒ mia tisa hamsini na mbili
- 680 ⇒ mia sita themanini
- 4521903 ⇒ milioni nne, na mia tano ishirini na moja elfu, na mia tisa na tatu
- 556100016 ⇒ mia tano hamsini na sita milioni, na mia moja elfu, na kumi na sita
- Andika tarakimu zifuatazo kwa nambari
- sufuri ⇒ 0
- mia tatu ishirini na mbili ⇒ 322
- sabini na tatu elfu, na mia nane hamsini na tano ⇒ 73855
- mia tano sabini na nane elfu, na mia tatu hamsini na tisa ⇒ 578359
- mia sita tisini na sita milioni, na mia tisa tisini na nane elfu, na mia saba ishirini na tatu ⇒ 696998723
- Andika akisami zifuatazo kwa maneno
- 240/295 ⇒ mia mbili arobaini kwa mia mbili tisini na tano
- 41/45 ⇒ arobaini na moja kwa arobaini na tano
- 26/51 ⇒ ishirini na sita kwa hamsini na moja
- 59/74 ⇒ hamsini na tisa kwa sabini na nne
- 1/3 ⇒ thuluthi
|